OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Hapa hatujadili mapenzi,tunalalamikia mauaji yanayoendelea kuhusiana na wivu wa kimapenzi.
Vifo vingi vinavyoendelea kuripotiwa vimehusishwa na wivu wa kimapenzi. Wanandoa wanauana na kudhuliana. Wavamizi wa ndoa wanauana na kudhuliana.
Taifa linazidi kupoteza nguvu kazi na jamii zinapoteza kaka,dada,ndugu mbaya zaidi kuna watoto wanapoteza mama au baba na kupoteza mwelekeo. Inatia uchungu sana.
Ukisoma habari hizo huwezi kuacha kujifikiria matukio uliyopiga na mke au mume wa mtu. Unajiuliza "Hivi na mimi ningedakwa pale gesti si ningecharangwa mapanga?".
Kwa kweli nimeanza kupata uoga sana na kukumbuka matukio kadhaa niliyowahi kupiga-ujana mbaya sana.
Lakini kuna matukio mengine wala hujui kama ni mke wa mtu. Sometimes unaulizia anaficha na pengine kavua pete ya ndoa.
Unabeba unapiga unakolea. Siku ya siku unadakwa na mwenyewe!! Unawaambia watekaji mimi sikujua hawaelewi.
Pamoja na hatua zingine za kuchukua,wake za watu wana nafasi ya kutuokoa. Wawe wanasema kweli,ili wale tusiotumia wake za watu tusikusogelee.
Naandika kwa uchungu kwa sababu jamaa yangu kaopoa dada huku ugenini. Kumbe yule dada ni mke wa askari na ameshashindikana.
Askari anamtafutia target tu kujua nani anamuibia mke. Yule askari alishajiapiza siku akimdaka anakimbilia bunduki polisi anakuja kuua.
Nasisitiza kwa wake za watu ukitongozwa kataa mwambie mtongozaji wewe umeolewa. Utakuwa umeokoa nguvu kazi ya taifa