Ombea Taifa dhidi ya Roho ya uadui na chuki za kidini iliyojidhirisha kupitia issue ya bandari

Ombea Taifa dhidi ya Roho ya uadui na chuki za kidini iliyojidhirisha kupitia issue ya bandari

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
331
Reaction score
416
Siyo kweli kwamba uwekezaji hauna faida au hasara Kwa mstakabali wa Taifa. Lakini hoja ya bandari imefunua mioyo ya wengi na kuonesha hatari iliyoko katika nchi yetu.

Tanzania hatutakuja kupigana vita ya wenyewe eti Kwa sababu ya kisiasa. Ccm Ina nguvu sana kuweza kutawala hata miaka hamsini ijayo!

Lakini tusipoangalia dini itakuwa ni chanzo kuvunjika Kwa amani katika nchi hii. Kila penye mjadala wa bandari angalia majina ya wanapinga na Yale wanaukubali.

Angalau wakristo hawana umoja katika hili lakini hao wengine wao ni kupinga tu! Wito wangu tuliombee Taifa umoja, amani na upendo utawale bila kujali misingi ya Imani na madhehebu.
 
Tatizo liko kwa mkuu wa nchi. Amekosa busara na hana karama za uongozi. BTW na wewe unajidanganya kuwa CCM kuwa na nguvu ndiyo tiketi ya kutawala miaka hamsini ijayo?

Hakuna kitu kinachozidi nguvu ya umma uliokosa matumaini. Chunga sana kaumu ya vijana ambao hawana ajira za kueleweka ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka huku viongozi wanakula anasa.
 
Kuna watu wa imani fulani wameonesha usaliti mkubwa sana kwa taifa hili kuutetea mkataba huu batili elimu muhimu sana
Kwenye mijadala wa bandari wewe soma comments za watu Kwa kuangalia majina ya watu kulingana na asili ya dini yake, utaona udini unavyoliangamiza Taifa.
 
Udini hakuna, chuki kubwa ni ya uzanzibari na utanganyika. Hata mm ninayo hii chuki
 
Back
Top Bottom