Ole wako mwanadamu

Ninaanza kwa salamu kwani siku zote huwa ni jambo la hekima pale popote linapotamkwa(muhali gani), ingawa mimi ni mgeni katika JF ila nahisi umeongelea kitu ambacho moyo wangu umekuwa na shauku ya kuongezea chochote katika hili@Eiyer

Mda mwengine ufahamu mbaya juu ya mambo unaweza ukapelekea product mbaya ya mambo kwani kile ambacho kitakuwa kinaendelea kitakuwa asili yake ni kutokana na ule ufahamu uliobebwa.

Maana ya kuabudu ni kufanya kitu chochote kile chini ya sheria ya Mungu, nasiyo kuenda misikitini au makanisani tu, halafu ukitoka huko Mungu hayupo ni sawa na kuwa na mzazi halafu ukamwambia awe mzazi wako nyumbani tu halafu ukitoka nje hamjuani. Mungu baada ya kumumba binadamu hakumuacha tu aishi tu anavotaka yeye tu, kwasababu alijua kuwa matatizo ni jambo ambalo litakuwa haliepukiki kwake yeye. hivyo alimpa muongozo kupitia huo jinsi gani aishi, kwavile yeye ndiye aliye tuumba basi bila shaka anatujua zaidi kuliko sisi kwa sisi tunavojuana.

Matatizo yote ambayo hii leo dunia inakumbana nayo ni matokeo ya mifumo ya maisha ambayo binadamu waliojitungia wao wenyewe kutoka vichwani mwao nakupangiana sheria ambazo asili wamezitunga wao, huku wakisahau tabia za kimaumbile ambazo wao wanazo, za kuathiriwa na mazingira waliyonayo, kwa kawida binadamu anatabia ya ubinafsi, ambayo inapelekea kujivutia vitu kiupande wake, ndomana leo tunaona wamiliki wa mfumo wa ubepari ambao tunaenda nao leo hii duniani wa kiwa juu na kuwaonea walioko chini, pia wakiendelea kutuletea sheria mbalimbali ambazo kimsingi haziendani na maumbile ya binadamu ndo mana matatizo, amani na utulivu wa nafsi kwa binadamu ni jambo ambalo halipo.

"kwahakika binadamu amepewa elimu ndogo tu" AL Qur-an Karim
 

AshaDii!

Nimependezwa sana na hoja yako .."Rahisi, Mazuri na Salama" ... Ulivyoifafanua nimeilewa lakini naona kama hukuitendea haki dhana nzima ya Rahisi,Mazuri na Salama! Mimi ninaona vyote ulivyojaribu kuonyesha kuwa ni Tatizo la urahisi uliojengwa na technologia na uzuri unaopatikana kutokea kwenye urahisi huo sio tatizo la msingi!

ILA

Tatizo la msingi liko kwenye UTASHI wa mwanadamu mwenyewe.

Kwa kuwa utashi ndio ASILI YETU YA MSINGI kama binadamu inapowekwa kando au kutupiliwa mbali matokeo yake ni kuharibika kwa kila jambo. Teknolojia yenyewe sio tatizo ..lakini ni pale inapotumika pasipo na utashi wa mwandamu.

Kama technolojia ingetumika kwenye utimilifu wa utashi wa mwandamu , uzuri na usalama vingechipua na pasipo na kasoro yeyote kwani Mwandamu hajaasi Utashi uliopia asili na utambulisho wake!

Bila utashi hakuna uzalendo!

Uzalendo ni muendelezo wa Utambulisho wa kweli wa mwadamu kwenye familia yake hadi kwneye jamii yake na hatimaye Taifa lake!

Swali? UTASHI unapatikana wapi? Na tunautunza na kuelea vipi ili usipotee kwenye familia na jamii yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…