Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Maishapopote,Mzee wangu nimemjua mzee mwariko tokea nikiwa mdogo mwaka 84-85 alikua maarufu sana na alishamchongea baba wa taifa kifimbo chake
Mzee mwariko yupona amejaribu mara kadhaa kupata nafasi ya kuwa mbunge wa moshi mjini kupitia ccm ila hakupata nafasi....
ukimtaja unanikumbusha utoto wangu...Mtaa wa Kenyata street, nikienda mtaa wa chini kuzurura na kuchungulia wakicheza ngoma kwa mzee mwariko...
MUNGU AMBARIKI...NA AKUBARIKI
Kuna kitabu kinaitwa, ''In Search of Exellence,'' kimeandikwa na waandishi wawili Peters and Waterman.
Hawa walifanya utafiti katika makampuni makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kama Apple, Microsoft, Cocacola, Xerox nk.
Katika mambo mengi waliyogundua kwa nini haya makampuni yamefanikiwa ni kuwa yote yanafanya mambo ambayo wanayamudu vyema.
Katika kitabu hiki haya ya mafanikio wameyaeleza katika sura wameipa jina, ''Stick to Knitting.''
Yaani kama wewe ni mshona sweta basi kaa na kazi hiyo uliyo na ujuzi nayo usitake kufungua duka la chips.
Mwariko yeye kipaji chake kikubwa kiko katika uchongaji sasa haya ya siasa ni mammbo mageni kwake na ndiyo maana hakufanikiwa.