Uchaguzi 2020 Ole Sendeka anahaha na ubunge wa Simanjiro,awatumia Mzee Mangula,Malecela na mkewe kumsaidia kutokatwa jina lake

"Mwenye matokeo ya kidato Cha sita ,old Moshi sekondari, ya "Ole sendeka tuna atuwekee hapa tafadhali"
 
buswelu moja wala haiitaji 'Akili' kubwa kuweza tu kujua kuwa huenda Wewe ndiye 'Mpuinzani' wake mkubwa au umetumwa na 'Adui' Kummaliza.
Aisee kwa Issue ya Ole Sendeka ukijua ujinga aliofanya katika utawala wake hutokaa umshawishi yyt ampgie kura.

Naongea kama mtu ninayeishi Simanjiro zaidi ya miaka 12.

Sendeka ana Ukabila sana na anatumia uduni na uelewa wa Wamasai kufitini maendeleo ya Simanjiro kwa kuwaaminisha Wamasai kuwa endapo maendeleo yatafika Simanjiro wamasai watapoteza maeneo ya malisho kwa sababu wahamiaji watakuwa wengi Simanjiro na hivyo watapoka maeneo hayo.

Amefanya kufitini viwanda vya nyama na maziwa vya Rotiana, viwanda ambavyo vilikuwa vimeajiri zaidi ya wakazi 2500 wa maeneo mbalimbali ya Simanjiro na Arusha.

Viwanda vilikuwa vikinunua Ng'ombe karibu 1000 kwa mwezi kutoka kwa wafugaji Simanjiro na maeneo jirani.

Katika kipindi chake cha utawala hakutaka kabisa miradi mablimbali ikiwemo ule Maji kwa kuhofia wageni kuwa wengi eneo hilo na kwamba wenyeji wataporwa maeneo.

Alisababisha migogoro mingi ya ardhi hasa maeneo ya Langai, Losinyai na Kitiangare, migogoro inayodumu hadi sasa.

Kauli mbiu yake ilikuwa ni Ng'ombe kwanza, Binadamu baadae....WHAT THE HELL?

Hata lami ya Mirerani hakutaka iwepo kwa sababu kwa madai yake lami inaumiza kwato za ng'ombe wakipita barabarani.

Alikataa Mwekezaji mzalendo Martin asiweke Kituo cha Radio makao makuu ya wilaya Orkesumet na kumwambia akafunge Mitambo na station hiyo ya Radio Terrat, Kwamba Martine anataka kumvuruga Sendeka katika anga la siasa endapo atafunga radio Orkesumet.

Kwa kifupi Sendeka anahitaji Jimbo kwa maslahi ya tumbo lake na si kwa maendeleo ya Simanjiro.

Na wahakikishia Kamati kuu wakimpitisha Sendeka wapinzani wanachukua jimbo hilo saa 2 asbh.

CCM CHAMA CHANGU MSIPOTEZE HILI JIMBO, MZICHANGE KARATA VEMA.
 

Kumbe Wewe ndiyo buswelu moja na hii ni ID yako nyingine? Sawa Mkuu sasa nimekuelewa na kweli 'Jamaa' unamchukia na humpendi sana tu.
 
Kwa wote aliogombea nao Sendeka anawaacha mbali sana kiuwezo na kwa ubora.
Hakuna Cha upinzani Wala Nini huko Simanjiro
 
Kwa wote aliogombea nao Sendeka anawaacha mbali sana kiuwezo na kwa ubora.
Hakuna Cha upinzani Wala Nini huko Simanjiro
Yuko mama mmoja aligombea Yuko vizuri kuliko huyo fisadi na aliyefeli shule.
 
Mwanasiasa na Rushwa ni kama Mvuvi na shombo
Mtoa mada atakuwa James ole Millya ambaye alishindwa na Ole Sendeka kwenye kura za maoni hivyo bado ana matumaini ya kupitishwa.
 
Mtoa mada atakuwa James ole Millya ambaye alishindwa na Ole Sendeka kwenye kura za maoni hivyo bado ana matumaini ya kupitishwa.
Mnyeti alishamalizaga Kura za maoni za James Ole Millya,kuweni na amani.
 
Wewe nawe ni wale wale. Na wewe umeleta haya kwa nia ya kumsaidia nani?

Kwanza kwa ujumla, hakuna hata mgombea mmoja ndani ya CCM ambaye hajahonga. Walizidiana tu viwango.

Ukisema uondoe wagombea waliohonga kupitia CCM, labda mchakato uanze upya. Na hata mchakato ukianza upya, hakuna kitakchobadilika. Kuhonga ndani ya CCM ni utamaduni wa miaka mingi ambao hauna dalili ya kukoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si waje mtaani tupambane wote?
 
Pole Pole anakwambia "IMEISHA HIYO".
 
Mkuu naona unashusha data zote, kikao cha kamati ni lini tujue?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…