Uchaguzi 2020 Ombi: NEC iwapime akili wagombea ubunge wa upinzani kabla haijawapitisha ili kupunguza chaguzi ndogo baadae!

Nadhani ombi lingekua CCM iache rafu za uchaguzi ili wananchi tuchague viongozi tunaowataka .na wenyewe wakae pembeni ili kuepusha nunua nunua ya wapinzani.
 
Na pia Chadema iwape vyeti wagombea wake kuthibitisha kuwa wamewafanyia vetting ya kutosha na kujiridhisha hawana njaa". Hii itazuia wanachama wa Chadema kuanza kuwasema vibaya wanapohama.
 
Mkuu hiyo sheria haitaweka na ccm kamwe.sababu hakuna mbunge anaweza kujiudhuru akijua hatorudi tena bungeni maisha yake yote
 

No problem bwashee. Hakuna hasara hapo; it’s value for the money.

Mara hii umesahau kwamba sisi Tanzania mikakati ya kisiasa ndio kipaumbele chetu? Nini marudio ya chaguzi? Pesa za manunuzi je? Unajua bei za wanunuliwa? You’re given an offer you can’t refuse or it’s curtains for you. Ni mwendo wa ki-Sisilia tu. Fikiria naibu waziri hadi haoni taabu kujilipua kuwa alikuwa kwenye mpango wa kumtiririshia shaba TL! Yaani hajali familia/ndugu zake watamchukuliaje.

Fikiria ufisadi unaofanywa na wawezeshaji wa manunuzi. Cha juu wanachochukua. Fikiria malipo ya kandarasi za wasiojulikana. Umeshawahi kupiga hesabu hela inayotumika kufanikisha propaganda nchini? Halafu CAG hagusi huko! Au unadhani akina ulanzi wetu wanafanya kazi ya kanisa hapa JF. Huu ni msimu wa neema kwa walio kwenye timu ya ushindi. Unataka kutoboa mtumbwi? We kamata bia, achana na Waitara; atakusaidia nini?
 
Samahani , hivi hawa wanaojiita MATAGA huwa wanataga nini? Mayai kama Tausi au nini hasa?
Hawa uvccm walimuiga slogan ya Trump Make America great again wakawa Wa asema 'Make Tanzania Great Again" - Mataga
 
Mimi napendekeza wote wapimwe hata ccm pia maana kuna wengine wamedai wanapenda "ukichaa_kichaa".
Ccm wakipima hata Mwenyekiti hatoboi. Atatoboa Jokate tu. KWa hio bibie atakuwa rais mondi akitaka kujipigia anapiga tu president Wa mataga
 
Kwanza kabisa Yohana ibara ya 67(2)(b) imeweka wazi mbunge lazima agombee akiwa mwenye akili timamu. Hili la kuwapima ni kama kupoteza muda.
Ila hawa wa upinzani kuhama nafikiri wengi wamehama baada ya kufanyiwa mabaya. We fikiria unachangia chama kwa nia njema laki tano kila mwezi. Alafu fixed account ajiri ya uchaguzi. Baada ya muda hela. Imeyeyuka hapo hata kama una akili timamu lazima uhame.
Unalazimishwa ukae lockdown kisa tu muikomoe serikali ambayo haijaweka lockdown. Hapo lazima uondoke. Vyama. Vingine ni matatizo.
 
..."Hakuna.chama cha Siasa kilicho bora,kuliko uhai wa binadamu"...Na.Mwigulu Nchemba-Katoro...nimesahau mwaka,mwezi,siku,na tarehe.
 
Anza na wanaojiita matanga, huku kwetu mstanga ni tusi, kamwe siwezi jitusi kwa kujiita matanga aka fisiemu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acha matusi mkuu, huyu Waitara ni mlevi tu na asiye utu lakini anaakili timamu.

Tuweke kanuni,atakayeachana na ubunge kwa hiari yake ama hata kufukuzwa chama husika kizibe hilo pengo.

Hawa wahamaji wakae miaka 5 ndiyo wagombee tena.
 
..Kumbe mwanachama akinunuliwa,chama.kinakuwa kimenunuliwa...?!Samahani.lakini
Hapana, ila kinaonyesha udhaifu mkubwa kuwatathmini watu wake kinaowakabidhi uongozi. Samahani lakini.
 
Wapimwe wote ccm, chadema, Tlp, Act, nccl yani wote maana kuna maccm mengine nayo kichwani ni Nazi tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…