Uchaguzi 2020 Oktoba 2020 - Hali inaonesha Magufuli kushinda kwa zaidi ya asilimia 90, wabunge na madiwani wakutosha

Tusibabaishane. Maneno haya yote ya nini? CCM ina kete moja tu itakayoipa ushindi wa asilimia 100. Nikuhakikisha mazingira ya sasa ya kutokuwa na tume huru ya uchaguzi na kutokuwa na katiba mpya yanaendelea. Hapo ushindi ni dhahiri hata kabla ya uchaguzi.
 
Siyo kweli mleta mada
My Raise atashinda kwa asilimia 100.Viti vyote vya ubunge na udiwani vitaenda CCM.Baada ya halo utaona uchumi utakavyopaa,Tanzania itakuwa zaidi ya Marekani,tutakuwa wafadhili Wa miradi mikubwa huko ulaya.
 
Ungesema tu zaidi ya 100% ili Moyo wako na MATAGA wengine muendelee kufurahi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalali hawezi shinda, kimbinu zenu za goli la mkono atashida,maana mnabebwa na dora
 
Tume ya CCM, wanaohesabu kura CCM, wanaotangaza matokeo CCM.hata ingekuwa mimi nashinda uchaguzi.
 

Sasa mnapunguza asilimia. Si mlisema atapitan kwa 100%, iweje leo ifike 90. Jiangalie, utafatwa weyeeeee.
 
Bila uchaguzi justification (Uhalali) wa serikali unapatikana vipi? Uchaguzi ni takwa la kikatiba ni lazima twende hivyo hivyo..na tume hii hii kwani tusipofanya uchaguzi mataifa watatutenga na tutaonekana sisi ni madikteta mtuelewe wadanganyika.
Ikiwa jaji Lubuva aliwahi kusema kwenye mfumo huu tulionao huwezi kuwa na tume huru, ikiwa tume inateuliwa na Raisi aliyepo madarakani unafikiri huo ni uchaguzi au ni uchafuzi.
 
Mimi ambacho huwa najiuliza kila siku ni swali hili: Kama kweli kazi iliyofanywa na CCM inaonekana, sasa harakati zote za kuhonga madiwani na wabunge wa upinzani na kuwapitisha kugombea bila kuwa na mpinzani ndani ya CCM ni za nini? Matumizi ya polisi kwenye uchaguzi ni ya nini? Hofu ya kuwa na katiba mpya ni ya nini? Hofu ya kuwa na tume huru ya uchaguzi ni ya nini? Kampeni za 'kufa mtu'ni za nini? Yaani ukiitishwa uchaguzi hata wa diwani wa kata tu ni tabu tupu, mavyombo yote ya dola yanahamia hapo kwenye eneo la uchaguzi. Kwa nini? Hofu ya nini jamani nyie CCM wakati mnasema mmetekeleza ilani vizuri na kazi inaonekana kwa sisi wananchi.
 
Mkuu October ni mbali sana,acha tupiganie uhai kwanza,anything can happen anytime
 
Analysis bila data ni C'RAP
 
Naunga mkono hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu upuuzi ingekuwa vyema ungeupeleka kwenye Uhuru na Mzalendo wakachapishe huko. Kwa kifupi ccm kupitia vyombo vyake vya ukandamizaji watajitangaza kushinda kama inavyofanyika kila uchao huku Bara na kule Zanzibar. Hatujasahau ile kauli ya yule malaika "nikuteue mimi, nikulipe mshahara mimi, nikupe gari mimi na nikuwekee mafuta mimi, halafu umtangaze mpinzani!?" Hii kauli maana yake matakwa ya malaika ndiyo yatimizwe hata pale wananchi ambao kwao ndiko madaraka yanatoka wataamua vinginevyo.
 
Atashinda au atajishindisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama Hali ingekua hivi unazani kungekua na haja ya NCCR kuwa agent WA political slave trade
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…