Ombi kwa Rais Mwinyi: Wakumbuke Masheikh wa Uamsho ambao wanateseka huku familia zao zikiishi kwa shida

Walifanya makosa gani?? Kunawakati tusitumie dini kama chaka la kuficha maovu yetu. Kama hawakua na kosa Insha Allah wataachiwa
 
Kuna mambo unaanza changanya apa kua makini na weka akiba ya maneno
 
Mkuu, vijana wa leo ni wapumbavu kwel kwel hiki kizazi sijui itakuaje, hakitumii akili kabisa kuchakata mambo... inatisha

Nilikuwa sitaki kuchangia ila sababu nimekukuta na comment yako hii,

Kuwa makini na EXTREMIST YOYOTE, awe kwenye ulokole, usabato, uislamu etc au mlengo wa kabila ama race yake.

Nakuhakikishia hata huyu ambaye ameweka chuki yake dhahiri dhidi ya "makafiri" kwa mgongo wa Rais kwa kuwa yupo jf. Amini ukimkuta anacheka nao huwezi kuamini ila hivi ndivyo vilivyoujaza moyo wake

Hata wale waliouana Rwanda kwa ukabila, waliishi kama majirani wa ukaribu kwa unafki mkubwa for years ila genocide iliporipuka ndio sura zao halisi zikaonekana...

Brothet, EXTRIMISTS wanafanya maamuzi kwa hisia za chuki walizolishwa ila ukitumia akili kuwa_judge hiyo ni hasara yako maana wao hawatumii.
 
Tunarud pale pale AKILI hazitumiki.
 
Usiseme wakumbuke mashehe wa uamsho maana hawajashitakiwa Kama mashehe Bali wameshitakiwa kama raia wanaotuhumiwa kwa uhalifu fulani!

Sema wakumbuke watuhumiwa wa ..............
Kukaa mahabusu miaka yote hio tayari ni hukumu tosha.
 
Musiba angekuwa ni muislamu kitambo Sana angekuwa guantanamo ya bongo.Ponda kinachomponza ni dini yake.
 
pona pona yao Mashehe wetu hawa ni Tume huru ya uchaguzi tu before 2025. Hakuna njia nyingine. Tuungane sote tudai haki ya kuwepo tume hii.
Waislamu awajaamua wakiamua hakuna atakeendelea kuwepo guantanamo
 
Tuseme Mheshimiwa alikuwa na uchungu na wale wa nchi ya malkia wa sheba kuliko hao wazee wanaoishia ndani.

Hivi wana nguvu gani tena za kukwaruzana na serikali ? Awaachie tu waje wajingojelee siku zao za mwisho wakiwa huru.

Vile ana uchungu wa kunyonga watu, nakuomba Mheshimiwa uwe na uchungu huo huo na hao wazee wenzetu.
 
Sasa kwanini inatumika nguvu kuwatetea hao masheikh tu wakati wapo waislamu ambao wako huko jela kwa dhulma pia kama hao masheikh au kwa sababu wao si masheikh?

Si ndio apo sasa! Mapovu kila sehemu utadhani ndio waislam peke yao waliofungwa! Waendelee kusota tu manake walianza kuleta mihadhara ya hovyo ya uamsho blah blah na kukashifu dini zingine mi nasemaje kesi yao ianze kusikilizwa 2050! Inchi ina mambo mengi ya kuhangaikia sio eti ngombe kachinja John Abubakar asile nk mambo ya hovyo kabisa
 
Wahukumie basi, tujue Moja

Uchunguzi bado unaendelea kua mpole! Tangia hawa jamaa wadakwe Zanzibar imetulia sana saivi kuna warusi kibao wanaishi kule kwa kukwepa corona kwao na makanisa hayajachomwa moto na waislam wenye msimamo wa kati hawashambuli tena! Hao kesi yao isisikilizwe mpk wote wafie jela huko wakija mtaani saivi wataeneza sumu mbaya.
 
Eyce upo sahihi kwa asilimia zote, lakini kwa nini mtu anafikia kuwa kwenye msimamo mkali? Na kudhihirisha chuki zake hadharani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…