Ombi kwa viongozi wetu wa CCM sehemu ya kwanza

Ombi kwa viongozi wetu wa CCM sehemu ya kwanza

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
OMBI KWA VIONGOZI WETU WA CCM SEHEMU YA KWANZA.

Na Frey Cosseny

Niwaombe viongozi wetu wa Chama Cha Mapinduzi mnapomuongelea Hayati Mwenyekiti wetu Taifa Dr. John Pombe Joseph Magufuli muchukue tahadhari kubwa sana.

Hayati Magufuli katika Marais waliyopita anayeweza kumfutia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume kwa Kuongezea CCM thamani basi ni yeye.

-UPANDE WA KAZI YA CHAMA NDANI YA CHAMA;-

RASIMALI WATU.

Ikumbukwe kuwa wakati Hayati Magufuli anachukua Uenyekiti CCM alikuta wanachama Milioni Nane toka enzi ya TANU na ASP hadi 2016.

Hayati Magufuli amefariki mwaka huu CCM ikiwa na idadi ya wanachama milioni 12 hii ni kutokana na taarifa ya Kikao cha mkutano Mkuu iliyopita 2021. Katika kipindi cha miaka mitano hayati Magufuli kaongezea CCM wanachama Wapya milioni 4 ambayo ni sawa nusu ya wanachama wa CCM toka TANU na ASP.

Nadhani kama ni kichaa basi ni kichaa mzuri sana CCM inahitaji ipate kichaa mwingine zaidi ya Hayati Magufuli. Pia wakati Hayati Magufuli anakuwa Mwenyekiti 2016 CCM ilikadiriwa kuwa na wafuasi yaani Wakereketwa na Washabiki Milioni 12 wakati Hayati Magufuli anafariki 2021 CCM inakadiriwa kuwa na washabiki na Wakereketwa milioni 25 ndani na nje ya nchi yetu. Basi kama alikuwa kichaa CCM inatakiwa Impate Mwenyekiti kichaa zaidi ya Hayati Magufuli.

-RASIMALI FEDHA

Wakati Magufuli anaingia kama Mwenyekiti 2016 CCM ilikuwa na Mali yenye thamani inayokadiriwa kufikia shilingi 100bilioni, wakati anaondoka 2021 CCM inakadiriwa kuwa na fedha taslimu shilingi 100B na Mali zenye thamani ya shilingi 1.2Tirilioni.
CCM ikiwa ni taasisi hapa nchini yenye Mali nyingi nyuma ya National Housing Cooperation.

-UWAKILISHI KATIKA VYOMBO VYA DOLA.

Wakati CCM inachukua dola chini ya hayati Magufuli Wapinzani walikuwa na Wabunge 100 ikiwa na Wabunge wa majimbo 66 na viti maalum 44 wakati hayati Magufuli anafariki ameacha wapinzani wakiwa na Wabunge 25 ikiwa ni Wabunge 8 wa majimbo kutoka Wabunge karibu 66 wa majimbo.
Kama Hayati Magufuli alikuwa kichaa basi CCM inahitaji Mwenyekiti kichaa zaidi ya Magufuli.

-KURA YA RAIS
Wakati Hayati Magufuli anaingia Ikulu CCM ilipata 58% ya kura ya Urais wakati hayti Magufuli anafariki ameacha mtaji wa kura ya Rais 84% kiwango ambacho haijawahi kupatikana CCM toka tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi kama huyu ni Mwenyekiti kichaa basi tunahitaji Mwenyekiti mwingine kichaa zaidi ya Magufuli.

Hapa sijaongelea Madiwani na Wenyeviti wa serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji ni katika awamu ya Magufuli Kwa mara ya Kwanza vijana wengi wadogo wamepata fursa katika nafasi ya wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji ndani ya CCM.

Tunafahamu kuwa Kauli ya Dr. Antony Dialo (Mnec) siyo yake pekee yake Bali kuna kundi kubwa la Viongozi wafanyabiashara ndani ya CCM waliyohathirika na Uongozi wa Hayati Magufuli ndani ya chama wako nyuma yake.

Kosa la Hayati Magufuli ni kutafsiri Imani, Philosophy na itikadi ya CCM kama ilivyoasisiwa na Wazee wetu jambo ambalo limehathiri wanachama wa CCM waliyojipa daraja la juu la Uanachama.

CCM inaamini kuwa binadamu wote ni sawa uwe mwanachama Kiongozi, Tajiri au Maskini hadhi yenu ni sawa ndani ya CCM. Hayati Magufuli hakufahamu kuwa ndani ya CCM wanachama tulishagawanywa mafungu na madaraja.

Daraja la juu zaidi ni wanachama viongozi wakuu wenye mamlaka makubwa ndani ya dola na chama. Wanachama wa ngazi juu kati ni wanachama watoto wa viongozi na wanachama viongozi wenye Utajiri mkubwa. (Mabwenyenye) Wanachama wa ngazi juu ni wanachama ambao siyo viongozi lakini matajiri (Makabaila).

Halafu sisi wanachama wa kawaida ambao hatuna madaraka ndani ya CCM wala dola ambao sisi ni watumwa wa kundi la kwanza la pili na la tatu.

Shida ya Hayati Magufuli ni kuwaunganisha makundi haya katika kapu moja katika kundi la wanachama jambo ambalo iliwahudhi wakubwa na kumtengenezea Maadui wengi sana ndani ya chama na nje ya chama.

Kosa la Hayati Magufuli ndani ya viongozi wenzanke matajiri ndani ya CCM ni kuwapenda watanzania Maskini na kuwatetea dhidi ya maonevu ya Matajiri Mafisadi ndani ya CCM.

Viongozi wetu wa CCM wakumbuke kuwa kabla ya Hayati Magufuli kuchukua Uongozi chama cha Mapinduzi iliyonekana kuwa ndiyo moyo wa Mafisadi kiasi kwamba kampeni ya 2015 iligeuka kampeni dhidi ya Mafisadi, kabla 2015 wanachama, Wakereketwa na washabiki wa CCM walisusia kuvaa sare za chama kwa kuogopa aibu ya kuzomewa na wananchi kwa kashfa ya Ufisadi.

Lakini waliyotumbukiza CCM kwenye kadhia hii ya Ufisadi walikuwa wanachama wachache sana ndani ya CCM ambao walikuwa viongozi Wafanyabiashara.

CCM ikageuka kama hekalu la wafanyabiashara na wanyang'anyi kama ile soko ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alienda kupindua meza.

Hayati Magufuli alilikuta nyumba ya Baba yetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume imegeuzwa pango la Wanyang'anyi na wakwepa Kodi. Losa la Hayati Magufuli ni kupindua meza ya wanyang'anyi na wakwepa Kodi ndani ya CCM na kumwaga bidhaa zao.

Ni Sauti ya Mwanachama kundi la Watumwa nikiwa Ikwiriri Rufiji
Frey Cosseny
Mungu ibariki CCM
 
Wanachama 12 m wa tume ya uchaguzi au wapi ?

Sikiliza wakati unaangaika na siasa ambayo huijui utachomwa moto bure siku yako ya mwisho,nakuonya Kama Mungu aishivyo ACHA Mambo aya, ACHA uongo, maana uongo ni dhambi pia eti mil 12 wanachama wa ccm , ACHA, ACHA , ACHA kabisa, tafuta pesa hachana propaganda uchwara nasema
 
Magufuli anafariki ameacha mtaji wa kura ya Rais 84% kiwango ambacho haijawahi kupatikana CCM toka tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi
Utakuwa na ugonjwa uitwao "Sukuma gangiasis" au "Push gang disorder".

Dawa ya ugonjwa huu ni kwenda Chato mara tatu kwa mwezi kuangalia kaburi la mwendazake na kisha kukubaliana na ukweli kwamba amekufa haswa na hatafufuka tena!

Alipata 84% kwa uchafuzi siyo uchaguzi. Ndiyo maana mzee Diallo amesema ktk kipindi cha jiwe taifa limepita ktk kiza kizito. Akamalizia kwa kusema jiwe alikuwa na faili lake Milembe.
 
Kununua wanachama
Kuchukua hela zawastaafu Nssf kupeleka kwenye miradi
Kubambikiza kesi wakosoaji nk.

Mazuri yote ya Magu yalijifuta na unyama wake.
Hata umwelezee vipi,hasafishiki
Pole kwa gazeti lako hapo juu.
 
Wanachama 12 m wa tume ya uchaguzi au wapi ?

Sikiliza wakati unaangaika na siasa ambayo huijui utachomwa moto bure siku yako ya mwisho,nakuonya Kama Mungu aishivyo ACHA Mambo aya, ACHA uongo, maana uongo ni dhambi pia eti mil 12 wanachama wa ccm , ACHA, ACHA , ACHA kabisa, tafuta pesa hachana propaganda uchwara nasema
Si wanachama hewa wapo upande wa NEC lakini siyo binadamu
 
Kununua wanachama
Kuchukua hela zawastaafu Nssf kupeleka kwenye miradi
Kubambikiza kesi wakosoaji nk.

Mazuri yote ya Magu yalijifuta na unyama wake.
Hata umwelezee vipi,hasafishiki
Pole kwa gazeti lako hapo juu.
Kufunga watu hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom