OMBI MAALUM: Naomba kujulishwa gharama za ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

OMBI MAALUM: Naomba kujulishwa gharama za ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Heri ya Krismas.

Ikulu kuu ya Taifa ya Chamwino iliyopo Dodoma ni Ikulu namba moja duniani kuwa na eneo kubwa sana la Aridhi. Sijasema ni Ikulu kubwa bali ndiyo namba moja kuwa na aridhi kubwa iliyotengwa kwa eneo la Ikulu tu. Majengo tu yamechukua ekari nane na eneo kubwa sana bado limebaki.

Ikulu hii tuliambiwa itajengwa kwa gharama ndogo na SUMA JKT bila kushirikisha wakandarasi binafsi ambao hutumia miradi ya serikali kama mtaji.
Sasa naomba kujuzwa gharama zote za ujenzi wa Ikulu hii kwani ni kama vile kuna USIRI. Mfano siku ya ufunguzi serikali ilikwepa makusudi kutaja gharama hizo.

Kwa Heshima na Taadhima kama mwanainchi naomba kujua gharama za ujenzi za ofisi yetu kuu hii ya Taifa.

Ahsante.
 
Ni ktk kuwaenzi wajenzi Dr Magufuli, Dr Samia na Charles Mbuge aliyesimamia Suma JKT. RIP kwa hao wawili.
Mafundi Wanaojenga majengo nyeti kama haya huwa wanaondoka mapema. Sijui kama wale madogo wako poa
 
..gharama za ujenzi wa ikulu ni sawa na ujenzi wa viwanda vingapi?
 
Back
Top Bottom