popah21
Member
- Jun 8, 2023
- 13
- 6
Sisi wachimbaji wadogo kutokea mkoani Tanga wilaya ya Tanga kata ya Kiomoni mtaa wa Kiomoni, tunamuomba mheshimiwa raisi awaamrishe makamishna wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro waweze kutulipa fidia zetu, tumekua tukidai fidia zetu miaka na miaka kutokea mwaka 2021, tunasomesha watoto katika hali ngumu, tuliahidiwa tutalipwa fidia kutokana na mamlaka kuchua maeneo yetu tuliyokua tukiyamiliki kihalali kabisa, ila imefikia hatua hatuna namna zaidi ya kukuomba mheshimiwa raisi utusaidie, tunaishi katika mazingira magumu kwa zaidi ya miaka mitatu Sasa, wengine ni wajane tunaishi kwa tabu sana, tunakuomba mheshimiwa raisi uunde tume itakayokuja kushughulikia hili suala,