Okra magic acheze namba ya Max Nzengeli ili kuongeza kasi ya mashambulizi

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920

Baada ya kuwa majeruhi karudi tena uwanjani, nimeiona kasi yake, Okra anakasi sana pia ni mpiga krosi mzuri hajui kuremba, combination ya Okrah na guede imetiki.

Maana Guede ni mzuri kwenye vichwa, nzengeli akae benchi ili Waarabu wafe kwa mkapa
 
Max anafanya kazi nyingi sana kwa wakati mmoja, kwenye beki yupo, kiungo yupo, kwenye ushambuliaji yupo.
huko kwenye match za klabu bingwa anakuaga kama vile hayumo anamalizaga hata dakika ishirini bila kupiga krosi mpaka pacome ndio anaanza kufanya kazi ya ushambuliaji kwa kukokota mpira kuupereka kati kisha kupiga mashuti , okrah atatufaa ikiwezekana wagawane dakika au nzengeli akae benchi mwanzo mwisho
 
Mimi nashauri waanze wote tu pale mbele ili kuleta maafa kwa Mwarabu. Yaani Pacome, Okrah, Nzengeli, Aziz Kii, Mzize, Mudathir, na Aucho.

Halafu kule nyuma Mwamnyeto tu ndiyo aangaliwe kwa jicho la karibu. Maana hatabiriki.
sasa mkuu makianza wote okrah atacheza namba ngapi?
 
sasa mkuu makianza wote okrah atacheza namba ngapi?
Okrah anacheza 7, Pacome 11, Aziz Kii 10, Mzize 9, Nzengeli 8, Aucho 6, na Mudathir ataanzia nje ili hesabu ya wachezaji 11 ikamilike.
 
Mimi nashauri waanze wote tu pale mbele ili kuleta maafa kwa Mwarabu. Yaani Pacome, Okrah, Nzengeli, Aziz Kii, Mzize, Mudathir, na Aucho.

Halafu kule nyuma Mwamnyeto tu ndiyo aangaliwe kwa jicho la karibu. Maana hatabiriki.
Hii timu itabaki na beki wawili, Mkuu unataka kuwa profesa wa soka uvumbue mifumo?
 
Hii timu itabaki na beki wawili, Mkuu unataka kuwa profesa wa soka uvumbue mifumo?
Nimerekebisha hapo juu baada ya kugundua nimeweka viungo wengi. 😁

Ila kimsingi ili kuwadhibiti Waarabu hiyo Jmosi, ni lazima kocha apange viungo wengi washambuliaji, na pia wenye sifa ya kumiliki mpira.
 
Okrah kama atakuwa amejifunza kweli kuacha ubinafsi na kucheza kitimu atakuwa asset kubwa pale Yanga.
Jana kacheza kama mchezaji wa kawaida anayepambania timu badala ya sifa binafsi. Mambo ya masifa ndiyo yalimponza akiwa Simba.

Nimependa pia mguu wake dhaifu wa kulia ulivyokuwa na nguvu na shabaha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…