Padri mwingine huyo aliyenusurika kifo kuuawa na hao Mashehe.
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na shabulio la risasi dhidi ya Padri Ambros Mkenda (52) mwishoni mwa wiki iliyopita.
Afisa habari mkuu wa jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Muhina amesema watuhumiwa hao wamekamatwa usiku wa kuamkia leo kwa ushirikiano wa Makachero wa Zanzibar na wenzao kutoka PHQ DSM bila ya kuwataja majina kwa kuhofia kuingilia upelelezi wa kuwapata wengine.
Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa ili kuwapata washiriki wote katika njama za kumvamia na kumshabulia kwa risasi Paroko wa Parokia ya Mpendae mjini Zanzibar.
Amesema bado makachero hao wa polizi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, jana akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Naibu DCI Zanzibar ACP Yusuf Ilembo amesema polisi watahakikisha wale wote waliohusika katika shambulizi hilo wanatiwa nguvuni na kukabili mkono wa Sheria.