Ombi maalumu: Tafadhali mwenye mawasiliano na Mjumbe yoyote aliyeteuliwa na Rais kupitia Upya misururu ya Kodi TRA anifikishie ujumbe huu muhimu

Hili jambo ni serious sana TRA unamkataje Kodi mtu aliyefuluzwa kazi bila kujali atapata kazi au laaa?

HUU NI UONEVU.
 
Umesoma vizuri hilo andiko?

Umeambiwa mtu aliyefuluzwa kazi au kwa lugha nyepesi aliyestaafishwa kwa lazima na Mwajiri kwanini akatwe Kodi?

Je, malipo anayolipwa sio pension fund Ile?
 
Umesoma vizuri hilo andiko?

Umeambiwa mtu aliyefuluzwa kazi au kwa lugha nyepesi aliyestaafishwa kwa lazima na Mwajiri kwanini akatwe Kodi?

Je, malipo anayolipwa sio pension fund Ile?
Sawa kabisa hii,
 
Sasa mtu Kafukuzwa kazi Kodi ya Nini tena hapo mbona kama huu ni uuwaji wanafanya TRA?
 
HUU NI UONEVU WA KIWANGO CHA JUU SANA KWA WAFANYAKAZI WALIOPATA MATATIZO KAZINI
 
Japo muhimu sana hili lizingatiwe na tume
 
Nimesoma andiko lako zuri ila eneo moja tu utawalaumu TRA. TRA wao wanatekeleza sheria zilizotungwa na kupitishwa bungeni na wasipozifata huwa wanachukuliwa hatua kama vile CAG kwenye kaguzi zake , PCCB n.k. Nadhani cha msingi ni kuomba kamati ipendekeze muswada katika bunge lijalo la marekebisho ya sheria kulitizama upya. Tukisema TRA wao wataendelea tu sababu ni sheria hawana budi kutizimiza takwa la sheria.
 
Ni sheria ndiyo inayoelekeza TRA kukusanya hiyo pesa kwa sababu hata kama mtu kafukuzwa kazi alicholipwa ni ni haki yake kwa maana mshahara wake. Na sihivo tu hata pension kwa sasa ukipokea mshahara haikwatwi kodi wanachukua mshahara toa pension kinachobaki kinakatwa kodi. Mwisho ukija chukua pension yako ndiyo utakutana na kodi sababu ni mapato. Sheria ya kodi inasema mtu atakatwa kodi kwenye uwekezaji, biashara na ajira hivo mapato yoyote hapo unakatwa kodi. tra wao wanapewa sheria hizi kuzisimamia na kuhakikisha wanakusanya kwa mujibu wa sheria hizi. Cha msingi ni uomba tume hii ipitie hili na liweze fanyiwa marekebisho kwa kupitia Bungeni lasivyo TRA wataendelea sababu ni sheria wamepewa kutimiza.
Mfano nimesoma hapa kakitabu ka tra
anayepata smahara 270,000 kwa mwezi halipi kodi
270,000 mpaka 520,000 8% atakatwa kwa kile kinachozidi 270,000 yaani 520,000-270,000=250,000 ndiyo itakatwa 8%
na 520,000 mpaka 760,000 atakatwa 20% ya kinachozidi 520,000+20,000
760,000 mpaka 1,000,000 atakatwa 25% inachozidi 520,000+68,000
na zaidi ya 1,000,000 kinachozidi atakatwa 30% +128,000
 
Nadhani ndio maana ujumbe unakwenda kwa Wajumbe wa tume ya Rais ili wafanye hayo
 
Acha kuwaonea TRA bure. TRA hawatozi kodi kwa utashi wao; ni sheria zilizopitishwa na Bunge (akiwemo mbunge wako). Kwa hyo jikite kwenye marekebisho ya sheria zilizopo na sio kuwalaumu TRA
 
Acha kuwaonea TRA bure. TRA hawatozi kodi kwa utashi wao; ni sheria zilizopitishwa na Bunge (akiwemo mbunge wako). Kwa hyo jikite kwenye marekebisho ya sheria zilizopo na sio kuwalaumu TRA
Siku zote TRA ndiko wanalaumiwa hata kama wao hawajatunga hizo Sheria but this is collective responsibility
 
Unahoja ya msingi na nadhani hii Rais mwenyewe aiangalie kwa ukaribu sana
 
Hii inasikitisha sana,😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…