Hakimu hajafanya kazi kwa kukariri. amefanya kazi kwa kuzingatia gap zilizokuwepo kwenye ushahidi wa Sabaya na tafsiri yake kisheria.
Kitendo cha Sabaya kukiri kumiliki silaha, hata kama ni kwa ulinzi wake binafsi, na kuwa nayo siku ya tukio alipoingia ofisini kwa watu bila kibali kinachotambulika kisheria, hapa ndipo alipoharibu. Mahakama ilitafsiri hili amefanya uvamizi wa kutumia silaha.
Kwasababu unapoingia ofisini kwa mtu na silaha, hata kama huja point kwa muhusika, lakini psychologically unakuwa na advantage mbele ya muhusika, anaingiwa hofu kwa kuiona ile silaha uliyonayo, so unaweza muamrisha chochote na akatii kwa hofu ya silaha uliyonayo usije kumdhuru.
Silaha kuwa ndio "ingredient" muhimu kwenye kesi yake, alitakiwa kwenye utetezi wake either;
1. Akatae kabisa kumiliki silaha yoyote ya moto.
au
2. Akubali kumiliki silaha LAKINI hakuwa nayo siku ya tukio.
Huo utetezi wa pili ungesaidia kumsogeza mbele kwa kuisumbua mahakama itafute mashahidi wa ku-prove kwamba siku ya tukio kweli alikuwa na silaha.
Ili mahakama iamue jambo, lazima kuwe na ushahidi usioacha shaka, na huu ushahidi mostly ungetakiwa uje toka kwa third parties, hapa wangeweza kuwahonga mashahidi kama walikuwepo na kesi ingeishia hapo, au angepewa hukumu ndogo kama ingethibitika aliingia kwa watu bila kibali ila hakuwa na silaha.
Lakini kwa kukiri kwake kuwa na silaha eneo la tukio bila kibali alijimaliza mwenyewe, alimpunguzia hakimu kazi kwa kiasi kikubwa sana, mawakili wake hawakum "coach" vizuri kwenye hili.