Ole Sabaya hata kama alikuwa na hatia lakini sio ya unyag'anyi wa kutumia silaha. Hakimu aliyehukumu hana weledi

Ole Sabaya hata kama alikuwa na hatia lakini sio ya unyag'anyi wa kutumia silaha. Hakimu aliyehukumu hana weledi

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na silaha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia silaha.

Ili unyang'anyi wa kutumia silaha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa silaha, kutumia silaha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linathibitishwa.

Lakini hata mashahidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya Serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.

My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
 
Hakimu hajafanya kazi kwa kukariri. amefanya kazi kwa kuzingatia gap zilizokuwepo kwenye ushahidi wa Sabaya na tafsiri yake kisheria.

Kitendo cha Sabaya kukiri kumiliki silaha, hata kama ni kwa ulinzi wake binafsi, na kuwa nayo siku ya tukio alipoingia ofisini kwa watu bila kibali kinachotambulika kisheria, hapa ndipo alipoharibu. Mahakama ilitafsiri hili amefanya uvamizi wa kutumia silaha.

Kwasababu unapoingia ofisini kwa mtu na silaha, hata kama huja point kwa muhusika, lakini psychologically unakuwa na advantage mbele ya muhusika, anaingiwa hofu kwa kuiona ile silaha uliyonayo, so unaweza muamrisha chochote na akatii kwa hofu ya silaha uliyonayo usije kumdhuru.

Silaha kuwa ndio "ingredient" muhimu kwenye kesi yake, alitakiwa kwenye utetezi wake either;

1. Akatae kabisa kumiliki silaha yoyote ya moto.

au

2. Akubali kumiliki silaha LAKINI hakuwa nayo siku ya tukio.

Huo utetezi wa pili ungesaidia kumsogeza mbele kwa kuisumbua mahakama itafute mashahidi wa ku-prove kwamba siku ya tukio kweli alikuwa na silaha.

Ili mahakama iamue jambo, lazima kuwe na ushahidi usioacha shaka, na huu ushahidi mostly ungetakiwa uje toka kwa third parties, hapa wangeweza kuwahonga mashahidi kama walikuwepo na kesi ingeishia hapo, au angepewa hukumu ndogo kama ingethibitika aliingia kwa watu bila kibali ila hakuwa na silaha.

Lakini kwa kukiri kwake kuwa na silaha eneo la tukio bila kibali alijimaliza mwenyewe, alimpunguzia hakimu kazi kwa kiasi kikubwa sana, mawakili wake hawakum "coach" vizuri kwenye hili.
 
Wewe mwenye weledi nenda basi kamuhukumu ili uridhike,ule wakati wa mahakama kupokea amri kutoka juu umeisha sasa hivi watu wanafanya kazi kwa taratibu walizosomea.

Alikuwa anakupa kula na subiri siku zinakuja utazidi kuuona ugumu wa mtaa.
 
Sasa hiyo silaha aliyo kuwa nayo eneo la tukio, ilikuwa ni kwa ajili ya nini? Kuwalingishia hao wafanyabiashara?

Halafu unakili mwenyewe 'hata kama Sabaya ana hatia! Sasa si ndiyo hiyo ya unyang'anyi wa kutumia silaha!!

Hata kama alitishia tu, bado sheria iko pale pale! Miaka 30 jela, na viboko juu.
 
Back
Top Bottom