Ombi: Serikali iwalipe mshahara watumishi waliotia nia Ubunge

Mheshimiwa M/KITI WA CCM NA RAIS WA JMT,

Narudia kukukumbusha kuwa 'KIBURI SI MAUNGWANA'

Huo ni msemo wa kiswahili lakini una maana kubwa sana. Endapo mwezi huu wa nane makada wa CCM ambao ni watumishi wa Umma wapatao elfu 7 na zaidi hawatalipwa mishahara yao ya mwezi wa nane...basi tegemea kuanguka kwa chama katika taasisi nyingi za Umma na chama hakitaungwa mkono na hilo jeshi.

Lakini kwa kuwa unaamini kuwa CCM itashinda kwa kishindo basi subiria wahanga/ wajuba wauze ramani .

Narudia tena : walipe mshahara was wa mwezi wa nane.....FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE!

HUO NI USHAURI AS BURE TU !
 
nikweli kabisaaaa
 
naunga mkono hoja,ubabe waache kabisa
 
nakwambia ramani ikiuzwa,nyumba haina siri tena
 
Polepole: CCM inawataka wagombea wote waliofeli kura za maoni kuwapigia kampeni washindi watakaokaidi kukosa teuzi!
 
Kiufupi watumishi wote waliotia Nia wamesimamishwa kazi kwa miezi 6, mama yangu mdogo ni muhanga, Ni vilio kila siku, CCM wamekuwa wakatili Sana this time around
 
Hapo ndio wajue gharama za kusogezaa majina yao jiweni! kwani vyama vingine watumishi wa umma hawakujitokeza? AU sio rahisi kujipambanua hivyo kwa wakati tulioonao!!
 
Kwani tuliwatuma? “toshekeni na kazi zenu au kuweni risk takers”
 
Mtu analilia mshahara wa mwezi mmoja kiasi hicho? hivi akikosa mshahara mwaka si atajiua?.
 
Mlienda kugombea mkiwa mtamba sana acha kidogo mhenyeshwe ikimpenda rais awafukuze kazi maana mna uchu wa madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…