World light
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 382
- 352
Ukinunua dai Risiti,
Ukiuza toa Risiti.
Mhe Mjumbe habari,
Kwanza, natumia jukwaa hili kukupongeza wewe binafsi pamoja na wenzako wote kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa wajumbe wa Kamati hii maalum ya kusikiliza sauti za wasiokuwa na sauti juu ya Kodi mbalimbali kandamizi hapa nchini.
Mhe Mjumbe, TRA kupitia Sheria mbovu wamekuwa wakiwaonea wafanyakazi wa Tanzania kupitia pay as you earn [PAYE] hasa pale mfanyakazi anapopata matatizo kazini na baadae kumaliza mgogoro ule na mwajiri wake kisha kuondolewa kazini na mwajiri huyo kwa mujibu wa Sheria na Mwajiri kulazimika kumlipa mishahara yake yote iliyopita au ijayo kwa mkupuo ( Lump sum)
Mhe Mjumbe, Mapato anayoyapa mfanyakazi huyu asiye na ajira baada ya kufukuzwa kazi hayana tofauti kabisa na "PENSION FUND" hasa pale Mwajiri anapogoma kumrejesha kazini Kwa mujibu wa Sheria kwani anayo hiari ya kufanya hivyo.
Mhe mjumbe, Ile Mishahara anayolipwa kwa Mkupuo ndio pesa pekee anayobakiwa nayo mfanyakazi huyu wa Kitanzania baada ya kukosa ajira maana yake hiyo ni sawa kabisa na PENSION FUND kwanini ikatwe Kodi?
Mhe Mjumbe, Ni kwanini basi TRA wanawatoza wafanyakazi hawa Kodi tena ya kiasi cha asilimia 30 ya kiasi watakacholipwa kama malimbikizo kwa pamoja au Mkupuo (lump sum).
Kwanini 30% kwa mtu mwenye Mshahara wa laki 4 iliyokusanywa?
Mhe Mjumbe, Tutafakari hili vizuri, Kweli mtu anayelipwa tupesa twake tena pengine Mwajiri wake kaamua kuachana nae ili vimsaidie kufungua kabishara ili ale na wanae kisha afe nyie mnagawana nae karibu nusu kwa nusu lazima tuwe na huruma hasa kwa hawa wanyonge tunaowaongoza waliokosa ajira.
Mfanyakazi akifukuzwa kazi hana tofauti na yule aliyestaafishwa kwa lazima kwa maoni ya wengi hatakiwi kukatwa Kodi ya aina yoyote kwani anacholipwa hakina tofauti na Pension funds.
Nashauri Kodi hii iondolewe Mfanyakazi akishinda kesi na Mwajiri akagoma kumrejesha kazini basi Mishahara yake isikatwe Kodi kwani mapato hayo hayana tofauti na Pension funds.
Asante naomba kuwasilisha.
Mungu awaongoze vema ili mlisaidie Taifa na Rais wetu.