Ombi langu Simba day: Wazomeeni magarasa wakitambulishwa

Kwa upande wangu nilikuwa nahisi mambo mawili ambayo ni tatizo Simba ni fedha na uongozi. Nashukuru sasa kujua mojawapo ni hakika sasa kuwa fedha ni shida pale Simba.

Lakini hata mkopo wa kulipa sehemu tu ya mshahara wa mchezaji umeshindikana?
 
Bwana njaalikali ngoja nikusaidie jambo, Mimi ni mwananchi lakini kwenye fact sipepesi macho, Uyo kagere na mugalu bado wana mikataba ya mwaka mmoja mmoja kila mtu, simba kwa sasa awana pesa ya kuvunja mikataba yao, wameona kwakuwa caf imeruhusu kusajili wachezaji 40 watakaotumika kwenye michuano ya kimataifa tu nafikiri wameamua wawaache wawe wanatumika michuano iyo tu kuliko kuvunja mikataba yao, na timu ikiondolewa kwenye iyo michuano watajua namna nyingine ya kumalizana nao, hivyo basi tatizo kubwa hapo ni pesa ya kuvunja iyo mikataba
 
Akili na mawazo ya kitumwa na kipumbavu kwamba wachezaji wazawa ni magarasa, simba inao kina mkude, inao kina KAPOMBE, Hussein inaye Manula, Boko walisajiliwa kutoka wapi? Simba iliyowahi kuitoa ZAMALEK pale Misri ilikuwa na kina PAWASA,ULIMBOKA,JUMA KASEJA walisajiriwa kutoka wapi? Akili zile ukipanda papai likazaa sana linaitwa la kizungu.
 
Ao wachezaji wa nyumbani wanahitaji fedha, ndio maana Dili la Mpole limeshindikana tatizo ni fedha.
 
Ao wachezaji wa nyumbani wanahitaji fedha, ndio maana Dili la Mpole limeshindikana tatizo ni fedha.
BIASHARA ni zaidi ya pesa , jaribu kuangalia hata huko Ulaya, kuna wakati timu kubwa zinapambana na deal zina shindikana. Nakama umetambua tatizo ni hela wewe umefanya nini kuisaidia timu yako? Umesahau hii ni timu ya wanachama? Kanunue mchezaji mmoja basi uisaidie kamati ya usajili. Jezi tu ya elfu 30 hutaki kununua au huwezi kununua hela zinatoka wapi? uwanjani huendi unatizama mechi vibandani hela timu inapataje hela?
 
Ahmad Ali alishatoa ufafanuzi kuna wachezaji wanatakiwa waachwe lakini wana mikaba mirefu bado na ni wengi hvyo huwezi vunja mkataba wanasubiriwa wamalize mikataba yao kwanza umeelewa utopolo.
 
Hao wachezaji wote wanesajiliwa na kicha mpya, ni matakwa ya kocha wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…