Ole wako Kikwete ukileta usanii report ya BOT

Ole wako Kikwete ukileta usanii report ya BOT

Naona kazi ya U-komando huiwezi unaanza kubatiza watu majina hata huwafahamu. Pole sana utapata pressure ya bure hapa.

hahahahahaah kaka is a kind JOKES au ume-mind?sorry sana basi.
 
Hongera Mwafrika wa kike!..

Tunahitaji sauti za kimapinduzi kama hizi.Kwa muda mrefu viongozi wetu wanadhani sisi ni majuha na waoga.Lazima waelewe kuwa mtu mmoja tu anaweza kutimiza azma ya watu milion mia!
Tafadhali viongozi wetu msidhani kuwa wananchi hawaoni matendo yenu.Kila kukicha mnakula maraha tu wakati wananchi pale muhimbili wanakufa kwa kukosa dawa ambazo zinapatikana? Kwa nini wazawa na wananchi wa kawaida wafe?? Kwanini wananchi wasubiri maisha mazuri mwaka 2010?? fedha za nchi na rasilimali zetu mnaziachia tu zinapotea na kuingia mikononi mwa marafiki zenu halafu tukitaka maelezo mnaunda vikamati uchwara halafu riport mnazibadili!
Nchi umeichukua ikiwa safi kabisa.Wananchi wake wanaupendo tena wapole lakini bado mnawauwa kwa kuwanyima mahitaji muhimu huku kundi lako la akina Rostam Aziz na waIran likiwa linajitajirisha na kudharau wananchi? sasa muda unaelekea ukingoni.Tumechoshwa kuuliwa wadogo zetu wachanga na mama zetu wajawazito pale muhimbili.Nchi yetu ni tajiri sana na hatupaswi kuishi maisha ya namna hii huwezi kuleta maendeleo nchini ikiwa utaacha rushwa kushamiri na kuuza kwa wageni.Ipo siku utakumbuka maneno haya na pengine itakuwa too late!

-Wembe
 
Si sahihi kumtishia Rais. Tunaweza kumkosoa, kumpinga, kumshutumu, kumlalamikia, n.k., lakini kumtishia ni kinyume cha tunayoweza kuyafanya kwa faida ya Tanzania.

Kuna kutishia hapa. Hasa ukiangalia tafsiri aliyokuwa nayo Asha alipoandika: “The power of women is beyond giving birth. We have the courage to give life and take it away” Naamini hii siyo maana aliyokuwa nayo Mwafrika wa Kike.

Mwafika wa Kike amekuwa akitoa maoni mazuri sana hapa JF. Inaelekea wakati huu amekasirika mpaka akakosea.

Kwa maoni yangu, si sawa kumtishia mtu yoyote hapa JF. Hata hivyo, nadhani Mwafrika wa Kike alitaka kuonya tu, na si kutishia. Asha ndiye ametumia lugha inayoweza kuleta tafsiri mbaya.

Naomba tusameheane na tuendelee kujadili kwa namna itakayoleta faida kwa taifa. Kwa kiasi, JK ni mvumilivu wa criticism. Nimeona hayo, na naomba nimpe shukrani kwa hilo.
 
Mwafrika wa KIKE,and others

Naona humu ndani watu tayaari mnamajibu yenu,kama huna dhamira mbaya why uhisi kuna usanii utafanyika?why mtu atoe vitisho? Rais amechaguliwa na watanzania including nyie wote,si vizuri kumtisha,pia si vizuri kuwa na majibu kabla,its healthy to live postively kuliko kuwaza -ve always.

Mwisho kwa niaba ya chama cha mapinduzi na serekali na serekali yake tumewaahidi watanzania report mtaipata tumesha sema ktk vyombo vya habari kua mtapata report as per your expectation.

Kidumu chama cha mapinduzi
 
Komandoo kutania wakati watu wako kazini unanifanya nikuelewe kwamba uko kenye kundi lile la kuja kupoza makali hapa . Lakini wembe ni mkali sana na haangaliwi mtu usoni hapa .

Mtoto wa Mkulima bora jiite mtoto wa Fisadi. I questioned your name before ukafifia naona sasa umekuja kwenye lile nililokuwa nawazia . Look here you are allowed to be a CCM support hata member nk lakini acha majina yetu . Hakuna mtoto wa mkulima hata mmoja anaweza kuitetea CCM ala kusema udumu Ufisadi wa CCM.

Mwafria mke nasema kaza kamba .Nilisema majuzi kwamba is about 3 weeks now I have the real copy ya report. I am kimya nangoja watamke nami nimwage hapa si kutishia ila kuwaeleza kwamba wasome na wailete kama ilivyo na kama wataweka viraja hatishiwi mtu tutaimwaga hapa maana tunayo .

Tuendelee kuwasha moto wananchi .Hya ni mapambano kuanzia Fikra na kuendelea.
 
Asha na MWK: shukrani sana, kwa utaratibu huu ukombozi tutaupata sooner than later.

Ila tu naomba ile report kama mnayo muiweke hapa hata kabla wao hawajaitoa, yaani hapo tutakuwa tumemkoma nyani sana.
 
Asha na MWK: shukrani sana, kwa utaratibu huu ukombozi tutaupata sooner than later.

Ila tu naomba ile report kama mnayo muiweke hapa hata kabla wao hawajaitoa, yaani hapo tutakuwa tumemkoma nyani sana.

Mkuu

Nafikiri ikiweza kuwekwa hapa litakuwa fundisho kwa wale wanaotumia hela kibao kuunda tume na mwisho ripoti zikaozea kwenye droo zao.
 
Mwafrika wa KIKE,and others

Naona humu ndani watu tayaari mnamajibu yenu,kama huna dhamira mbaya why uhisi kuna usanii utafanyika?why mtu atoe vitisho? Rais amechaguliwa na watanzania including nyie wote,si vizuri kumtisha,pia si vizuri kuwa na majibu kabla,its healthy to live postively kuliko kuwaza -ve always.

Mwisho kwa niaba ya chama cha mapinduzi na serekali na serekali yake tumewaahidi watanzania report mtaipata tumesha sema ktk vyombo vya habari kua mtapata report as per your expectation.

Kidumu chama cha mapinduzi

Mkuu Heshima Mbele

Mimi sikujua kama na wewe huko kundini.

Kwa maana nyingine kama unahusika ktk kuwatea Mafisadi
 
Hivi, jamani katika kujikumbusha, hiyo ripoti tunayoisubiri ilichunguza mambo gani hasa BOT?

Kwa kumbukumbu zangu najua kuna kashfa kibao zimeelekezwa BOT, kama vile akaunti ya madeni ya nje (EPA), kuna hilo la kufanya malipo kwa kampuni hewa, kama meremeta na wadogo zake, kuna kuchota kwa ajili ya uchaguzi mwaka 2005, na nyingine nyingi tu, sasa wakuu hao E&Y walifanyia kazi maeneo gani? Yale yote yaliyotajwa na DK. Slaa au baadhi yake<? na kama sio yote, nini tutarajie kifanyike katika maeneo mengine ya ufisadi ambayo hayajachunguzwa?
 
Nakubali kweli Wadada wameamka. Hakuna kulala hadi wakubali kubadilika au kuondoka. Mwafrika wa Kike Endelea kutupa vitu. Unajua Watanzania kwa sasa ni sawa na majani ambayo yameshachomwa sana na jua yanashubiri tuu mtu apite na sigara aidondoshe pale ndipo palipuke.. Nachujua mimi Watanzania hawatalipuka na silaha watalipuka kwa kuwazomea na hatimae kuwanyima kura mwaka 2010
 
Kwakweli tabu kwelikweli,tunachoomba ripoti iwe haijaguswa.Waandaaji wa ripoti hawawezi kukosa draft zote za ripoti hivyo wao ndio wanajua kuwa nini kitatokea baada ya Hali ya mambo kuwa bayana.Ni CAG,Rosta,JK,Meghji au Karamanji.
Ni ngumu kidogo kuthibitisha kuwa kuna au hakuna mkono wa mtu.Hii ni kwasababu mbona mchakato wenyewe unaonekana ni wa mzunguko mno kuna nini hapa?
Kila la kheri Tanzania.Sipendelei tufike huko lakini ahki Itendeke.
Chukia DHULMA popote pale.
 
Mambo hayo na hiyo ripoti ya kwanza mbona sina nayo wana JF
 
Naomba niseme yafuatayo kuhusu hiyo ripoti inayosubiriwa:
  1. Jitayarisheni kisaikolojia kuwa dissapointed nayo. Remember that we are not waiting for a report of an independent investigation into loss of public monies at the BoT. Ni kazi inayofanywa kwa niaba ya CAG. Yatafunuliwa tu yale ambayo CAG atataka yafunuliwe. Msisahau watu wote kwenye nafasi kama ya CAG ni wana CCM (overtly or covertly)
  2. Hakuna mtu hapa JF mwenye hiyo ripoti hadi sasa. Angekuweko, basi ni lazima angeshaitoa. Angeacha kwa kisa gani? The very nature of JF would require a full publication of the report at the first opportunity.
  3. Nilivyosoma kwenye magazeti ni kwamba ripoti itahusu fedha zilizopotea kwenye akaunti ya malipo ya madeni. Serikali ya CCM haiwezi ikataka kuweko ripoti ya kubainisha ukweli wote kuhusu wizi wa fedha za uma hapo BoT. That would be suicidal.
 
Naomba niseme yafuatayo kuhusu hiyo ripoti inayosubiriwa:
  1. Jitayarisheni kisaikolojia kuwa dissapointed nayo. Remember that we are not waiting for a report of an independent investigation into loss of public monies at the BoT. Ni kazi inayofanywa kwa niaba ya CAG. Yatafunuliwa tu yale ambayo CAG atataka yafunuliwe. Msisahau watu wote kwenye nafasi kama ya CAG ni wana CCM (overtly or covertly)
  2. Hakuna mtu hapa JF mwenye hiyo ripoti hadi sasa. Angekuweko, basi ni lazima angeshaitoa. Angeacha kwa kisa gani? The very nature of JF would require a full publication of the report at the first opportunity.
  3. Nilivyosoma kwenye magazeti ni kwamba ripoti itahusu fedha zilizopotea kwenye akaunti ya malipo ya madeni. Serikali ya CCM haiwezi ikataka kuweko ripoti ya kubainisha ukweli wote kuhusu wizi wa fedha za uma hapo BoT. That would be suicidal.

Mkuu Augustine,

Inaonekana umesahau namna JF inavyofanya kazi au umeamua tu kuwa negative. Hivi unajua ilichukua siku ngapi kabla mkataba wa Buzwagi haujawekwa hapa? Hivi unajua ilichukua negotiations kiasi gani behind the scene ili mkataba uwekwe hapa?

Tatizo ni pale watu wakiona vitu vimewekwa hapa wanadhani vimepatikana tu na vikawekwa hapa - NO, lazima kila kitu kifanyike kuhakikisha kuwa kilichopatika sio kasa au fake.

Jiulize tu kuwa ilichukua muda gani Mwanakijiji kuweka picha za ajali ya mama mbatia? karibu masaa manne baada ya picha kupatikana. Jiulize pia ilichukua siku ngapi kuweka barua ya Balali kujiuzulu - karibu siku mbili!

Kila jambo lina taratibu zake na sio kuwa kila kitu JF ikipata kinawekwa hapa. Unajua robot (invisible) lazima ipewe program kibao na ulinzi kibao kabla ya kuandika program mpya hapa (yaani kuweka mikataba na nyeti za serikali kama hizi) - unakumbuka ile report ya kamati ya madini iliyowekwa hapa juzi? ilichukua karibu wiki kabla haijawekwa!

Mkuu Augustine, kama ukitaka kupotosha uma ni vyema ukafanya hivyo ila kwa sasa inaonekana huna habari namna JF inavyofanya kazi. So far kuwa happy kuwa una watu kibao wanaosaidiana kufanya mambo hapa na I am happy to be part of group ya kina Mkjj na wengine wengi wanaopenda kubakia sirini.
 
Mwafrika wa Kike,

Nakubali kwamba nimekuwa nasahau kwamba "ukiona vyaelea vimeundwa"! Nawashukuru wale wote mnaofanya kazi kubwa ya kutuletea habari muhimu hapa. Kukosekana uwazi serikalini kumechangia sana kudumaza maendeleo yetu.

Ukiangalia historia yangu hapa JF (kwa kusoma postings zangu) utatambua kwamba siwezi nikawa na malengo ya kupotosha umma. Msimamo wangu ni ule ule tangu zamani wakati tukiwa kwenye bcstimes. Ni wa kujenga nchi. Wako wengi hapa wanaoweza kushuhudia hilo.
 
Kama ipo waachieni serikali waitoe yao kwanza, tuone kama kuna "doctoring" halafu toeni "original".
 
nyie humu ndani bado mnatuletea upuuzi hivi rais aliyechaguliwa na wananchi mnataka tusimpe vitisho kwanini? naomba muwe werevu rais anakoromewa na raia bila kujali hali yake rais ni nani kwa raia wewe?

kikwete anawajibika kwa upumbavu wote unaofanyika bila kujali ujinga wake ni gharama kwa damu ya watu, nani hajui Bhutto amekufa na watu wengi sana?

nani hajui kilichowaua ni demokrasia nani hajui gharama ya demokrasia ni ghali sana hata damu ya watu ? mnataka nini tufikie huko kwa uzembe wa kughushi report? anayeogopa kumshinikiza rais awe kimya na atuache sisi tunaojua kila madhara ya kuchezea amani ikipotea kikwete marekani wewe unayeleta mzaha utakuwa wapi sio maiti mimi na wewe?

rais si zaidi ya wananchi uwezo wa kumtisha tunao au unafikiria jeshi linamtii bila kura zetu?

acheni ujinga na mzaha unamuogopa kikwete kwa lipi wakati sisi tunampigia simu na kumtumia email bila kujificha? mbona anakubaliana nasi.
 
Back
Top Bottom