Omari Mwariko nani anamfahamu?

Omari Mwariko nani anamfahamu?

Kolola,
Mzee mwenzangu.

Nadhani umesoma na kuona kuwa hizo ni kumbukumbu zangu nikiwa mtoto wa miaka 10 hadi 12 kiasi.

Naeleza yale ambayo nimepitia na hawa niliowataja ndiyo walikuwa wenzangu.

Sasa mzee mwenzangu unaniambia mbona sijaweka Mabudha na Wapagani.

Labda nikufahamishe.

Mimi katika umri wangu wote si hapa nyumbani wala si nje ya mipaka yake na nimezunguka sana dunia, sijakutana na mpagani ukimtoa Mzee Ngombale Mwiru.

Kwani wewe unakereka kusoma majina ya Kiislam?

Yanakuudhi huyapendi?
Hivi mzee mwezangu Kila mtu akileta stori za masahibu wake wa utotoni humu jamvini patatosha..
Nami nianze kuwaelezea kina John enzi twala kongoro la kitimoto huko peramiho!!
 
28 Apr 2015

Artist Julius Njau Officially Opened Latest News Exhibition Videos Nagoya Japan​


Julius Njau Celebrity Profile - Check out the latest Artist Julius Njau photo gallery, biography, pics, pictures, interviews, news,. on the published Exhibition in 2015 Nagoya Japan The latest Officially Opened The Exhibition Of Artist Julius Njau At Aichi Prefectural Museum Of Arts Located In Nagoya Japan in 2015 With Prefectural Governor Mr Hideaki Omura
Source : Julius Njau

Artist Julius Njau Painting Tribute- Great Exhibition of All Time


Julius Njau è nato nel 1961 a Marangu nel Moshi in Tanazania. Ha frequentato la scuola elementare Kilimanjaro e la scuola media tecnica Moshi preso la quale si è diplomato. La sua carriera di artista inizia nel 1972 quando, costretto a trascorrere due anni in ospedale per una brutta frattura alla gamba, iniziò a dipingere. In quel periodo la sua terapista, una radiologa finlandese, incoraggiò il suo talento mettendogli a disposizione materiali e comprandogli le sue stesse opere. Essa fu poi, nel 1983, l'organizzatrice della sua prima esposizione in Finlandia. Le prime opere erano rappresentazioni, basate sulle tematiche delle tradizioni della sua gente e la fauna selvatica. Il 1984 segna un cambiamento drastico nella sua tecnica e nello stile che approda nell'astratto. I suoi dipinti sono costituiti su giochi di colori e un miscuglio di forme oscure. L'ampio repertorio di opere di Julius Njau è stato acquisito dalla prefettura di Osaka ed il Museo d'Arte Moderna di Toyama in Giappone; Il Museo Etnografico di Francoforte e la Galleria ZAK di Furth in Germania; Galleria Amos Anderson Helsinki in Finlandia e il Quinto British Museum in Inghilterra. Nel 2002 Julius Njau ha ricevuto il Nagoya Mayor's Prize e nel 2003 si è aggiudicato il Gran Premio presso la prefettura di Toyama nell'ambito della competizione internazionale "Sukiyaki Meets the World" Festival del Design del Poster. Julius Njau è fra i membri fondatori e presidente della Marafiki ñAmicizia e Arte.
Ni dini gani huyo julius njau? Tunaandika historia za waislam wenzetu yakhe,hao wengine andikeni nyie
 
Macho...
Tuna serikali ina mawaziri 23.

Waislam 3 tu katika Baraza la Mawaziri lakini sijasikia hapa yeyote kusema kitu kuhusu hili.

Mimi naandika kumbukumbu zangu nataja majiina ya Kiislam watu wanakuja juu wananishutumu kwa udini.
Inashangaza sana.
Mohamed Said mimi ni mkristo. Nakubaliana na wewe. Licha ya ya baraza la mawaziri. Utawala huu umejaa kila namna ya inda. Sioni zile nyaraka za kitume kutoka kwa maaskofu. Zamani nilikuwa sielewi lakini sasa nakubaliana na wewe.
 
Hivi mzee mwezangu Kila mtu akileta stori za masahibu wake wa utotoni humu jamvini patatosha..
Nami nianze kuwaelezea kina John enzi twala kongoro la kitimoto huko peramiho!!
Inside...
Unataka kuniambia Mzee Mwenzangu (MM)kuwa hukuwa unajua kuwa hukatazwi kuandika hayo hapa?

Hivi kumbe hayo maneno yote ukidhani nakosea?
Kwa nini hukuuliza kabla?

Unadhani mimi kwa fikra zako zangu ni stori tu?

Unataka kuniambia huyaoni mengi ya kuelimisha katika post zangu?

Kuna ubaya gani kueleza historia ya Peramiho na ulaji wa nguruwe?

Hakuna tatizo lolote wala usihofu kitu.
 
Mohamed Said,

..umewahi kuisikia hii story kwamba kifimbo cha Mwalimu Nyerere kilichongwa na Omar Mwariko?

..sikiliza mahojiano ya Omar Mwariko hapo ktk video.


 
Mzee wangu nimemjua mzee mwariko tokea nikiwa mdogo mwaka 84-85 alikua maarufu sana na alishamchongea baba wa taifa kifimbo chake

Mzee mwariko yupona amejaribu mara kadhaa kupata nafasi ya kuwa mbunge wa moshi mjini kupitia ccm ila hakupata nafasi....

ukimtaja unanikumbusha utoto wangu...Mtaa wa Kenyata street, nikienda mtaa wa chini kuzurura na kuchungulia wakicheza ngoma kwa mzee mwariko...


MUNGU AMBARIKI...NA AKUBARIKI
hadi miaka ya 90 hivi nyumba yao ilikuwa na fensi ya majani na mti kama wa embe au parachichi mazingira kama kwa mganga vile...kuna kipindi vingoma vinapiwa usiku hadi kanisa la korongoni dar street tulikuwa tunasikia
 
OMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?

Huyo hapo chini aliyevaa kofia ni Omari Mwariko.

Nimemfahamu Omari Mwariko nakua na nasoma shule ya msingi Moshi katika miaka ya 1960.
Miaka hiyo Omari Mwariko alikuwa mtu maarufu sana.

Omari Mwariko ni msanii bingwa katika kuchonga na kazi zake zimeonyeshwa hapa nchini, Uingereza na Marekani.

Lakini kwa miaka mingi akawa kapotea katika ulimwengu wa usanii akawa haonekani wala hasikiki.

Siku moja miaka 13 iliyopita niko Moshi ghafla nikakutananae barabarani.
Nikamsalimia na nikajitambulisha kwa kumtajia jina la ndugu yake Athmani Upepo.

Hili jina "Upepo," si jina lake ila alipachikwa kwa ajili ya uwezo wake wa kukimbia mbio kwa kasi kubwa.
Nakumbuka utotoni Moshi kila mtu alikuwa na lakabu yake.

Kulikuwa na Ali Maresi.

Hili jina "Maresi," alipewa kwa uhodari wake mpirani kuwa akitanguliziwa pasi mpira akadodoshewa kwa mbele na kuupokea mabeki hawampati na atafunga goli.

Kulikuwa na Athumani Makufuta.

Kisa cha jina hili ni kuwa tukisomeshwa somo la Hand Craft Majengo Middle School na Mwalimu anaitwa Fritz (sina hakika na "spelling").

Huu ulikuwa mwaka wa 1963.

Mwalimu Fritz alichukia sana mwanafunzi kuchora kisha akafuta.
Adhabu yake ni viboko papo kwa papo.

Athumani akafuta na akala mboko sote darasani tunashuhudia.
Athumani Mfinanga toka siku ile akawa Athumani Makufuta.

In Shaa Allah iko siku nitaandika kuhusu haya majina na kuwatafuta wahusika ili tucheke.
Nitaanza na "Toligogo" Omari Matola golikipa hodari amefariki miaka michache iliyopita.

Sote tulikuwa wanafunzi wa Mwalimu Juma darsa yake baina ya Maghrib na Isha Msikiti wa Ijumaa.
Jina hili ukimwita lilikuwa na staili yake maalum.

Unalitamka kama vile unaimba.

Rafiki yangu Allah amrehemu kila nilipokutananae iwe Dar es Salaam au Moshi Mtaa wa Chini akiniadhimisha kwa mapenzi makubwa.

Turudi kwa Omari Mwariko.

Omari Mwariko alinipa muda wake na alipoona namdadisi sana kuhusu kazi zake pale pale akanikaribisha nyumbani kwake Njoro ili anioneshe baadhi ya vinyago alivyokuwa amechonga.

Nilifika nyumbani kwake na akanionyesha kazi zake na akachukua muda kunifungulia maktaba aliyohifadhi picha zake toka ujana wake alipoanza kuchonga.View attachment 1698508
Sheikh Mohamed Said: Mwariko ni Manyema?
 
Nasema kila siku anasimulia waislam tu!
Wakristo hapa ndipo mnapokosea, na sisi wapenzi wa kuyatafakari mambo kwa kina ndipo tunapoamini kwamba uimara na umadhibuti wannchi hii kutokuingia kwenye vuta ni kuvute ya kidini ni waislam.

Utitiri wa wakristo katika kila nyanja na sekta katika nchi hii kuanzia Serikalini hadi sekta binafsi, waislam wamenyamaza kimya.

Mohammed Said kama mwanahistoria Nguli kuleta historia hapa imekua ni Waislamu tu.?

Unaonaje nawe ukasoma historia na kuanza kuandika za wakristo tu kumrusha roho Mohammed Said?
 
Kwa masikitiko tunatangaza kifo Cha Mzee Omari Mwariko kilichotokea usiku wa Leo wa tarehe 21.
Taarifa za maziko nitawajulisha punde familia itakapotoa maamuzi sehemu husika
 
Back
Top Bottom