Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha: Kushoto ni Chongolo, kulia ni Thadei Ole Mushi
Katiba mpya si mali ya chama chochote ni mali ya wananchi. Na katiba mpya si utashi wa chama kipi kitupatie ni takwa la wananchi kama wakiitaka lazima ipatikane."
"Ni makosa vyama vya siasa kuhodhi mchakato huo na kusema bila sisi katiba mpya haiwezi kupatikana. Hakuna chama chenye mamlaka ya kuamua katiba mpya iweje. Mamlaka hiyo ni ya wananchi."
"Tatizo viongozi wetu wa CCM wanaona bado watu wamelala kule kwenye miaka ya giza. Lazima watofautishe wananchi alioongoza Nyerere na wananchi wa sasa" Thadei Ole Mushi, Kada wa CCM.