Kwanza kabisa TAMISEMI hamkua na ulazima wa kutoa ahadi ya ajira kwa walimu wapya ifikapo 25/04/2015. Tamko mlilolitoa limeathiri watu wengi kisaikolojia, hivyo mkiwa kama taasisi yenye dhamana kubwa katika nchi yetu hii ya amani hamna budi kuita upya waandishi wa habari na kuomba radhi kwa kile kilichotokea tofauti na matarajio ya wengi. Hivyo basi mtoe sababu ya sintofahamu hii na kisha mseme kile mnachodhani kitakua muafaka wa ajira hizi. Natanguliza shukrani za dhati.