DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema harakati za vijana na maandamano ya kudai haki si jambo jipya, bali ni mwendelezo wa historia ndefu ya mapambano ya kidemokrasia duniani.
Akizungumza katika kipindi cha Maswali na Majibu cha Jambo TV, Wakili Olengurumwa ameeleza kuwa katika historia ya dunia, nchi nyingi ziliwahi kupitia mapambano makali ya kuondoa mifumo ya kikoloni na tawala za wachache maarufu kama ambapo familia chache zilikuwa zikiongoza mataifa.
“Hii tunayoiona leo, ya vijana kufanya maandamano, kama Gen Z, tayari ilishafanyika huko nyuma. Lengo lilikuwa ni kuondoa mifumo ya watu wachache waliokuwa wakiendesha nchi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapinduzi barani Ulaya vililenga kujenga mifumo mipya ya kisiasa. Usione leo hizi nchi zimekaa katika mfumo wa kidemokrasia, zilipitia changamoto nyingi kabla ya kufikia hatua hiyo,” amesema Wakili Olengurumwa.
Amesisitiza kuwa maendeleo ya demokrasia yanahitaji historia ya mapambano na kwamba mifumo ya sasa ya kisiasa na kijamii imejengwa kutokana na mafunzo ya kihistoria yaliyopatikana kupitia changamoto hizo.