POTOSHI Olengurumwa: Katiba mpya inakwamishwa na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo

POTOSHI Olengurumwa: Katiba mpya inakwamishwa na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu Je, Olengurumwa aliyasema maneno haya au amemezeshwa? kwamba Katiba mpya inakwamishea na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo.

OLENGURUMWA.jpg
 
Tunachokijua
Onesmo Olengurumwa ni Wakili na mratibu wa mtandao wa kitaifa wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC).

Madai

Chanzo kimoja kupitia mitandao ya kijamii kilichapisha kipande cha video Oktoba 3, 2025 kinachomuonesha Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa akizungumza huku kikiwa kimeambatanishwa na ujumbe unaosomeka "KATIBA MPYA INAKWAMISHWA NA CCM MTANDAO WANAOUFAIKA NA MFUMO".

Je, uhalisia ni upi?

JamiiCheck imefuatilia kwa kina kubaini ujumbe ulioambatanishwa na video hiyo unapotosha uhalisia.

Ufuatiliaji kwa kupitia marejeo ya video ya mahojiano aliyofanyiwa Wakili Olengurumwa na kituo cha habari cha Jambo TV umebaini kuwa ujumbe ulioambatanishwa kwenye kipande hiko cha video yanapotosha uhalisia wa kile kilichozungumza na Wakili huyo kwa kuongeza maneno ambayo hakuyazungumza.

Kupitia mazungumzo yake Wakili Onesmo alipoulizwa kuwa andahani kwa nini mchakato wa katiba mpya unakuwa mgumu kufanyika alieleza kuwa;

"Hata Mwalimu Nyerere alisema, mtu yeyote yule ambaye anaendelea ku enjoy au mtu yeyote ambaye anaendelea kupata faida ya mifumo tuliyonayo hawezi kuona faida ya kubadilisha mifumo. Mwalimu Nyerere alisema kwamba watu wote ambao wanaogopa mabailiko ni wanyonyaji, hatuwezi kupata katiba mpya au tunarudi huko tulipo.

Kwa sababu, sababu nyingine inayoturudisha huko kwa sababu kuna watu hawapendi maboresho, kuna watu ambao hawapendi mifumo hii ya kidemokrasia kama vile vyama vingi, asasi za kiraia, vyombo vya habari kwa sababu ya tabia zao za kinyonyaji kama Mwalimu Nyerere alivyosema. Kwa hiyo sasa watu wachache wanaweza wakawa wanaweka vizingiti tusipate katiba mpya, tusifanye mabadiliko kwa sababu kwa kufanya hivyo tunakwenda kutishia mirija yao, tunakwenda kutishia maslahi yao".


Katika mazungumzo yake alieleza hivyo bila ya kukitaja chama cha mapinduzi ama CCM mtandao kama wakwamishaji wa mchakato wa katiba mpya na badala yake alizungumza lugha ya jumla.​

Attachments

  • photo_2025-10-03_22-40-29.jpg
    photo_2025-10-03_22-40-29.jpg
    125.7 KB · Views: 36
Back
Top Bottom