Ombi kwa Polisi: Nyinyi ni wenzetu, kwenye Maandamano yetu tafadhali msigeuke Gestapo au Makaburu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kazi Kuu ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao, katika kutimiza jukumu hilo, pia wanawajibu wa kutuliza ghasia na kuhakikisha kunakuwepo amani na utulivu kwa ustawi wa taifa hili.

Dar es Salaam



Mtwara


Iringa

Dodoma

Ruvuma

Singida

Musom



Hizi picha ni picha za mazoezi ya kawaida ya ukakamavu ambayo hhufanyika mara kwa mara and they have nothing to do with maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima siku ya tarehe 1 September. Siku hiyo kazi ya polisi itakuwa ni kuyaongoza maandamano hayo na kulinda mikutano ya hadhara ya Chadema nchi nzima.

Kwa vile tayari kuna viashiria vyote vya uwezekano wa kutokea vitendo vya fujo na uvunjifu wa amani ambapo ni jukumu la polisi wetu kutuliza fujo hizo, ila katika kutuliza fujo hizo, naomba wazitulize Kitanzania na sio Kikaburu! .
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Ukaburu sio rangi ni matendo tuu! . Hata ukiwa mweusi kama mkaa, ukiwa na tabia za Kikaburu, wewe ni kaburu tuu! .

Siamini Polisi wetu wanaweza kuwa Makaburu hiyo tarehe mosi September, maandamano na mikutano nchi nzima kuhamasisha UKUTA ikipata kibali, tujitokeze kwa wingi! .
Pasco
 
Hahahaha ikipata kibali.

NB. :Kwaniaba ya bodi ya wakurugenzi wa NHC tunapenda kumkumbusha Mh Mbowe a.k. a mzee wa Dubai kale kamzigo ketu.
 
Wasipopata kibali lakini wakaamua kuandamana itakuwaje?

Unatoa ushauri gani kwa polisi katika kukabiliana na maandamano yasiyokuwa na kibali?

Unatoa ushauri gani kwa waandamanaji wasiokuwa na kibali?

Ndani ya fikra zangu ninafahamu hakuna maandamano yatakayofanyika siku ya tarehe 1 Sept. Hizi ni kelele tu kama zilivyo kelele za kila siku ili kupitisha siku.

Uzuri/tatizo lililopo kwa sasa huu utawala uliopo unachukulia serious kila kelele wakati kuna kelele zingine kama za chura kwa tembo anayekunywa maji kwenye bwawa!
 
Pasco wastaarabu hufanya hivi



Raila Odinga akiongoza maandamano ya Wapinzani mjini Nairobi dhidi ya uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta!



Rais Uhuru Kenyatta akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kuhusu hatma ya taifa lao

Kama ni ukaburu tayari umepiga hodi Tanzania na Magufuli kafungua mlango!
 
Wasipopata kibali lakini wakaamua kuandamana itakuwaje?

Unatoa ushauri gani kwa polisi katika kukabiliana na maandamano yasiyokuwa na kibali?

Unatoa ushauri gani kwa waandamanaji wasiokuwa na kibali?
Lipumba anakumbuka sana dawa aliyopewa na pamoja na wezake 2015
 
Pasko

mbona kama umechanganyikiwa hivi? nini tatizo Kaka?

Tarehe moja hakuna maandamano hizi ni kelele tu.

afu uliona watu waliotangaza maandamano afu ndio wanaomba waitwe kuzungumza? Msuya kawaambia wazungumze nini?

Acha uwoga
 
Pasko

mbona kama umechanganyikiwa hivi? nini tatazo Kaka?

Tarehe moja hakuma maandamano hizi ni kelele tu.

afu uliona watu waliotangaza maandamano afu ndio wanaomba waitwe kuzungumza? Msuya kawaambia wazungumze nini?

Acha uwoga
Nilidhani Yule kada wa CCM Mtungi ndiye kaitisha mazungumzo! Sikumbuki kusikia kiongozi yeyote wa Chadema akiitisha au kuomba kuitwa kwenye mazungumzo. Wao wamesema kama wakiitwa watakwenda. Sasa kwa kuwa huyo Mtungi kaamua kucheza sanaa kama za ile kesi ya mita 200, nadhani hapo mazungumzo hakuna tena.
 
hujamskia lowassa? hujamskia Kingunge? hujamskia Kashinje?

ila serikali iko kimyaaaaaa si mmesema mnaandamana? andamaneni tuuuu kwani shida iko wapiiiiii?
 
hujamskia lowassa? hujamskia Kingunge? hujamskia Kashinje?

ila serikali iko kimyaaaaaa si mmesema mnaandamana? andamaneni tuuuu kwani shida iko wapiiiiii?
Kingunge? Tangu lini huyu akawa mwanachadema? last time I checked, alikuwa rafiki wa Lowassa, na hakuwahi kujiunga chadema

Na huyu Kashinje ni nani?
 
Kingunge? Tangu lini huyu akawa mwanachadema? last time I checked, alikuwa rafiki wa Lowassa, na hakuwahi kujiunga chadema

Na huyu Kashinje ni nani?
Mbona Lowassa hujamtaja?

sio Kashinje sorry ni Mashinji KM Chadema.

Kingunge ni mwanachama hai wa chadema alichukua kadi kigamboni siku lowassa alivyohutubia huko
 
Damu ya raia ambayo mataifa duniani inalinda kwa nguvu zote,polisi wetu wanaimwaga kikatili kwenye mchanga kulinda haramu.
 


Nimejisikia vibaya sana kwaajili ya hizo picha, kwanini tufikie hatua hio jamano.?!

Kwanini yasiwepo malidhiano angali bado mapema.?!

Kwanini ccm wasisikilize hoja za Chadema na upjnzani kwa ujumla.?!!

Dah, hizi picha nadhani wangeionyesha serikali na upinzani.
 

Hii Picha nimeipenda sana
 
Nitawahi Mwananyamala kutoa damu kwa wale mtakao patwa na ya kupatwa. Unakatazwa unaenda na wanaokukataza ni polisi.

Wakikushughulikia utasemaje. Wengi mnataka kuua image ya nchi kama mlivyofanya na Edo. Karibuni fu.
 
Wafuata mkumbo hawajui hilo kwamba kuandamana bila KIBALI ni kosa ambalo litasababisha haya mazoezi ya askari kutumika kiuhalisia.
Hasira hasara , maandamano yatasimamisha shughuli nyingi za kiuchumi mwishowe hakutakuwa na maendeleo yote zaidi ya malumbano ya wanasiasa wakifanya kazi zao za kisiasa ambazo zinasikika nchi nzima tena bila hayo maandamano wala mikutano wanayoipigania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…