Habari zenu ndugu zangu jamii forum..mimi ni mmoja ya wafanyabiashara na walipa kodi wazuri sana kutoka Halmashauri ya Mji wa Nzega. Lengo kubwa na kuleta hoja hii hapa jukwaani ni kuwasilisha dukuduku langu linapelekea kutofurahia kazi yangu ya ujasiliamali na kwa niaba ya wenzangu pia na ningependa hoja hii iwafikie wadau kwa ajili ya kupata suluhisho maana si Peke yangu nianaeumia nimebeba wenzangu wengine wengi wenye malalamiko.
HOJA YA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA
Sisi wafanyabiashara tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu kuongezeka na kukithiri kwa tozo mbalimbali tunatozwa katika shughuli zetu za biashara hasa tulio katika vibanda vya biashara . tunalalamikia:
TOZO ZA SERVICE LEVY
inayotozwa na halmashauri kwetu sisi wafanyabiashara ni mzigo mkubwa mno kwetu tena tunadaiwa na kutishwa kufungiwa vibanda vya biashara na wakusanya mapato, hali ambayo imekuwa mzigo mkubwa kwa wafanyabiashara wengi, hasa wadogo na wa kati.
Mfano kuna baadhi wanadaiwa elf 50 hadi 8 kila mwezi kwa miezi 3 wauza nyama samaki (bucha)vitenge na urembo wa nyumbani, Vyakula n.k
Hii ni sumu kwetu na ni mzigo mkubwa mno imepelekea wenzetu kiacha biashara sababu ya mzigo mkubwa wa hii Service Levy.
MBAYA ZAIDI KIRUSI HIKI HUKIKUTI KWA WILAYA NYINGINE ISIPOKUWA HAPA NZEGA TU kwanini?tunaomba ufafanuzi
Tueleweke kuwa hatukatai kulipa Kodi lakini si mfumo huu...mbona wafanya biashara wa wilaya zingine wanalipa TRA (kwa miezi 3 ya makadirio)na Leseni ya biashara mara moja kwa mwaka kwa nini kwetu iwe tofauti kuna nini kinaendelea hapo?je ni nani wanahusika kutwisha mzigo mkubwa huu wafanya biashara wanaojitafuta..imagine kwa mwaka mfanyabiashara inakutoka zaidi ya milion 2.5 kwa mwaka ..kwa mitaji yetu hii ya kusuasua .mzunguko wa biashar mdogo ..kuacha hatuwezi tunakomaa huku kukifa na tai shingoni ..INAUMA SANA. Mamlaka husika mlitizame hili kwa maikini
Kutokana na hali hiyo, tunaiomba serikali na mamlaka husika Hususani HALMASHAURI YA MJI NZEGA
Kufanya mapitio ya mfumo wa utozaji wa Service Levy ili kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara.
Kuweka uratibu mzuri wa kodi Hii ya service levy( ushuru wa Halmashauri) na tozo mbalimbali ili kuepuka migogoro na wafanya biashara na kuweka mfumo wa malipo yanayofanana na Wilaya zingine
Kusikiliza maoni ya wafanyabiashara kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya kodi na tozo hii inatuumiza mno kuturundikia utitiri wa Kodi HASA HII SERVICE LEVY na ushuru wa halmashauri .
Wafanya biashara wa Nzega Tunaamini kuwa kupunguza mzigo wa kodi na tozo kutachochea ukuaji wa biashara kulipa kodi kwa wakati na kufurahia tunachokifanya bila manung'uniko, na hatimaye kuongeza mapato ya serikali kwa ujumla.
Wafanyabiashara tuna wasiwasi kwamba mfumo wa utozaji wa tozo nyingi unaotekelezwa katika halmashauri hii unaonekana kuwa mzigo mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine. Tunakutana na malipo ya Service Levy ushuru, kodi za TRA, leseni za biashara na tozo nyingine mbalimbali kwa wakati unaokaribiana, jambo linalopunguza mtaji na kuathiri ukuaji wa biashara.
Tunaiomba halmashauri ,baraza la.madiwani na MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI NZEGA kutoa ufafanuzi kuhusu:
Sababu zinazofanya mfumo huu wa tozo kuonekana kuwa mkubwa zaidi katika halmashauri hii kuliko maeneo mengine YANI KWA NINI MZIGO HUU WA TOZO NYINGI HIZI WAPEWE WAFANYABIASHARA WA MJI WA NZEGA TU NA SI SHINYANGA ,SONGEA WALA SUMBAWANGA .
Hatua zinazoweza kuchukuliwa kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara bila kuathiri ukusanyaji wa mapato.
Pia tunaomba kufanyika kwa majadiliano kati ya halmashauri na wafanyabiashara ili kupata suluhisho litakalolinda maslahi ya pande zote, kwa kuwa wafanyabiashara ndio wadau muhimu katika ukuaji wa uchumi na ongezeko la mapato ya halmashauri.
NOTE:
IFAHAMIKE KUWA TUNAIPENDA NA TUNATHAMINI JITIHADA ZA SERKALI KATIKA KUKUSANYA KODI KWA AJILI YA MAENDELEO YA NCHI YETU NA HATUNA NIA OVU YA KUKWEPA KULIPA KODI LAKINI KWA HILI TUNAONA HATUTENDIWI HAKI.