Okrah aiponza Yanga, yapewa siku 45 kuilipa Bechem United Mil. 216

Okrah aiponza Yanga, yapewa siku 45 kuilipa Bechem United Mil. 216

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Shirikisho la soka duniani ( FIFA ) limeitaka klabu ya Yanga kuilipa kiasi cha USD 80,000 sawa na Tsh Milioni 216 klabu ya Bechem United ya nchini Ghana ,pesa ya malipo iliyosalia katika uhamisho wa Augustine Okrah kutoka Bechem United kwenda Yanga.

FIFA imeitaka klabu ya Yanga kulipa pesa hiyo ndani ya siku 45 kuanzia sasa.

Soma Pia:Yanga yaachana na Okrah baada ya kuishia kufunga goli 1
 
Mbona imekuwa ghafla sana, okrah aliachana na Simba na kusajiliwa na timu nyingine kumbe kabla ya kuja utopoloni.......!
 
Ni mambo ya kawaida kama unahitaji kuimarisha kikosi, unatoa mchezaji aliye Bora anaingia Bora zaidi.
Tahasisi kudaiwa ni jambo la kawaida.
Kwa namna inavyodaiwa inatoa picha kuwa Uto inaendeshwa kiuswahili swahili.Tangu enzi za Mkapa Karibia kila msimu Uto inakuwa na kesi dhidi ya makocha wao waliopita au wachezaji na bado klabu haina maendeleo yoyote ya kujivunia.
 
Kama Barca na Madrid Wana madeni una shangaa vip kwa Yanga!!
 
Back
Top Bottom