PreGE2025 Omari Mtuwa: Viongozi CCM acheni kuwa madalali wa siasa

PreGE2025 Omari Mtuwa: Viongozi CCM acheni kuwa madalali wa siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Omari Mtuwa, amewaonya viongozi wa chama hicho kuacha tabia ya kuwa madalali wa siasa badala ya kukitumikia chama kwa uaminifu.

Akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya Kata na matawi katika Jimbo la Buchosa leo, Mtuwa alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa viongozi wa mashina kuhusu kubadilishiwa wazee wa mabalozi, jambo linalofanywa na baadhi ya makatibu wa matawi. Aliwaonya kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha, alisisitiza kuwa muda wa kampeni bado haujafika na ratiba ya uchaguzi haijatolewa, hivyo wabunge walioko madarakani na madiwani wanapaswa kuheshimiwa na kuachwa waendelee na kazi zao.

Akitolea mfano Jimbo la Buchosa, Mtuwa alifafanua kuwa mbunge wa sasa ni Eric Shigongo hadi uchaguzi utakapofanyika.

Mwanza CCM.png
 
Back
Top Bottom