Ombea magauni na suti mnazovaa harusini; kuna zenye maagano ya kutengana, vifo, kutokuzaa n.k

Ombea magauni na suti mnazovaa harusini; kuna zenye maagano ya kutengana, vifo, kutokuzaa n.k

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Kwa wewe umeoa au kuolewa, hapa ujiombee na kuomba toba na rehema kwa ajili yako na nguo ulizovaa.

Hujaoa? Nikujulishe tu kwamba baadhi ya mavazi mnayovaa yana maagano ya vifo, kutengana, kutokuzaa. Kuna koo ambazo hazikai na mke au mume zaidi ya miezi 6. Vita vya ndoa vimejaa huko.

Leo nakushauri kama hujaoa au hujaolewa haijalishi umenunua wapi au umekodisha nguo za harusi wapi.

Ushauri mkuu kabisa, kama huko nyuma nilivyowashauri ombeni zawadi kabla ya kufungua. Siku hizi wanandoa wanapigiwa kule waliko.

Wakati huu wamekuja kwenye nguo mnazovaa.

Leo nashauri ombea yale magauni au suti unazoenda kuvaa, na kama una muda funga hata masaa kadhaa, kemea hizo roho kabla ya kuzivaa.

Sasa kumezuka ya kukodishana. Wale waliozivaa wengine hawajazaa mpaka leo ni sababu ya maagano.

Wengine wameshazivaa hizo nguo, hawako kwenye ndoa mpaka leo.

Wengine walivaa, baada ya miezi wakajifungua wakafa, wao watoto wakabaki.

Sikutishi, hii sio tu kwa hizi za kukodisha, hata za kununua dukani.

Kodisha, nunua, ziweke maombini, kemea roho zote nilizozitaja hapo juu.

Kila la heri.

Usiku mwema.
 
Magauni wanayovaa wakati wa harusi Yana maagano kuzimu,kabla hujafunga ndoa hakikisha unaliombea na kulitakasa gauni la harusi ndipo uvae ,ukivaa bila kuomba mengine yanabeba roho za mapepo za kutengana au roho za mauti, BWANA YESU KRISTO akupe macho ya rohoni
 
Leo umeandika vizuri kinoma since 2012 leo nimekupata clear
 
Kwaharaka haraka ile ya kuwahiana hakuna anaekumbuka,ni mpaka honeymoon iishe ndio akili zinakaa sawa...
 
Pdidy watu watausikiliza sana ushauri wako Kwa Sasa. Umeteka media japo Kuna vitu uliwafanyia watu wanasema sio vizuri kuwekwa hadharani.

Any way, na sie ambao tuli shake well before use kisha tukaja kufunga ndoa baada ya miaka zaidi ya kumi ya kuishi pamoja unatupa ushauri gani?

Zingatia (tulishona nguo mpya sio kukodisha) harusi kama ya kimagendo inaishia kanisani tu, saa mbili mnaangalia taarifa ya habari nyumbani.
 
KWA WEWE UMEOA AMA KUOLLEWA HAPA UJIOMBEE NA KUOMBA TOBA NA REHEMA KWA WEWE NA NGUO ULIZOVAA

HUJAOA
NIKUJUZE TU YALE MANGUO MNAVAA MENGINE YANA MAAGANO YA
VIFO
KUTENGANA
KUTOKUZAA
UKOO HUKO HUKAI NA MKE WALA MUME MIEZI 6
IN GEN YAMEJAA VITA YA NDOA

LEO NIKUSHAURI KAMA HUJAOA HUJAOLEWA AIJALISHI UMENUNUA WAPI UMEKODISHA NGUO ZA HARUSI WAPI

USHAURI MKUU KABISA KAMA HUKO NYUMA NILIVYOWASHAURI OMBEEN ZAWADI KABLA YA KUFUNGUA SIKUHIZI WANAAAPIGIA KULE WANANDOA

NA DID.TIME WAMEKUJA KWENYE NGUO MNAZOVAA

NA LEO NASHAURI OMBEA YALE MAGAUNI AMA SUTI UNAZOENDA KUVAA NA KAMA UNA MDA FUNGA HATA MASAA KADHA KEMEA HIZO ROHO KABLA YA KUZIVAA

NA SASA KUMEZUKA YA KUKODISHANA WALE WALIOVAA WENGINE HAWAJAZA MPAKA LEO N SABABU YA MAAGANO

WENGINE WAMESHAZIVAA HIZO NGUO HAWAKO KWENYE NDOA MPAKA LEO

WENGINE WAMEVAA BAADA YA MIEZI WAKAJIFUNGUA WAKAFA WAO WATOTO WAKABAKI

SIKUTISHI HII SIO TU KWA HIZI ZA KUKODISHA HATA ZA KUNUNUA DUKAN

KODISHA ..NUNUA..ZIWEKE MAOMBIN KEMEA ROHO ZOTE NILIZOZISEMA HAPO JUU

KILA LA KHERI

USIKUMWEMA
Pdidy Asante kwa ushauri, nakubaliana Sana na wewe, yaani kweli we mtu wa Mungu... Ila hako kajina Kako Mpendwa kanaweza kufanya tu siamini... Maana mwenye jina lake huko majuu mh... Mzee wa matopeni. 😁 😁 😁 🙏🙏
 
Pdidy watu watausikiliza sana ushauri wako Kwa Sasa. Umeteka media japo Kuna vitu uliwafanyia watu wanasema sio vizuri kuwekwa hadharani.

Any way, na sie ambao tuli shake well before use kisha tukaja kufunga ndoa baada ya miaka zaidi ya kumi ya kuishi pamoja unatuoa ushauri gani?

Zingatia (tulishona nguo mpya sio kukodisha) harusi kama ya kimagendo inaishia kanisani tu, saa mbili mnaangalia taarifa ya habari nyumbani.
Hahahaaaaaa nachekaaa mazurii mwamba

Jtanoo naendaa kanisa moja la kkt saa nne nkakuta jamaa wawili wanafunga ndoa na wake zao na wasimamizi yaan awakuzdi 15

Nkasema shikamoo ndoaa
 
Mk

Uuu niko ktk maongezi ya kuongeza

Pdidytz

Amaa nitoe p

Bado nashauriana na familia mkuu maana wajiina alivyotrend naweza pata rebate za ndege buree
 
Hahahaaaaaa nachekaaa mazurii mwamba

Jtanoo naendaa kanisa moja la kkt saa nne nkakuta jamaa wawili wanafunga ndoa na wake zao na wasimamizi yaan awakuzdi 15

Nkasema shikamoo ndoaa

Hao ndio wazee wa kazi. Mambo yasiwe mengi.
 
Pdidy watu watausikiliza sana ushauri wako Kwa Sasa. Umeteka media japo Kuna vitu uliwafanyia watu wanasema sio vizuri kuwekwa hadharani.

Any way, na sie ambao tuli shake well before use kisha tukaja kufunga ndoa baada ya miaka zaidi ya kumi ya kuishi pamoja unatuoa ushauri gani?

Zingatia (tulishona nguo mpya sio kukodisha) harusi kama ya kimagendo inaishia kanisani tu, saa mbili mnaangalia taarifa ya habari nyumbani.
Hongera sana,nimeipenda sana hii
 
Hongera sana,nimeipenda sana hii
Ahsante Mkuu. Siku hiyo tulisambaza upendo kanisani, watu wakala, wakanywa na watoto wa uswahilini walibeba wali kwenye mashati...

Caterer alikuja akapiga kambi pale tulivyomaliza hakuna Cha ukumbu Wala MC. Biashara iliishia pale pale.

Nikavuta mwali wangu tukaelekea zetu Ramada tulipewa offer ya siku tatu sea view Bei nzuri.
 
Kabisaa unajua hata wahuburi wanatakiwa kusisitiza hili wengi wanaishi maisha ya uzinzi kisa kusubiri wapatehelazaharusi
Hao ndio wazee wa kazi. Mambo yasiwe mengi.
 
Pdidy watu watausikiliza sana ushauri wako Kwa Sasa. Umeteka media japo Kuna vitu uliwafanyia watu wanasema sio vizuri kuwekwa hadharani.

Any way, na sie ambao tuli shake well before use kisha tukaja kufunga ndoa baada ya miaka zaidi ya kumi ya kuishi pamoja unatupa ushauri gani?

Zingatia (tulishona nguo mpya sio kukodisha) harusi kama ya kimagendo inaishia kanisani tu, saa mbili mnaangalia taarifa ya habari nyumbani.
10 yrs nkuu hapo n toba ya unzizi na rehema the. Mnaenda kimya kimya kansani ama msikitin mnatamaliza
Maana watoto wakisikia mmenda kuoana kwenye party kama za kina didy na wako la saba woiiiwoiiii

Hioo dhambii nyingine
 
Back
Top Bottom