HOJA Ombi la ufafanuzi kuhusu hali ya maombi ya ajira TAKUKURU

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
YAH: OMBI LA UFAFANUZI KUHUSU HALI YA MAOMBI YA AJIRA TAKUKURU​

Ndugu zangu,

Mimi ni mmoja wa waombaji wa nafasi za ajira zilizotangazwa na TAKUKURU mwaka huu. Baada ya kutuma maombi, baadhi yetu tulipata nafasi ya kushiriki katika hatua mbalimbali za mchakato wa usaili, ikiwemo mtihani wa maandishi, mtihani wa vitendo pamoja na usaili wa mahojiano.

Baadaye, mwezi Septemba 2026, baadhi ya waombaji walipokea majibu kupitia barua pepe pamoja na akaunti zao za Ajira Portal. Hata hivyo, kuna baadhi yetu ambao hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2026 hali ya maombi kwenye akaunti zetu ilikuwa bado ikionyesha neno “Pending.”

Kuanzia tarehe 1 Oktoba 2026, baadhi ya waombaji tulipoingia kwenye akaunti zetu, tulikuta ujumbe ukisema “Dirisha la maombi limefungwa”, bila kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kuhusu maana ya hali ya awali ya “Pending.”

Kwa heshima, tungependa kupata ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika:
  1. Je, hali ya “Pending” iliyokuwa ikionekana kwenye akaunti zetu hadi tarehe 30 Septemba 2026 ilimaanisha kuwa mwombaji hakuchaguliwa (Not Selected)?
  2. Au hali hiyo ilikuwa bado inaashiria kuwa mchakato wa uteuzi ulikuwa unaendelea na kwamba waombaji hao wanapaswa kusubiri majibu rasmi kutoka TAKUKURU au mamlaka husika?
  3. Je, kuna uwezekano wa waombaji ambao akaunti zao zilikuwa na hali ya “Pending” kupata majibu rasmi baada ya dirisha la maombi kufungwa?
Tunaomba ufafanuzi huu kwa sababu suala hili lina umuhimu mkubwa kwa maisha na mipango yetu ya baadaye. Baadhi yetu tumeshiriki katika hatua zote za usaili na tumekuwa tukisubiri majibu kwa matumaini, hivyo tunahitaji kujua kwa uhakika hali ya maombi yetu ili tuweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yetu.

Tunaomba TAKUKURU au mamlaka husika itupatie taarifa rasmi na ya wazi kuhusu maana ya “Pending” na hatua inayofuata kwa waombaji ambao hadi sasa hawajapokea majibu.

Tunawashukuru kwa muda na kwa kuzingatia ombi letu.

Wenu kwa heshima,
Kijana Mpambanaji
 
Kwa uzoefu wangu ukichaguliwa kwenda Kozi ya TAKUKURU CCP, Mkurugenzi Mkuu hukutumia barua ya WITO WA KUSHIRIKI MAFUNZO kwenye Email yako hivyo maelekezo yote ya kuripoti CCP tarehe nk huwa kwenye Barua hiyo.Sasa kama hujatumiwa Barua basi elewa hukuchaguliwa
 
YAH: OMBI LA UFAFANUZI KUHUSU HALI YA MAOMBI YA AJIRA TAKUKURU​

Ndugu zangu,

Mimi ni mmoja wa waombaji wa nafasi za ajira zilizotangazwa na TAKUKURU mwaka huu. Baada ya kutuma maombi, baadhi yetu tulipata nafasi ya kushiriki katika hatua mbalimbali za mchakato wa usaili, ikiwemo mtihani wa maandishi, mtihani wa vitendo pamoja na usaili wa mahojiano.

Baadaye, mwezi Septemba 2026, baadhi ya waombaji walipokea majibu kupitia barua pepe pamoja na akaunti zao za Ajira Portal. Hata hivyo, kuna baadhi yetu ambao hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2026 hali ya maombi kwenye akaunti zetu ilikuwa bado ikionyesha neno “Pending.”

Kuanzia tarehe 1 Oktoba 2026, baadhi ya waombaji tulipoingia kwenye akaunti zetu, tulikuta ujumbe ukisema “Dirisha la maombi limefungwa”, bila kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kuhusu maana ya hali ya awali ya “Pending.”

Kwa heshima, tungependa kupata ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika:
  1. Je, hali ya “Pending” iliyokuwa ikionekana kwenye akaunti zetu hadi tarehe 30 Septemba 2026 ilimaanisha kuwa mwombaji hakuchaguliwa (Not Selected)?
  2. Au hali hiyo ilikuwa bado inaashiria kuwa mchakato wa uteuzi ulikuwa unaendelea na kwamba waombaji hao wanapaswa kusubiri majibu rasmi kutoka TAKUKURU au mamlaka husika?
  3. Je, kuna uwezekano wa waombaji ambao akaunti zao zilikuwa na hali ya “Pending” kupata majibu rasmi baada ya dirisha la maombi kufungwa?
Tunaomba ufafanuzi huu kwa sababu suala hili lina umuhimu mkubwa kwa maisha na mipango yetu ya baadaye. Baadhi yetu tumeshiriki katika hatua zote za usaili na tumekuwa tukisubiri majibu kwa matumaini, hivyo tunahitaji kujua kwa uhakika hali ya maombi yetu ili tuweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yetu.

Tunaomba TAKUKURU au mamlaka husika itupatie taarifa rasmi na ya wazi kuhusu maana ya “Pending” na hatua inayofuata kwa waombaji ambao hadi sasa hawajapokea majibu.

Tunawashukuru kwa muda na kwa kuzingatia ombi letu.

Wenu kwa heshima,
Kijana Mpambanaji
Na pia kama majibu ni Not selected n vyema taarifa rasmi kupitia email itolewe kuliko kuwaacha watu hanging
 
Kijana uliyeuliza Mafunzo yamefunguliwa jana CCP,kwa kawaida huanza kuripoti wenye Digrii,kisha baada ya mwezi mmoja wenye Elimu chini ya Digrii ndio huripoti lakini kumaliza huwa wanamaliza siku moja
 
Attachments

  • Screenshot_20261009-091401.png
    Screenshot_20261009-091401.png
    144.8 KB · Views: 8
Kwahyo na wale wa diploma tayari wametumiwa jumbe kwenye email au bado
 
Kijana uliyeuliza Mafunzo yamefunguliwa jana CCP,kwa kawaida huanza kuripoti wenye Digrii,kisha baada ya mwezi mmoja wenye Elimu chini ya Digrii ndio huripoti lakini kumaliza huwa wanamaliza siku moja
Mkuu kwahyna wale wa diploma jumbe wamepata kupitia email
 
Wenye Diploma waliomba nafasi ya WACHUNGUZI au WACHUNGUZI WASAIDIZI??vyovyote ilivyo wote 500 waliochaguliwa walishatumiwa Email,kwa hiyo wameripoti kwanza WACHUNGUZI kisha WACHUNGUZI WASAIDIZI wataripoti mwezi ujao
 
Back
Top Bottom