Olduvai Gorge

Olduvai Gorge

kodo

Member
Joined
May 11, 2011
Posts
14
Reaction score
4
Bonde la Olduvai ni sehemu maarufu sana hapa Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla. Umaarufu wa bonde hili unatokana na historia yake iliyotukuka kwani ndipo mahali ambapo fuvu la binadamu wa kale kabisa kuwahi kuishi duniani liligundulika na Dr Louis pamoja na mkewe Mary Leakey. Bonde hili linapatikana eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambapo jamii ya wafugaji hususani wamasai wanapatika na wingi. Asili ya neno Olduvai inatokana na makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wajerumani waliokuwa wakitawala Tanganyika karne ya 19 ambapo walishindwa kutamka vyema jina la bonde hilo ambalo kwa lugha ya maasai linajulikana kama Oldupai yaani shimo kubwa. Kwa hiyo ni wakati wa kubadili mitaala ya elimu zetu na kutia uhalisi katika vitabu vya kujifunzia kuliko kuendelea kufundishwa makosa ati kwa sababu yalifanywa na wazungu.
 
olduvai gorge inapatikana jijini arusha afadhari makosa ya zamani kuliko hili lako.
 
Aisee kumbe ni oldupai.sasa hilo george ni la nani?
Nalog off
 
Ndio KODO.
Nimejiuliza kuhusu makosa ya wageni kutumika katika baadhi ya vivutio vyetu,kwa mfano.
OLDUPAI kuwa OLDUVA.
ELMANYARAI kuwa MANYARA.
Pia kwa ambao hawajatembelea eneo la OLDUVAI ni vyema wafanye hivyo kwani kuna mengi mazuri ya kujifunza kama safari ya yule mtaalamu wa kichina alofika olduvai kwa baiskeli.
Pamoja na hayo bado tunaviheshimu na kupeta rasilimali zetu,ni wakati wetu kuzilinda kadri inavyowezekana.
 
Ni kweli kaka kuna haja ya kuondoa uzungunization katika elimu yetu ili tupate uhalisi wa mali asili zetu. Lakini nadhani jitihada hazijafanyika vya kutosha kuhamasisha utalii kutoka nje na ndani pia, hata uliopo unawanufaisha wachache tu
 
linapatikana wapi ndugu yangu hebu nirekebishe basi?
Kodo hujambo ndugu yangu olduvai gorge inapatikana wilayani ngorongoro pamoja na kuwa jiji la arusha liko mkoani Arusha kama ngorongoro, lkn huwezi sema kuwa bonde hilo liko jijini Arusha.nakutakia siku njema.
 
Mkuu kwanini si jijini Arusha??
 
Kodo hujambo ndugu yangu olduvai gorge inapatikana wilayani ngorongoro pamoja na kuwa jiji la arusha liko mkoani Arusha kama ngorongoro, lkn huwezi sema kuwa bonde hilo liko jijini Arusha.nakutakia siku njema.

uko sahihi ndugu yangu japo jiji ni alama ya mkoa wa Arusha so sioni tatizo nikisema jijini Arusha
 
Back
Top Bottom