Elections 2010 Ombi langu kwa mawakala chadema.

Elections 2010 Ombi langu kwa mawakala chadema.

majata

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2010
Posts
431
Reaction score
180
Kazi kubwa ambayo imesalia sasa ni kuhakikisha kura zinalindwa na zinahesabiwa kwa uangalifu kwani ushindi upo wazi kwa Dr slaa, naomba mawakala wazingatie yafwatayo:
1. Wawe waaminifu na wapenda mabadiliko wa ukweli.
2. wakatae kabisa kupokea rushwa ilikubadilisha matokeo.
3. wawe makini wahakikishe wamejiandaa kisaikolojia na wahakikishe wamepumzika
vizuri kabla yakuingia chumba cha kupigia kura ili wasije kusinzia, nikosa kubwa.
4. Wawe wakali wanapoona mambo yanayoweza kuingiza udanganyifu kwenye kura.
5. watambue hatma ya watanzania wameishikilia wao.
na mwisho chadema wahakikishe wanatakwimu sahihi za vituo vyote vya kupigia kura na mawakala wao wote lazima wawe wamehakikiwa na tume ya uchaguzi kwani kuna tetesi za kuwepo vituo feki vya kura ilikuchakachua matokeo, na wahakikishe kila kituo wana mawakala.
 
Pia kuwe na mawakala mbadala kama sheria ya uchaguzi ya 2010 inavyosema ili Chadema watapoona mwenendo wa wakala sio mzuri basi anabadilishwa. Pia wapeane zamu, yaani ikifika saa tisa kabla ya kituo kufungwa saa kumi wakala aliyeanza asubuhi anaondoka na yule mbadala anaingia ili kuongeza ufanisi kwenye zoezi la kuhesabu kura na kulinda matokeo na kuweza kukaa mpaka anaweka sahihi na kuondoka na nakala ya matokeo (kila wakala au wakala mbadala lazima awakilishe nakala ya matokeo kwenye chama chake, hii itasaidia kuonesha kuwa wakala amekuwapo mpaka mwisho). Nasema hivi kwa sababu zoezi linaweza kwenda mpaka saa nane au tisa za usiku.

Pia mawakala wasikubali vyakula kutoka kwa watu wengine, kwani wanaweza kujikuta wakati wa kuhesabu kura na kubandika matokeo wanapiga usingizi wa kufa mtu. Wachukue maji ya kilimanjaro - chupa kubwa, biskuti za glucose za kutosha, na simu zao ziwe na vocha za kutosha, wapige picha matukio yote ya kutatanisha kama simu zina kamera au ata kurekodi!
 
Agenda ya mawakala tuijadili sana kwa kila siku ili kupata mbinu mpya lengo ni kudhibiti kura kuibiwa
 
Back
Top Bottom