Ombi kwa WCB: Mchukueni Nuruel..

Ombi kwa WCB: Mchukueni Nuruel..

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Kipo kipaji kimoja kikongwe sana cha r n b kinaitwa Nuruel. Huyu jamaa ni mwanamuziki kweli. Ni zaidi ya Raymond. Alitoka na 'mng'aro wa silver. Akaja na kilio. Akaja kuimba na b band wimbo wa 'nzela'. Naona anawayawaya tu. Nasikia ni mtumiaji. Ila kiukweli kama WCB wakijaribu kuiona fursa ndani ya mtu huyu watakuwa wamefanya jambo adimu sana.

Niwaambie tu watu wote kuwa, sisi wa kizazi chetu cha 70s na 80s hatuna wawakilishi kwenye burudani. Tunabakia kusikiliza nyimbo za watoto hadi tunaona aibu. Nyimbo zenyewe za kitoto japo nzuri ila ujumbe si sahihi kwetu. Ukimsikiliza Chamellion wa uganda na Jaydee ndio utajua nasema nini. Nyimbo zao zinaakisi utu uzima wetu.

Sasa kwangu kwa upande wa rnb na afro pop hapa tz bado naona nuruel anafaa sana kutuwakilisha. Mfikishieni Diamond ujumbe huu. Pia tafuteni wimbo wa nzela muusikilize tena. Halafu tafuteni wimbo wa Kala Jeremia ft nuruel-usikate tamaa.
 
Sio kila mtu lazima aingie WCB, kama ni msanii mzuri kwann asijitahidi atoke mwenyewe?

Hii ndiyo inafanya diamond aonekane bila yeye watu hawawezi fanya vizuri.
 
Nadhani ametoa maoni Yake mazuri.. Wewe itakuwa sio mdau wa mziki mzuri
 
Sio inafanya aonekane ilishaonekana na iko ivo tayari
 
Watu wa umri wako bado mnasikiliza bongo flava?!
Na watoto wako watasikiliza nini?!

Nyie ndio mkizeeka mtakuwa kama Le Mutuz....umri umemtupa mkono ila bado anajiona kijana kwa kuvaa mikaptura na kukesha club na wajukuu zake.

We nenda kasikilize nyimbo za zamani...Tafuta nyimbo za Msondo,Sikinde,Dar International kaa ndani kwako usikilize hayo mambo ya Wcb waachie watoto wako.
 
Kipo kipaji kimoja kikongwe sana cha r n b kinaitwa Nuruel. Huyu jamaa ni mwanamuziki kweli. Ni zaidi ya Raymond. Alitoka na 'mng'aro wa silver. Akaja na kilio. Akaja kuimba na b band wimbo wa 'nzela'. Naona anawayawaya tu. Nasikia ni mtumiaji. Ila kiukweli kama WCB wakijaribu kuiona fursa ndani ya mtu huyu watakuwa wamefanya jambo adimu sana.

Niwaambie tu watu wote kuwa, sisi wa kizazi chetu cha 70s na 80s hatuna wawakilishi kwenye burudani. Tunabakia kusikiliza nyimbo za watoto hadi tunaona aibu. Nyimbo zenyewe za kitoto japo nzuri ila ujumbe si sahihi kwetu. Ukimsikiliza Chamellion wa uganda na Jaydee ndio utajua nasema nini. Nyimbo zao zinaakisi utu uzima wetu. Sasa kwangu kwa upande wa r n b hapa tz bado naona nuruel anafaa sana kutuwakilisha. Mfikishieni Diamond ujumbe huu. Pia tafuteni wimbo wa nzela muusikilizetena. Halafu tafuteni wimbo wa Kala Jeremia ft nuruel-usikate tamaa.
RnB siyo aina ya muziki unaofanya vizuri Afrika. Kitu AfroPop
 
kwa nini asiende kwa king kiba??? kila mtu mzuri akienda wcb mziki hutakosa ushindani
 
Sio kila mtu lazima aingie WCB, kama ni msanii mzuri kwann asijitahidi atoke mwenyewe?

Hii ndiyo inafanya diamond aonekane bila yeye watu hawawezi fanya vizuri.
Pigia mstari maneno yako ya mwisho
 
Sio kila mtu lazima aingie WCB, kama ni msanii mzuri kwann asijitahidi atoke mwenyewe?

Hii ndiyo inafanya diamond aonekane bila yeye watu hawawezi fanya vizuri.
Nurueli hana bahati ya kutoka (au tuseme hataki kutoka?). Kwa historia tu ni kwamba kaanza muziki kitambo sana na akina Sugu (Mr II), kunako miaka ya 1990. Lakini vijana wametoka na wanaendelea kutoka, ila yeye bado. Kuna kipindi alikuwa anaimba na B Band ya Banana, sijajua kaishia wapi!
 
Nadhani ametoa maoni Yake mazuri.. Wewe itakuwa sio mdau wa mziki mzuri
Mkuu na mimi nimetoa maoni yangu, hapana ni mdau wa mziki mzuri ila wasanii wetu tusiwajenge kuwa wategemezi, tusimpe mond mizigo zaidi!! nuruel kaanza kuimba zamani sana enzi hizo mond ana hata wazo la usanii, na kama umeangalia WCB wanapenda damu changa na sio kizazi cha nuruel
 
Naona Hana nafasi tena labda aende kwa amorapa Majani hua anawachukua wanamna hio so unajua Na yy anataka kurudisha hadhi ya bongo recod
 
Mambo yanaenda kwa kupokezana vijiti yeye kama hakujitambua na kuongeza juhudi kipindi kanyanyuliwa na B-band basi ndio imetoka hiyo.
 
Kiukweli namjua vizuri Nuruely ni bonge la mwanamuziki kinachomuangusha ni sapoti kwa mashabiki na vyombo vya habari. Ana kazi nyingi nzuri ambazo amezitoa lakini hazipewi kipaumbele sana.... Baada ya kuachana na B Band aliamua kupumzika kidogo kimuziki akaenda Mtwara kuishi na familia yake lakini kwa sasa amerudi tena Dar na yupo chini ya Mrisho Mpoto.
 
Sio kila mtu lazima aingie WCB, kama ni msanii mzuri kwann asijitahidi atoke mwenyewe?

Hii ndiyo inafanya diamond aonekane bila yeye watu hawawezi fanya vizuri.
Sio kwamba nuruel hajaribu kutoka. Inaonekana anakutana na changamoto nyingi. Wasafi wako vizuri. Si lazima pia wamsajili bali wampe sapoti ya kutosha maana wasafi ina menejimenti kubwa
 
Kiukweli namjua vizuri Nuruely ni bonge la mwanamuziki kinachomuangusha ni sapoti kwa mashabiki na vyombo vya habari. Ana kazi nyingi nzuri ambazo amezitoa lakini hazipewi kipaumbele sana.... Baada ya kuachana na B Band aliamua kupumzika kidogo kimuziki akaenda Mtwara kuishi na familia yake lakini kwa sasa amerudi tena Dar na yupo chini ya Mrisho Mpoto.
Huko kwa mpoto amekula chaka. Akae karibu na kina Taletale
 
Kiukweli namjua vizuri Nuruely ni bonge la mwanamuziki kinachomuangusha ni sapoti kwa mashabiki na vyombo vya habari. Ana kazi nyingi nzuri ambazo amezitoa lakini hazipewi kipaumbele sana.... Baada ya kuachana na B Band aliamua kupumzika kidogo kimuziki akaenda Mtwara kuishi na familia yake lakini kwa sasa amerudi tena Dar na yupo chini ya Mrisho Mpoto.
Yupo chanika nasikia ni mjasiriamali kwenye sekta ya kilimo na mifugo
 
Back
Top Bottom