Okra Agustine amfuata mwenzake Mkude Yanga

Okra Agustine amfuata mwenzake Mkude Yanga

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ila utopolo....
Screenshot_2023-12-28-18-58-57-35.jpg
 
Usajili mzuri, ukilinganisha na mawinga waliopo Yanga. Sijawahi kuelewa kwa nini Simba walimkatia tamaa kirahisi.
Mchezaji mzuri na hakustahili kuachwa na Simba ila pia wachezaji wafupi nao kuna vitu wanashindwa kukupa. Mpira wa kisasa timu zinategemea sana set pieces na wachezaji wafupi wanakuwa hawana faida sana. Matokeo yake wachezaji kama Saidoo ili aonekane ana umuhimu, analazimisha apige kila kona na faulo wakati amedhihirisha siyo mpigaji mzuri wa mipira hiyo ukiacha penati.
 
Mchezaji mzuri na hakustahili kuachwa na Simba ila pia wachezaji wafupi nao kuna vitu wanashindwa kukupa. Mpira wa kisasa timu zinategemea sana set pieces na wanakuwa hawana faida sana. Matokeo yake wachezaji kama Saidoo analazimisha apige kila kona na faulo wakati amedhihirisha siyo mpigaji mzuri wa mipira hiyo ukiacha penati.
Sijaelewa unataka kumaanisha nini?
Kwamba wachezaji wafupi hawajui kupiga set pieces? Au ulikuwa unamaana gani?
 
Kwa sababu ya ufupi wanakuwa siyo tegemeo sana kucheza mipira ya juu, siongelei kupiga. Saidoo anakimbilia kupiga kona na free kicks kwa sababu anajijua hana msaada sana kuicheza kwa kichwa
Ingekuwa timu inaangalia set pieces tu wangekuwa wanasajili mangongoti tupu, yule kondeboy aliyekuwa anaisadia Simba kipindi hicho kabla ya kwenda Al Ahly alikuwa ni tall?
 
Husi conclude tetesi kwani hiyo michuano kuna wachezaji kibao walikuja kufanyiwa majaribio na wakaachwa.
 
Ingekuwa timu inaangalia set pieces tu wangekuwa wanasajili mangongoti tupu, yule kondeboy aliyekuwa anaisadia Simba kipindi hicho kabla ya kwenda Al Ahly alikuwa ni tall?
Sijasema wachezaji wote wafupi hawafai. Kwa timu za level ya Simba, ukiwa mfupi inabidi uwe na kipaji cha hali ya juu sana na mchango wako uwanjani uwe juu sana kiasi kwamba ufupi wako unakuwa siyo ishu. Bila kwenda EPL, niambie mchezaji wa kimo cha Okrah anayechezea Al Ahly, Mamelodi au Wydad
 
Mchezaji mzuri na hakustahili kuachwa na Simba ila pia wachezaji wafupi nao kuna vitu wanashindwa kukupa. Mpira wa kisasa timu zinategemea sana set pieces na wachezaji wafupi wanakuwa hawana faida sana. Matokeo yake wachezaji kama Saidoo analazimisha apige kila kona na faulo wakati amedhihirisha siyo mpigaji mzuri wa mipira hiyo ukiacha penati.
Penalty yenyewe mpaka arudie kupiga mara mbili
 
Ingekuwa timu inaangalia set pieces tu wangekuwa wanasajili mangongoti tupu, yule kondeboy aliyekuwa anaisadia Simba kipindi hicho kabla ya kwenda Al Ahly alikuwa ni tall?
Baada ya kuisaidia Simba , vipi ilifika malengo?

Mimi sijafurahishwa ujio wa kiburushuti Okrah kwenye klabu yangu ya Yanga.

Soka la kisasa linahitaji mchezaji mrefu.

Msimu uliopita US Monastir ya Tunisia ilitufunga bao mbili za haraka haraka kule kwao, na mabao yote ni kwasababu mabeki wetu ni wafupi.
 
Okrah
Moloko
Kibwana
Kibabage
Sureboy
Farid
Job
Nkane
 
Mchezaji mzuri na hakustahili kuachwa na Simba ila pia wachezaji wafupi nao kuna vitu wanashindwa kukupa. Mpira wa kisasa timu zinategemea sana set pieces na wachezaji wafupi wanakuwa hawana faida sana. Matokeo yake wachezaji kama Saidoo analazimisha apige kila kona na faulo wakati amedhihirisha siyo mpigaji mzuri wa mipira hiyo ukiacha penati.
Vipi kubabage
 
Ila huyu mchezaji alikuwa ni hatari sana wakati anasajiliwa simba. Na kwa upande wangu nilikuwa namhofia sana wakati alipocheza kwenye ile michezo ya derby.

Naamini kama taarifa ni ya kweli, basi anaweza kuisaidia Yanga kwa upande wa pembeni. Maana ni aina ile ya viungo washambuliaji wachache wa pembeni wenye ujasiri wa kuwafuata mabeki. Muhimu tu asiwe majeruhi.
 
Back
Top Bottom