Ballerina,
Huyu mama yupo sana tu ingawa umri ulishaanza kukimbia. Ni mwaka 2008 pale uwanjani Stade De France, Paris walishehekea miaka 30 ya KASSAV duniani.
Bahati mbaya mmoja wao, Patrick St. Eloi alishajitenga na mwaka 2010 akawa amepoteza mpambano na Kansa ambayo ilikuwa ikimsumbua.
Jocelyne Beroad alikuja juu sana na kulibadilisha kundi zima la Kassav na hasa wimbo wa SIWO. Ila baadaye walikuja akina mama wengine kumpa msaada kama backgorund Vocals. Kuna sehemu wamekuwa hata wanawatumia ZOUK MACHINE.
Waweza kuwaona hapa enzi wakiwa wote wazima. Kwenye video ya kwanza, Patrick ni yule anaimba mwanzo na kavaa kofia. Alikuwa na sauti ya kipekee sana huyu jamaa, RIP Patrick.
Tofauti nyingine ni kuwa Jocelyne anapata shida kidogo kwenye high pitch, angalia 3:26.
Mpiga Bass na Drums hapa huwaoni maana nao ni sehemu ya FACE ya Kassav.
Katika nyimbo ninazozipenda kwa sasa, ni huu wimbo ambao unapoanza, unaona wa ovyo sana ila unavyokwenda ndivyo unakuvuta na hutaacha kuusikilza tena na tena. Cha ajabu ni watu wanavyotulia na kuanza kusikiliza vitu vinavyotoka kwa heshima na hata wapigaji wenyewe, unaona wanaupiga kwa heshima sana. Sijui una maana fulani
Hivi huyu dada yu wapi???????Nina hakika wapenda zouk wanamkumbuka jamani