Olympiki - Target 2012 - Medali 20

Olympiki - Target 2012 - Medali 20

Mwanakijiji,

..unajua suala hili limekuwa likiniumiza kichwa kidogo.

..tunao wanariadha wengi tu waliopata mafunzo Marekani[Filbert Bayi,Nyambui, Shahanga,Zakaria Barie,Ikangaa] sijui wanatumiwa namna gani.

..kuhusu mbio fupi nadhani ziko very scientific zinahitaji vifaa kuliko mbio ndefu[100m to Marathon]

..inawezekana kipindi kile raw talent ndiyo iliyotuletea mafanikio yale. lakini inasemekana Filbert Bayi trained for 6 solid months kabla hajavunja rekodi ya 1500m.

NB:

..pia tulikuwa viongozi na mawaziri wanaopenda na kujituma ktk suala zima la michezo.

..Maj.Gen.Mirisho Sarakikya yeye mwenyewe alikuwa ni mwanamichezo. Chediel Mgonja alikuwa mhamasishaji mzuri sana. hata hii michezo ya halaiki tuliiga baada ya ziara ya Mgonja China.
 
Naamini hapa pia ni sehemu ya tatizo letu. Hawa kina Filbert Bayi na Juma Ikangaa ndio wamekuwa wakisimamia riadha yetu kwa muda mrefu sasa. Tatizo ni kuwa hawa ni kizazi cha zamani ambacho kilikimbia riadha kutokana na vipaji na ujuzi wa wakati huo.

Naamini tunahitaji damu mpya kuangalia riadha yetu na wazee hawa wakabakia kuwa washaurri tu na kama ningekuwa mimi wangebakia kuwa inspirational na siyo wasimamizi wa moja kwa moja.

..kuhusu mbio fupi nadhani ziko very scientific zinahitaji vifaa kuliko mbio ndefu[100m to Marathon]

Sidhani ni hivyo, si umeona Jamaica; mbio fupi ndio rahisi sana kwa sisi watu wa pwani, vilimani na tropics.. kwa Wamarekani ni ngumu sana bila madawa. Ndio maana mwaka huu utaona wajamaica wanavyopasua mbio hizi.

..inawezekana kipindi kile raw talent ndiyo iliyotuletea mafanikio yale. lakini inasemekana Filbert Bayi trained for 6 solid months kabla hajavunja rekodi ya 1500m.

Raw talent is a must; sasa ukichanganya raw talent plus training ya kutosha unachopata ni kupasua katika michezo. Ni lazima kipaji kiwepo kwanza na ujuzi unaendeleza tu kipaji hicho na kukinoa kifikie makali yake.

NB:

..pia tulikuwa viongozi na mawaziri wanaopenda na kujituma ktk suala zima la michezo.

..Maj.Gen.Mirisho Sarakikya yeye mwenyewe alikuwa ni mwanamichezo. Chediel Mgonja alikuwa mhamasishaji mzuri sana. hata hii michezo ya halaiki tuliiga baada ya ziara ya Mgonja China.

JokaKuu mimi singumzii michezo hii toka hewani, na mimi ni MwanaUmiseta na nimecheza kuanzia ngazi za chini hadi mashindano ya mkoa kabla ya kwenda Taifa, kule Mbule (tulipiga kambi pale Sekondari ya Karatu) tuliona vipaji vya ajabu vya mbio fupi na ndefu. Lakini vipaji vile havikuenda popote kwa sababu hatukuwa na scouts wa vipaji, na hatujaona kuwa ni biashara ambayo inaweza kutengeneza fedha kwa mtu na kulipa.
 
Mwanakijiji,

..labda nimefungwa na historia yetu mpaka kuona kwamba mafanikio yetu yako kwenye mbio za kati na ndefu.

..Mzee kama ulikuwa Umiseta basi nadhani hii ni field yako kuliko hata huo uandishi.

..kwa kweli ukiangalia pochi wanalopata washindi katika mashindano kama Boston Marathon, New York,..sijui kwanini vijana wetu hawajitumi, au watu hawasaki vipaji Tanzania.

..michezo inaweza kuwa tiketi ya kumtoa mtu kwenye umasikini.

NB:

..kwa kweli mawazo yako ni mazuri na yanapaswa kufanyiwa kazi.
 
..wakati huo huo Thunder Bolt ameweka rekodi mpya ya mita 200 ya kwa kukimbia kwa sekunde 19.30, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Micheal Johnson wa USA ya 19.32. tokea mwaka 1994
 
Naamini hapa pia ni sehemu ya tatizo letu. Hawa kina Filbert Bayi na Juma Ikangaa ndio wamekuwa wakisimamia riadha yetu kwa muda mrefu sasa. Tatizo ni kuwa hawa ni kizazi cha zamani ambacho kilikimbia riadha kutokana na vipaji na ujuzi wa wakati huo.

Naamini tunahitaji damu mpya kuangalia riadha yetu na wazee hawa wakabakia kuwa washaurri tu na kama ningekuwa mimi wangebakia kuwa inspirational na siyo wasimamizi wa moja kwa moja.

Sidhani ni hivyo, si umeona Jamaica; mbio fupi ndio rahisi sana kwa sisi watu wa pwani, vilimani na tropics.. kwa Wamarekani ni ngumu sana bila madawa. Ndio maana mwaka huu utaona wajamaica wanavyopasua mbio hizi.

Raw talent is a must; sasa ukichanganya raw talent plus training ya kutosha unachopata ni kupasua katika michezo. Ni lazima kipaji kiwepo kwanza na ujuzi unaendeleza tu kipaji hicho na kukinoa kifikie makali yake.

JokaKuu mimi singumzii michezo hii toka hewani, na mimi ni MwanaUmiseta na nimecheza kuanzia ngazi za chini hadi mashindano ya mkoa kabla ya kwenda Taifa, kule Mbule (tulipiga kambi pale Sekondari ya Karatu) tuliona vipaji vya ajabu vya mbio fupi na ndefu. Lakini vipaji vile havikuenda popote kwa sababu hatukuwa na scouts wa vipaji, na hatujaona kuwa ni biashara ambayo inaweza kutengeneza fedha kwa mtu na kulipa.

Mwanakijiji, kwetu sisi mbio fupi kwa kweli ni vigumu kuzimudu. Kwanza genetic body types zetu haziruhusu. Ukiangalia wanaotawala hizi mbio fupi wengi ni Wamarekani weusi na Wakaribiani. Kwa hiyo si sahihi kusema kuwa Wamarekani hawaziwezi. Carl Lewis, Linford Christie, Donovan Bailey, Maurice Green, Michael Johnson, n.k. Hata huyo Usain Bolt na yule demu alieshinda mbio za mita 100 wote wamevunja rekodi za Wamarekani weusi. Ben Johnson (yule Mjamaica aliyewakilisha Canadas) na yeye ilikuwa madawa. Halafu hata hawa Wajamaica wa sasa, wengi wao wana train Marekani na ni mabingwa wa track and field (All American).Sasa sisi wabongo wengi wetu ni watu wenye miili midogo midogo sana. Bongo ni nadra sana kukutana kwa mfano na mtu aliye 6'5. Ili uweze kutimka (sprinting) kwa kasi ile inabidi uwe unanyanyua vyuma kwa sana na inabidi uwe na mwili wa aina flani na hapa ndio mambo ya endomorph, mesomorph, na ectomorph yanapokuja. Angalia jinsi Gabri Haile Selasie jinsi mwili wake ulivyo....sio wa sprinting kabisa. Yeye ni masafa tu. Vilima, pwani, na tropiksi havisaidii katika sprinting...
 
NN.. itabidi uende Lushoto.. uone watu wafupi... sisi tuna mchanganyiko wa kila aina ya genes..
 
At least I can dream... and guess what.. it is the dream that make people dare to pursue it. The dangerous are the one who not dare to dream.. wanaenda enda tu.. kwa kufuata wimbi la wakati huo. I'm not one of them. If you can't dream it, you won't pursue it, and you won't achieve it.. so dare to dream!
 
Baada ya kutoa ufafanuzi zaidi, mimi sioni ubaya wowote na ndoto ya Mwanakijiji ingawa kwa wengine anaweza kuonekana kama hana subira maana 2012 siyo mbali na ukilinganisha tuko wapi kimichezo na lengo alilopendekeza. But heck, what's wrong with aiming high? One might as well shoot for the moon and if he doesn't get there, he'll fall among the stars. Weka lengo medali 20 (za aina yeyote ile) hata usiposhinda 20 na ukashinda 3 tu, bado ni bora kuliko 0!!!!
 
Nyani unajua hoja zenu na Pundit jana zilinisaidia kufikiri juu ya kitu kimoja ambacho sikukifikiria nacho ni reaction ya watu wa kawaida nyumbani. Nadhani reaction yao itakuwa typical na ile ya kwenu na hivyo kuweza kukushawishi wewe (I hope nimemshawishi Pundit pia) ina maana tukiweza kurefine argument hii tunaweza kuwashawishi watu wengi sana. Na hapo utakuwa ni mwanzo.

So, shukrani kwa sababu msingepinga vile nisingeweza kuona mapungufu ya hoja ya awali.
 
20 is an impossible target in such a short time, ukiangalia Italy ina 20 hadi sasa.
I think 3 medals is a more realistic target.
Au hata tusipochukua medali nadahani cha muhimu ni kuonyesha some sort of consistent planing and effort ya kufanya vizuri zaidi, hata kama ni simple try-outs za kutafuta naturally talented people, nakumbuka nilipokua shule kuna watu walikua wanakimbia vibaya sana, with some training wangefika mbali.
 
Kang, Italy inajaribu kushindana kwenye michezo ambayo watu weupe wana comperative advantage na hivyo wao wanashindana sana. Mambo ya kuogelea, gymnastics, n.k ni vigumu kwa nchi nyingine kufanya vizuri ukilianganisha na sports power houses kama US, UK, Australia na Uchina.

Sisi tutilie mkazo kwenye vitu ambavyo tunaviweza.
 
Jamani hata kulenga shabaha hatuna watu jeshini? Hakuna Ma-Sniper katika jeshi letu?
 
Nafikiri mnajua UK na Australia ni watani wa jadi na hawaelewani. UK furaha yao kubwa ni kwamba wamefanikiwa kuwapita Australia. Juzi walitoa kijembe kwamba wamewakalia na kuwajambia Australia.

Australia nao wametoa kijembe chao, kwamba, UK, hakuna kitu, wanashinda michezo ya kitoto ya kukaa (kuendesha baiskeli).

Labda na sisi tuendeleze utani wetu na watani wetu, Wakenya, ifike mahali tuamue kuwashinda hao kwanza mwaka 2012. Naona hata wao wanaporomoka.

Utani mwingine medals per GDP, Zimbabwe wanaongoza. kwahiyo sio wakati wote pesa zinasaidia sana.
 
Kwa nini tusipumzike mwaka 2012? Pengine ndipo wahusika watapata message!
Au tuungane na Kenya chap chap tuwe nchi moja!
 
Kampuni yajitokeza kuandaa wanamichezo wa Olimpiki London 2012
Na Mwandishi Wetu (Mwananchi)

KAMPUNI ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), imesema itasimama imara kuhakikisha Tanzania inapata medali katika Michezo ya Olimpiki itakayofanyika London, 2012.

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa TICTS, Predi Asenga, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa kampuni hiyo, katika hafla fupi ya kukabidhi bendera na kuwapongeza wanamichezo hao kwa kudumisha nidhamu katika michezo hiyo.

Asenga alisema wanamichezo wa Tanzania walikumbana na ugumu wa michezo kutokana na kukutana na wanamichzo walio na maandalizi ya nguvu, lakini ana imani kwa kadri TICTS watakavyoingia kwenye timu ya 2012, medali zitapatikana.

“Tunataka kufanya maandalizi ya muda mrefu, lazima Tanzania tuibuke na medali michezo ya London, lakini yote ni maandalizi, TICTS tunaliweza hilo na tutahakikisha Tanzania inaweka historia,” alisema.

Wanamichezo wa Tanzania walifanya vibaya katika michezo ya Olimpiki ya Beijing, ambapo kati ya wanamichezo wanane, hakuna hata mmoja aliyeibuka na medali.

''Tuna matumaini, ushirikiano wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), fedha zaidi zinaweza kupatikana kwa ajili ya kuwasaidia wanamichezo wetu, katika michezo ijayo kuelekea michezo ya Olimpiki ya London 2 012. Tutafanya kila tuwezalo kuunga mkono juhudi hizo kwa njia yoyote ile tutakayoweza.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Kanali mstaafu Idd Kipingu, ameipongeza TICTS, hasa kwa kufanimkisha ushiriki wa Tanzania katika michezo hiyo ya Beijing China.

Hafla hiyo iliyoambatana na chakula cha mchana kwa msafara wa wanamichezo wa Olimpiki ukijumuisha waogeleaji pamoja na wanariadha, iliandaliwa na serikali kwa kushirikiana na TICTS, kwenye hoteli ya Travertine, jijini Dar es Salaam.

Kipingu alisema, TICTS ni wapya katika medani ya michezo na kuwa kwa niaba ya serikali, akiwa kama Mwenyekiti wa BMT wanawapongeza na kuwakaribisha katika udhamini wa michezo nchini.

''Hatukupenda mlivyoitwa watalii, tena wengi wao ni Waandishi wa Habari, lakini nasikitika hawakujua nini maana ya Olimpiki, kuna mambo mengi huko ambako walimu, wachezaji wamejifunza…,'' alisema.

Naye Rais wa TOC, Ghulam Rashid, aliahidi kukaa pamoja na kujipanga kwa kuangalia upungufu uliojitokeza katika mashindano ya mwaka huu na kuanza mapema maandalizi ya michezo ijayo ya London 2012.
 
Mzee, nashauri ufanye sum-up baada ya mjadala wa wanajamvi na kumtumia Mhe. waziri wa michezo na baraza la michezo. wasipotekeleza tutawashitaki kwa uzembe. Eti hata hiyo michezo ya kulenga shabaha kwa kutumia upinde na mshale hatuwezi? mbona huo ndo utamaduni wetu! Pia wajeshi wetu bila shaka wanashabaha za kutosha kutumia bunduki. naamini kuwa tunaweza kufanya vizuri katika
1. Riadha
2. Kulenga shabaha kwa upinde na mishale
3. Kulenga shabaha kwa bunduki

Big up Mwanakijiji.

Ni ndoto za alinacha kudhani kuwa tunaweza kushinda medali yeyote acha hizo 20 huko London. Inatubidi kwa mara ya kwanza maishani mwetu tuwe wavumilivu na tupange mipango ya muda mrefu. Mavuno ya tutakachopanda sasa hayawezi kutokea hadi angalau 2016 kama siyo 2020.

Awali ya yote tuanze kwa kuwaheshimu wanamichezo wetu kwa dhati hasa kwa kuwaweka mbele katika matayarisho yetu yote na kuwaeleza ukweli wa hali halisi.

Tuwakaribishe wale walio wa vizazi vyetu walio nje. Togo imepata medali yake ya kwanza katika mchezo wa kayaking ambapo mshindani wake alitemwa na nchi yake ya kuzaliwa ya ufaransa!

Tuwekeze katika michezo na tuelewe kinachohitajika. Hatuwezi kuwa na waogeleaji wazuri bila kuwa na mabwawa ya kuogelea ya standard inayoeleweka na yaliyo accessible kwa watoto wetu wengi. Ni lazima tutambue kuwa kila kitu sasa hivi ni high tech., kuanzia chupi ya kuogelea, mipinde na bunduki. Tusitegemee kuwa ati kwa sababu tunavimudu hivi vitu kiasili kwa hiyo tutapata mafanikio katika mashindano. Mkuki wa Mmasai si sawa na javelin!

Mwisho ni lazima tujue kuwa watakaotushindia hizo medali sasa hivi ndiyo kwanza wako praimari au hata chekechea. Tuanzie huko!

Lakini, I am not holding my breath!

Nadhani njia ya uhakika zaidi ni kungoja tutakapoungana na Kenya!
 
Kambi ya Olimpiki 2012 yaanza

Kwa mara ya kwanza Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeandaa kambi ya vijana yenye lengo la kuwapatia elimu ya michezo na kujitegemea ikiwa ni maandalizi ya kujenga msingi bora wa wanamichezo katika kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi aliwataka wachezaji hao kutumia nafasi hiyo waliyopata kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu michezo na maadili ya Olimpiki.

Bayi alisema kuwa anaamini kuwa mara baada ya kumalizika kwa kambi hiyo kila mmoja atakuwa amepata ujuzi utakaomsaidia kujiamini na kujiendeleza katika shughuli mbalimbali za kila siku ambazo ni zaidi ya michezo.

Naye Rais wa TOC, Rashid Ghulam aliwaeleza kuwa katika michezo ya Olimpiki mbali na wanamichezo kushindana kuwania medali pia hupata nafasi ya kufahamu utamaduni wa nchi nyingine ambazo zaidi ya nchi 200 hupeleka washiriki katika michezo hiyo mikubwa duniani.

``Wengi wanafikiri katika olimpiki ni kushindana na kupata medali, kuna mambo mengi ukiondoa michezo 47 inayoshindaniwa, elimu ya kujitegemea mtakayopata hapa ni bora pia,`` alisema Gulam.

Mratibu wa kambi hiyo, Henry Tandau alisema kuwa jumla ya wanamichezo 23 kutoka katika shule mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam wanashiriki na lengo katika siku zijazo ni kuwa na kambi yenye sura ya kitaifa na baadaye ya bara la Afrika.

Alisema kuwa kambi hiyo inashirikisha wachezaji wa michezo mbalimbali ukiwemo soka, riadha, netiboli, judo, wavu, ngumi na kikapu.

Source: IPPMEDIA
 
Inafaa topik hii sasa ipelekwe kwenye sport... "Ushauri"
 
Back
Top Bottom