Oman yajiweka kimbelembele kutaka Houth waache kushambulia meli zipitazo bahari nyekundu

Oman yajiweka kimbelembele kutaka Houth waache kushambulia meli zipitazo bahari nyekundu

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Msemaji wa wanamgambo wa Houth amesema wapo Oman kwa mwaliko wa kuzungumza na upande mwengine wa kimataifa kwa ajili ya kuacha mashambulizi ya meli zinazopita mlango wa bahari wa Bab Mandeb.
Mohamed Abdel-Salam hakutaja huo upande wa pili katika mazungumzo hayo lakini akasisitiza kuwa msimamo wa kundi lake ni kuwa hakuna kusitisha mashambulizi hayo mpaka hapo Israel nayo itakapoacha uchokozi dhidi ya wapalestina na kuruhusu misaada ya mahitaji muhimu kuingia Gaza.
Akaendelea kusema kuwa msimamo wa kundi lao waliouweka wazi ni kuwa wanawaunga mkono wapalestina wa Gaza na hawawezi kufunga mikono kwa hilo.
 
Oman aache kimbele mbele
Hii ngoma waicheze israhell wenyewe na shost zake
Waarabu wamekua wapuuzi wapuuzi sana mbwa hawa
Waarabu bila wao kukubali israel isingeanzishwa 1948. Msikilize vizuri mwanahistoria:

Sawa, hao ni warabu wa huko, Je warabu wa huku africa wanafanya nini kuwasaidi Palestina?

Tuna Zanzibar, tuna Sudani, tunao Somalia, tuna Nigeria kwa mbali n.k, wanafanya nini?

Mbona lawama kwa wengine ili hali hata anayeongea ni mwarabu mweusi?? Yeye kasaidia nini?
 
Wao walitakiwa waongeze kasi sio kulala na kula tu wenzao wa Palestina wanakufa njaa.
Hapo kwa waarabu usitegemee kitu ndugu yangu. Mapema tu kwa.siku ya leo Marekani ilisema itatoa taarifa.

Na taarifa iliyotoka ni kwamba; Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, muungano wa kupambana na Yemen "Operation Prosperity Guardian" utakuwa sawa na Task Force 153.

Wajumbe wa Kikosi Kazi 153 ni
Marekani
Misri
Saudi Arabia
Umoja wa Falme za Kiarabu
Israeli
Ufaransa
Italia
Ujerumani
Uingereza
Uturuki
Jordan
Bahrain
Oman
Qatar

Houth imewajibu ipo tayari kupigana hiyo vita ya kihistoria.

Na Imethibitishwa sasa Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Saudi Arabia na Jordan zinaisaidia Israel kukwepa kwa meli zake kuzunguka bara la Afrika kwa sababu ya Yemen katika Bahari Nyekundu.

Israel inaingiza bidhaa kupitia bandari za UAE na Bahrain
 
Attachments

  • Screenshot_20231217_212448_X.jpg
    Screenshot_20231217_212448_X.jpg
    53.4 KB · Views: 4
WADAU TAFUTENI HELA ACHENI SIASA MTAKUFA KWA KIHORO CHA VITA VYA WAARABU NA WAYAHUDI,,,,.NA MTAONDOKA DUNIANI MTAWAACHA WANAGOMBANA
TOKA MWAKA 1967 MPAKA LEO KAULI ZA WAARABU DHIDI YA WAYAHUDI TUMEZIZOEA ILA VITENDO ZERO
 
Oman ameombwa na America na kwa kuwa Oman ni rafiki mzuri wa Yemen wana wafikishie ujumbe, lakini na uhakika Yemen hawezi kukosana na Oman na pia Oman hawezi kulazimisha Myemen wote wawili wanaheshimiana sana.

Inawezekana Oman anafikisha ujumbe kuwa watawafungulia chakula na mahitaji yaingie Gaza ili Yemen na yeye awache kushambulia hizo Meli.
 
Hapo kwa waarabu usitegemee kitu ndugu yangu. Mapema tu kwa.siku ya leo Marekani ilisema itatoa taarifa.

Na taarifa iliyotoka ni kwamba; Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, muungano wa kupambana na Yemen "Operation Prosperity Guardian" utakuwa sawa na Task Force 153.

Wajumbe wa Kikosi Kazi 153 ni
Marekani
Misri
Saudi Arabia
Umoja wa Falme za Kiarabu
Israeli
Ufaransa
Italia
Ujerumani
Uingereza
Uturuki
Jordan
Bahrain
Oman
Qatar

Na Imethibitishwa sasa Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Saudi Arabia na Jordan zinaisaidia Israel kukwepa kwa meli zake kuzunguka bara la Afrika kwa sababu ya Yemen katika Bahari Nyekundu.

Israel inaingiza bidhaa kupitia bandari za UAE na Bahrain
Dah [emoji45][emoji45][emoji45]
 
Dah [emoji45][emoji45][emoji45]
Yemen wamewajibu wapo tayari kupambana nao wote.

Imesema ipo tayari kupambana kwenye hiyo vita. Tena wenyewe wanasema vita adhimu ya kihistoria.

Na ukumbuke pia leo wameikamata meli ya Bulgaria na kulipuwa meli nyengine mbili.
 
Back
Top Bottom