GE2025 Olengurumwa: Tamaa ya Fedha Kipindi cha Uchaguzi Inatufanya Tukose Viongozi Bora

GE2025 Olengurumwa: Tamaa ya Fedha Kipindi cha Uchaguzi Inatufanya Tukose Viongozi Bora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wakili Onesmo Olengurumwa, ambaye ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa tamaa ya kupokea fedha zinazotokana na rushwa wakati wa uchaguzi imekuwa chanzo kikuu cha Taifa kukosa viongozi bora.

Amewahimiza wananchi kuachana na tamaa ya fedha wakati wa uchaguzi kwa kuepuka vitendo vya rushwa, akisisitiza kuwa viongozi wanaopatikana kwa njia hiyo hawawezi kuwa na uchungu wa kweli wa kuwatumikia wananchi.

Olengurumwa ameyasema hayo leo, Agosti 4, 2025, wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikifanya uchaguzi wa ndani kwa ajili ya kura za maoni. Ametoa wito kwa wajumbe wenye nafasi ya kupiga kura kutumia fursa hiyo kuwachagua wawakilishi wenye uwezo na dhamira ya kuwajibika kwa wananchi.
 
Kupanga ni kuchagua upokee baisikeli mbovu halafu uteseke kwa miaka mitano ijayo au ukatae upate kiongozi mwadilifu.(ukishapokea baisikeli ndio imetoka hiyo kinachobaki ni mtoa rushwa kurudisha hela yake ya hongo kwa miaka mitano ijayo haji jimboni tena)
 
Back
Top Bottom