Phamarcist
JF-Expert Member
- Apr 18, 2021
- 219
- 479
Habari za wakati wanamichezo wenzangu?
Nikiwa kama mkereketwa wa soka mwenye makazi ya muda ndani ya mkoa wa kigoma. Ninaliomba shirikisho la mpira wa miguu ( FF) liangalie muda wa kuanza kwa mechi za ligi kuu kwenye mkoa huu.
Mkoa wetu kigeografia upo tofauti na mikoa mingine kwenye suala la kuchomoza na kuzama kwa Jua, nini maana yangu! Kigoma mpaka saa moja na nusu jua bado linawaka, hivyo basi kitendo cha kuanza mechi saa kumi kinapelekea mashabiki kua kwenye jua kali ndani ya dakika zote tisini.
Ili kuzuia tatizo hili at least mechi zingeanza saa 11 kwani majukwaa yetu hayana kivuli kabisa ukiacha jukwaa la VIP ambalo ni dogo sana kua accommodate watu zaidi ya 50.
Najua changamoto hii wamekutana nayo wengi lakini wamekosa mahala pa kuisemea, mimi binafsi nimeona jukwaa hili linatosha pia kufikisha hoja hii.
Asanteni.