KWELI Omary Ramadhan Mapuri aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa tume ya Uchaguzi amewahi kuwa Katibu Mwenezi CCM

KWELI Omary Ramadhan Mapuri aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa tume ya Uchaguzi amewahi kuwa Katibu Mwenezi CCM

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na mijadala kwenye mitandao mbalimbali ikidai bwana Omari Mapuri aliyeteuliwa jana 29/06/2023 amewahi kushika cheo cha uenezi ndani ya CCM huku wengine wakidai kiongozi huyo hajawahi kuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama.

Je ukweli ni upi? Tunaombeni muweke jambo hili sawa

mapuri.jpg

Omari Ramadhani Mapuri
 
Tunachokijua
Omari Ramadhani Mapuri ni Mtanzania ambaye amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uchina kuanzia mwaka 2006 - 2012. Zaidi ya hayo, Omari Mapuri amewahi kushika wadhifa wa Uwaziri wa Mambo ya Ndani kipindi cha utawala wa Mzee Jakaya Kikwete, cheo ambacho alidumu nacho kwa muda mfupi kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi. Aidha, Makuri ameshawahi kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Uchaguzi wakati wa Utawala wa Hayati Magufuli.

Zaidi ya hayo, Mnamo tarehe 29/06/2023 Balozi Omari Ramadhani Mapuri ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa mara ya pili.

Kama alivyodokeza mleta mada, baada ya Rais Samia kumteua Balozi Omari Mapuri kuwa Mjumbe wa Uchaguzi kwa mara nyingine tena imeibuka mijadala katika mitandao mbalimbali katika mitandao ya kijamii ikimuhusisha Mteuliwa huyo kuwahi kushika wadhifa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Je upi ukweli wa mjadala huu?
Baadhi ya kuwapo mijadala huo JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali ili kubaini mbivu na mbichi za hoja kama ifuatayo:

Mjadala ndani ya JamiiForums
Mnamo mwaka 2013 Mwanachama wa JamiiForums aitwaye Concrete alidokeza kuwa Ramadhani Makuri amewahi kuwa Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kipindi ambacho alikuwa Waziri ya mambo ya ndani. Sehemu ya ujumbe wake inaeleza:

Madaraka ya Ukatibu mwenezi wa CCM na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa wakati mmoja yalimlevya sana Omary Ramadhano Mapuri, CCM walimtumia katika kuwadhibiti Wapinzani lakini mwisho wa siku wakamtupa ubalozini China

Hoja hiyo ya Mwanachama wa JamiiForums inatupa dokezo kwamba Omari Ramadhani Makuri ameshawahi kushika cheo cha Katibu Uenezi ndani ya Chama cha Mapiduzi.


Mijadala ndani ya Twitter
Mnamo Juni mwaka 2020 Watumiaji wa Twitter @Oraibtz na @JanethRithe walionekana kulalamikia kitendo cha Omary Mapuri kuteuliwa Mjumbe wa uchaguzi ikiwa alishawahi kuwa Katibu Mwenezi ndani ya chama cha Mapinduzi. @Oraibtz aliandika:

Huyu Omary Ramadhan Mapuri aliekuwa Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Sasa ni kati ya Mkuregenzi wa Tume ya Uchaguzi NEC.Aliteuliwa na Magufuli 2017.


Kauli ya Hayati Maalim Seif Hamadi
Nao ukurasa maalumu wa gazeti la Nipashe ndani ya Twitter Juni 10, 2020 lilimnukuu kiongozi wa ACT Wazalendo wa Wakati huo Maalim Seif Hamadi akipinga kitendo cha Omary Ramadhani Mapuri kuteuliwa kuwa Mjumbe wa NEC kwa sababu za kuwa Kada wa CCM. Baadhi ya nukuu za Mwalimu Seif zilisema:

""Katika ngazi ya Halmashauri, Wasimamizi wa Uchaguzi ni Wakurugenzi wa Halmashauri ambao kwa asilimia kubwa sana ni makada wa CCM. Unakuwaje na Tume Huru ambayo mmoja wa Makamishna wake ni Omar Ramadhani Mapuri, mtu aliyefikia kuwa Katibu Mwenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi? "-

Pia, mnamo Juni 29, 2023 baada ya Rais Samia kumteua tena Omary Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa NEC Mtumiaji wa Twitter @PMadeleka aliweka andiko katika ukurasa wake akidai kuwa Rais Samia amevunja Katiba ya nchi kwa kumteua Mapuri kwa kuwa ni mwanachama na hajawahi kana. Madeleka anaandika:

Uteuzi wa Omari Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, umevunja Katiba ibara ya 74(14) na (15)(c) ya Katiba ya Tanzania. Mapuri ni Mwanachama wa CCM na hajawahi kuukana Uanachama wake huo. Halafu mnataka tuamini kuwa tume ya taifa ya Uchaguzi ni Huru wakati Omari Ramadhani Mapuri ni mwanachama wa CCM ambaye amewahi hadi kuwa Katibu wa NEC, itikadi na uenezi? Ili tuwe na uchaguzi huru ni muhimu tukapata katiba mpya itakayokuwa na tume huru ya uchaguzi.
Maoni hayo ya Watumiaji wa Twitter na JamiiForums hayakinzani, yote yanakiri kuwa Omary Ramadhani Mapuri alishawahi kushika cheo cha Katibu Uenezi ndani ya Chama cha Mapinduzi wakati wa Utawala wa Kikwete kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ujumbe wa Kamati ya Uchaguzi (NEC).

Hivyo, kutokana na hoja hizo ambazo zimetolewa na Wadau ambao miongoni mwake ni vyanzo vya kuaminika. JamiiForums inaona kuwa hoja inayodai Omary Ramadhani Mapuri kuwahi kuwa Katibu Mwenezi ndani ya Chama cha Mapinduzi wakati wa Utawala wa Mzee Jakaya Kikwete ni kweli.
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na mijadala kwenye mitandao mbalimbali ikidai bwana Omari Mapuri aliyeteuliwa jana 29/06/2023 amewahi kushika cheo cha uenezi ndani ya CCM huku wengine wakidai kiongozi huyo hajawahi kuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama.

Je ukweli ni upi? Tunaombeni muweke jambo hili sawa

View attachment 2673829
Omari Ramadhani Mapuri
Sijui kipi hakijaeleweka hapo, Ukishasema kwamba alishawahi kuteuliwa kuwa Waziri kwa vyovyote vile alikuwa ana wajibika kwa aliyemteua . Na kimsingi alikuwa anawajibika kwenye Chama moja kwa moja ili kutekeleza Ilani ya Chama.

Je ni wapi tumeona Mhe, R.Mapuri amekanusha kuwa si mwanachama wa Chama chochote Tena? Tuache kujadili urefu wa Baabara wakati hatujafika mwisho wa Baabara husika .

Hakuna mjinga anaeset kisu kwenye makali yake harafu apitishe shingo yake kupima Kama kitamkata Never ever. Hata mi!!!!
 
TUNAUZABANDARI TUNAMLETA MWARABU SIJUI MFANYA BIASHARA KUJIBU.....tuna mchagua ostaz mapuri rama kuwa mwk tume mbele kwa mbele kwa mbele.. tunachuka tunawapa warabu waaah..
 
Back
Top Bottom