Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Jana katika pitapita zangu nikawa nimechill mahali. Mbele yangu kulikuwa na kijiwe cha bodaboda, kwa nilipokuwa nimekaa sidhani kama wale boda waliniona.
Ghafla akapita mwanafunzi wa sekondari na sare zake nadhifu, hakuwa na wenzake, alikuwa mwenyewe.
Mmojawapo wa waliokuwa pale kijiweni akamuita ,yule binti akasimama kusikiliza. Yule alomuita akaanza kushusha verse pale, kwa mazungumzo yao ni kama alikuwa amemtongoza binti lakini binti kakataa hivyo jamaa anazidi kubembeleza binti akubali.
Yule binti akawa anakataa lakini yule mwanaume kakazana tena na wenzie wawili wanasaidia kubembeleza.
Binti akazidi kukataa, mwisho akawasonya akasema " naenda kukushtaki kwa mama, si unamjua alivyo mkali, yatakayokukuta mi simo, na sipiti tena hapa kwenu", akaondoka zake.
Aisee, nilivyowatazama wale wanaume nilipandwa na hasira, nikafikiria kama na mimi dada zangu wangeharibiwa ndoto zao wakiwa na umri ule sijui wangekuwaje leo.
Pembeni yangu kulikuwa na tofali la block, nikatamani nichukue nimpige nalo kichwani yule aliyekuwa anamtongoza binti ila nikaona ujinga huu, niondoke hapa.
Ila nikajiuliza,kwanini kusiwe na sheria kali ya kuwaadhibu watu kama hawa wenye nia ovu za kuwaharibu mabinti wadogo tena bado wako shuleni ? Kama pale, binti anaenda nyumbani anapewa simu anaweka kwenye sound recorder,anarekodi mistari yote ya yule mwanaume ndo unakuwa ushahidi huo wa kumtia hatiani mtongozaji ( mbakaji ajaye).
Watu wazima wamejaa tele ushindwe wewe tu lakini sketi za shule ndo zinawachanganya.
Natamani Dkt. Gwajima D afanye jambo tuzuie ubakaji wa wanafunzi ukiwa kwenye hatua ya awali ya utongozaji kabla mwanafunzi hajabakwa. Kesi iwe" attempted rape"
Nawasilisha.