Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
KUbwa zaidi kidiplomasia ni pale alipowakilisha Tanzania Umoja wa Mataifa akiwa Rais wa Baraza la Usalama wa UM na kutoa msimamo wa Tanzania ambao uliiwezesha China kuweza kupata kura ya veto - kitu ambacho China haijasahau hadi leo hii! Lakini ikumbukwe kuwa nusura angekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kwanza kutoka Afrika kama isingekuwa veto ya Marekani katika mchakato uliowagonanisha China na Marekani; zipigwa kura mara 16 hadi Dr. Salim na mpinzani wake walipojiondoa kupisha watu wengine! Mchango wake UN ni wakukumbuka! Hata alipopewa Boutros Ghali aliyekuwa anafuatia ni Dr. Salim (Ufaransa ilitishia kumveto Salim).
Lakini ndani ya nchi yetu alifanya mengi sana ambayo labda tumesahau lakini katika kipindi cha 1980 - 1986 (baada ya vita ya Uganda na ukame) alitumikia kwa nafasi nyeti kama Waziri Mkuu (baada ya kifo cha Sokoine), Makamu wa Rais na nafasi nyingine nyeti kama Waziri wa Ulinzi! Kwa baadhi yetu tunaweza kusema hakuna mtu aliyewahi kuandaliwa kuwa Rais wa Tanzania kama JMT hadi yale makorogo yaliyomharibia 1995. Nilipata nafasi ya kufanya na mahojiano naye miaka kadhaa nyuma kitu ambacho hadi kesho kilinifanya niendelee kumheshimu kwani kwa tuliokuwa vijana wa enzi hizo Dr. Salim alikuwa ni kile ambacho kinawezekana kwa kijana kujituma, kusoma na kutumikia nchi.
Ombi langu basi ni kuwa Chuo cha Diplomasia kipewe jina la Dr. Salim A. Salim na kibadilishwe jina na hadhi yake.
Pendekezo:
Salim A. Salim College for Diplomatic Studies (CDS) kutoka Centre for Foreign Relations (CFR)
A College of the University of Dar-es-Salaam
Na kiongezwe ili kutoa kozi hadi za uzamivu (kama sehemu ya UDSM) kwenye mambo ya diplomasia.
NB: Aliyetengeneza website yao (CFR) afungwe!!
====
Pia soma: Rais Samia: Chuo cha Diplomasia sasa kitaitwa Chuo cha Dkt. Salim Ahmed Salim