Okwi aomba radhi Msimbazi, aapa kufa na Singida United

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Taarifa nilizonyapianyapia na za motomoto ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa Mganda Emmanuel Arnold Okwi ameomba radhi kwa kocha na viongozi wa simba pamoja na mashabiki huku akidhamiria kumaliza ukame wa magoli unaokumba klabu hiyo kwa sasa.

Okwi ambaye ameungana na kikosi hicho juzi akitokea nchini Uganda ambapo mara kadhaa kocha wa Simba Msoud Djuma amekuwa akimshutumu kwa kushindwa kusaidia klabu yake hasa katika michuano ya kombe la mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar.

Katika hatua nyingine kikosi cha Simba leo kinarejea jijini Dar Es salaam kutoka huko Morogoro tayari kwa pambano lake litakalofanyika hapo kesho tarehe 18/01/2018 kwenye uwanja wa Taifa.

Okwi ni Sithole,
Na ndomana alishindwa kucheza mpira Sweden na Tunisia anajua kuzchezea Simba/Yanga
 
Simlaumu Okwi nawalaum waliomsajili Okwi nadhani kipo walichokificha kwa Okwi haiwezekani afanye vituko kesho mnapokea tena, yaani waliomsainisha Okwi ni mazwazwa
 
Okwi ni mzigo na tapeli wa mpira wa miguu hapa Tanzania kwa sasa.
Okwi hana mapenzi na timu anamapenzi na pesa.
Okwi hana msaada na timu, anacheza anapotaka na uongozi unamwangalia tu sijui kawalisha nini hadi anafanya anavyotaka na wanamwangalia tu.
MO mfukuze Okwi kama ulivyomfukuza Amog.
Sisi wengi wa wanachama na wapenzi wa Simba hatuna imani na Emanueli Okwi.
Aende uganda akaendelee na utalii wake.
Simba inahitaji mshambuliaji wa Kimataifa mwenye MUDA wa kuichezea Simba na kuiletea mafanikio.
Okwi ni Kirusi kinachoitafuna Simba sc.
Okwi ni tapeli hatumtaki kuendelea kuitapeli timu ya Simba na viongozi wake.
Tafadhalini viongozi wa Simba, mfukuzeni Emanueli Okwi hana manufaa kwa timu yetu pendwa.
 
Taarifa nilizonyapianyapia na za motomoto ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa Mganda Emmanuel Arnold Okwi ameomba radhi kwa kocha na viongozi wa simba pamoja na mashabiki huku akidhamiria kumaliza ukame wa magoli unaokumba klabu hiyo kwa sasa.

Okwi ambaye ameungana na kikosi hicho juzi akitokea nchini Uganda ambapo mara kadhaa kocha wa Simba Msoud Djuma amekuwa akimshutumu kwa kushindwa kusaidia klabu yake hasa katika michuano ya kombe la mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar.

Katika hatua nyingine kikosi cha Simba leo kinarejea jijini Dar Es salaam kutoka huko Morogoro tayari kwa pambano lake litakalofanyika hapo kesho tarehe 18/01/2018 kwenye uwanja wa Taifa.

Kosa hilo hilo au utovu huo huo wa nidhamu angeufanya mdogo wangu mwenyewe na ' Fundi ' Jonas Gerald Mkude a.k.a Xavi Hernandez nae angesamehewa kama Emanuel Okwi? Uzuri tu ni kwamba Okwi anajua ni wapi pa ' Kututekenya ' wana Simba SC wote na tunanyamaza. Nimesikitishwa mno na Kitendo cha Kumsamehe haraka hivi Okwi na kuna uwezekano akaharibu ' morale ' yote ya Timu hali ambayo huenda pia ikaharibu mwenendo mzima wa Klabu yetu. Nampenda na namkubali sana Okwi ila nadhani ameshatuchezea na kutushika ' Sharubu ' wana Simba SC vya kutosha. Na ndiyo maana kumbe kwa tabia yake hii hii ya ' Kipuuzi ' Mchezaji ' Mtukutu ' aliyeshindikana Tanzania nzima Haruna Moshi ' Boban ' kuna siku alimpa ' Vitasa / Ngumi ' za kutosha na Kumpiga Okwi ' Vichwa ' vya maana katika dressing room kwa tabia zake za Kitoto Kitoto na Kudekadeka huku akijifanya yupo juu ya Simba SC.
 
Tatizo simba walisajir wazee wengi ndo maana awasogei mbele wasitegemee ...wazee akina okwi kuisaidia Simba.
 
Okwi ni mzigo na tapeli wa mpira wa miguu hapa Tanzania kwa sasa.
Okwi hana mapenzi na timu anamapenzi na pesa.
Okwi hana msaada na timu, anacheza anapotaka na uongozi unamwangalia tu sijui kawalisha nini hadi anafanya anavyotaka na wanamwangalia tu.
MO mfukuze Okwi kama ulivyomfukuza Amog.
Sisi wengi wa wanachama na wapenzi wa Simba hatuna imani na Emanueli Okwi.
Aende uganda akaendelee na utalii wake.
Simba inahitaji mshambuliaji wa Kimataifa mwenye MUDA wa kuichezea Simba na kuiletea mafanikio.
Okwi ni Kirusi kinachoitafuna Simba sc.
Okwi ni tapeli hatumtaki kuendelea kuitapeli timu ya Simba na viongozi wake.
Tafadhalini viongozi wa Simba, mfukuzeni Emanueli Okwi hana manufaa kwa timu yetu pendwa.
Siku hizi mpira si mapenzi tena, ni kazi. Ni biashara. Ni pesa!

Mapenzi yamebakia kitandani tu, sio uwanjani.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Okwi ni mzigo na tapeli wa mpira wa miguu hapa Tanzania kwa sasa.
Okwi hana mapenzi na timu anamapenzi na pesa.
Okwi hana msaada na timu, anacheza anapotaka na uongozi unamwangalia tu sijui kawalisha nini hadi anafanya anavyotaka na wanamwangalia tu.
MO mfukuze Okwi kama ulivyomfukuza Amog.
Sisi wengi wa wanachama na wapenzi wa Simba hatuna imani na Emanueli Okwi.
Aende uganda akaendelee na utalii wake.
Simba inahitaji mshambuliaji wa Kimataifa mwenye MUDA wa kuichezea Simba na kuiletea mafanikio.
Okwi ni Kirusi kinachoitafuna Simba sc.
Okwi ni tapeli hatumtaki kuendelea kuitapeli timu ya Simba na viongozi wake.
Tafadhalini viongozi wa Simba, mfukuzeni Emanueli Okwi hana manufaa kwa timu yetu pendwa.
We jinga sana
 
Hivi boban ndio mpira basi tena, yaani imeshindikana kumsaidia kabisa.
 
Back
Top Bottom