Bonde la Olduvai ni sehemu maarufu sana hapa Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla. Umaarufu wa bonde hili unatokana na historia yake iliyotukuka kwani ndipo mahali ambapo fuvu la binadamu wa kale kabisa kuwahi kuishi duniani liligundulika na Dr Louis pamoja na mkewe Mary Leakey. Bonde hili linapatikana eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambapo jamii ya wafugaji hususani wamasai wanapatika na wingi. Asili ya neno Olduvai inatokana na makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wajerumani waliokuwa wakitawala Tanganyika karne ya 19 ambapo walishindwa kutamka vyema jina la bonde hilo ambalo kwa lugha ya maasai linajulikana kama Oldupai yaani shimo kubwa. Kwa hiyo ni wakati wa kubadili mitaala ya elimu zetu na kutia uhalisi katika vitabu vya kujifunzia kuliko kuendelea kufundishwa makosa ati kwa sababu yalifanywa na wazungu.