Ombi kwa Serikali: Iruhusu huduma ya kujitoa uhai (euthanasia)

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Ombi langu kwa serikali ya JMT:

Mimi kama mwananchi wa taifa hili la Tanzania nina ombi kwa serikali yangu ya JMT kuruhusu huduma maalumu ya kujitoa uhai (Euthanasia) kwa magonjwa maalumu tu.

Hii huduma nilikuwa napendekeza iwe inapatikana kwa wagonjwa maalumu wenye magonjwa maalumu yasiyo na tumaini la uhai pasipo kujali aina gani ya matibabu mgonjwa anapatiwa.

Huduma hii ikiwepo nchini itasaidia kuokoa changamoto mbalimbali zinazo mkabili mgonjwa na walio mzunguka.

Nipende kutoa ombi langu.
 
Duh! Jitundike tu ndugu. Mi hata niugue vipi siwezi kuacha ugali na dagaa wa kukaanga.

Unaijua nyama choma wewe?

Thubutu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaaaaah mbona huduma hii ni ya kawaida tu kwa baadhi ya mataifa hapa dunia pili sipendekezi iwe lazima bali hiari ya mgonjwa mwenyewe mwenye uhitaji wa hii huduma kupewa
 
Tuongeeni hoja nyingine Wakuu, sasa hayo mambo ya kifo yanafata nini humu wakati watu wamepata mshahara Jana.

Kama vipi waiter leta mbili mbili kama tulivyo ila mtoa mada mruke 🥂
 
Upo sahihi, kuna wazee wanateseka sana hasa na saratani ila nadhani family za wenye kibunda huwa wanaongea na madaktari wawamalizie ndugu zao ambao hawana tumaini ila wanateseka tu,
Ila pia tukipata maendeleo hii sheria itawekwa ni vile bado tupo nyuma kimaendeleo.
 
Kwa namna moja ama nyingine nakubaliana na mleta mada. Kwanza hii itasaidia kupunguza gharama za matibabu, kumtibu mgonjwa ambaye hana uhakika wa kupona ni kupoteza pesa pengine zingesaidia kuboresha maisha ya wanafamilia.

Serikali inatakiwa kuliangalia hili maana jamii hususani wale wakipato cha chini wanapokuwa na mgonjwa asiye na matumaini ya kupona hutumia gharama nyingi hasa kwenye matibabu, chakula na pengine hata kwenye kuhudumia ni heri mgonjwa huyu akatolewa uhai ili kuipunguzia familia gharama za kumtibu maana kifo kipo na hakiwezi kuepukika
 
Haaaaaaah
 
Hii sheria ina muhimu sana kama ikifikiriwa mara mbili na serikali kupitia wizara husika
 
Kwa namna moja ama nyingine nakubaliana na mleta mada. Kwanza hii itasaidia kupunguza gharama za matibabu, kumtibu mgonjwa ambaye hana uhakika wa kupona ni kupoteza pesa pengine zingesaidia kuboresha maisha ya wanafamilia.

Serikali inatakiwa kuliangalia hili maana jamii hususani wale wakipato cha chini wanapokuwa na mgonjwa asiye na matumaini ya kupona hutumia gharama nyingi hasa kwenye matibabu, chakula na pengine hata kwenye kuhudumia ni heri mgonjwa huyu akatolewa uhai ili kuipunguzia familia gharama za kumtibu maana kifo kipo na hakiwezi kuepukika
Pamoja sana umeeleweka vyema kabisa
 
Back
Top Bottom