Ombi: Serikali ya Tanzania ipeleke agenda African Union (AU) ya kuwakatia eneo la makazi waafrika waliochukuliwa utumwani ili warejee nyumbani

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,891
Wananzengo, waswahili walisema maji hufuata mkondo.
Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
Akumulikaye mchana, usiku akuchoma.
Nakadhalika na kadhalika.

Tumeshuhudia kasi ya mateso na chuki kwa watu weusi ikipanda kiwango kila bara. Mtu mweusi anaonakana kama ni mtu ambaye utu wake ni wa kiwango cha chini kuliko binadamu. Mambo haya yamejidhihirisha miaka 400 (mianne) iliyopita ambapo mtu mweupe alianza kuchukua watumwa kutoka Africa. Watu wetu walitenganishwa na familia zao pasipo ridhaa.

Vilio na misiba ilizagaa katika kya. Mungu Samehe viongozi wetu waliokuwa wajinga, wabinafsi na dhaifu kwa kuamua hata kuwakamata vijana na kuwauza. Wengi walipoteza uhai kwa sababu mbalimbali kabla hawajafika walikokuwa wakienda. Waliofika utumwani walihesabiwa kama wanyama na si binadamu. Wengi waliuliwa kikatili na waliosalia walichukuliwa kama mifugo.

Baada ya kufutwa kwa utumwa, hao ndugu zetu walianza kuishi maisha yaliyobatizwa uhuru, wakati uhalisia ni kwamba kulikuwa na mapinduzi ya uzalishaji kiuchumi na hivyo hapakuwa na hitaji la watumwa tena. Hao ndugu zetu wameendelea kuishi katika jamii ambazo hazijabadilisha mentality kuhusu ubinadamu wetu.

Sote tunaona namna ubaguzi anaofanyiwa mwafrika sehemu nyingi duniani. Matukio yanayodhihirisha dhana hii ni mengi sana. Lakini tunaona kila siku yanayotokea kwa watoto wetu wanaokwenda uarabuni; tunaona mfano wa mauaji na George Floyd, mwafrika mwenzetu aliyepelekwa utumwani marekani na hatimaye anauawa hadharani kwa kuzuiwa kupumua huku akiwa amefungwa pingu mikono mgogoni.

Tumejionea namna hao wakamata watumwa, vile hasara waliyotusababishia kwa kutuchukua utumwani kwa nguvu, na kuacha familia huku zikilia vilio, walivyo na mitazamo miovu dhidi yetu kiasi cha kutangaza kutudunga sindano za majaribio za chanjo kwa lazima badala ya wanyama. Mahusiano ya kiuchumi yanaomfanya mtu mweusi kuendelea kuwa mtumwa kwa ngozi yake, na hata wanavyopanga kutupunguza eti dunia iwe na watu wachache kwa kupitia chanjo, na kadhalika na kadhalika.

Tuendelee kukubali kutumikishwa na hata kuuawa kwa maslahi ya rangi fulani ya ngozi? Ni nini ambacho hatuwezi hata tusiwe na dhana ya kujitegemea? Ni kweli hatuna elimu, raslimali wala uwezo wa kuzalisha mali na kuuziana wenyewe? Hatuna wataalamu wanaoweza kusimamia dhana ya kuj itegemea katika Africa, ili tupandishe kiwango hata tujenge msingi wa kuheshimiana na wafanyabiashara za binadamu weusi? La hasha.

Vipi ndugu zetu wanaotaabika vizazi na vizazi ughaibuni ambapo wanauawa kama chawa tena hdharani? Mmeona clip inayozungumzia wagonjwa wa Korona wakiwa hospitalini wenye ngozi nyeusi wanauliwa? Mmesikia hawa mawakala wa shetani wakitabiri Africa ingejaa mizoga ili kuwatia hofu waafirka kusudi wakubali kuchanjwa chanjo ambayo ni sumu na ywatu wawe watumwa tena watumwa wa hiyari?

Ndugu zangu huu ni muda wa mabadiliko si ya kabila wala ukoo mmoja mmoja.

Watu wote wenye rangi ni familia moja. Unajuaje kama George Floyd ni kaka ama mwanao kwa damu? Waarabu waliwaua na kuwahasi waafirka baada ya utumwa. Hata hawakutaka kuwaona. Tunasahau hayo, tunatuma watoto wetu wakawe wtumwa katika hizo nchi.

Ninaomba tuamke.

Ninajua viongozi wetu wanasoma haya mabandiko. Ninaomba serikai ya Tanzania ipeleke agenda AU ya kuwarejesha ndugu zetu walio utumwani katika nchi za ugeni.

Afrika ni bara kubwa na kuna sehemu kubwa hazijajaa. Waangalie nchi kama DRC ambayo ni kubwa sana ikiwa haina watu. Badala ya kuiacha kama maficho ya vita vya ndani, waigawanye sehemu moja wapewe ndugu zetu waliouhamishoni, wanaotaka kurudi Africa warudi wafanye nchi yao. Hii itawapa tumaini jipya la maisha kwa vizazi vyao kuliko hali ilivyo sasa ambapo mtu akitoka nyumbani, hamna hakika kama atarudi.

Agenda nyingine ya kusimamia ni kuimarisha mfumo wa uzalishaji na uhusiano wa kibiashara katika nchi zote za Africa ili tuondokane na udhalilishwaji wa kukataliwa sisi na kila kitu chetu hata kama hakina madhara. Mfano dawa ya Madagascar, raisi walivyoambiwa apewe dolla millioni ishirini ili aweke sumu kwenye hiyo dawa. hii ni dhahiri kwamba hawa watu hawataki dawa ipatikane, na wakitaka watu wafe kwa sababu wana agenda na korona hii.

Ninaomba tuendelee kujadiliana kama unapumzi. Wale walioishiwa pumzi hata hawaoni ubaya wa yote yanayotokea, ama kudhani hayawahusu, wanaweza kusoma tu na kupita bil kuchangia.

Karibuni
 
Wazo zuri........ Warudi Nyumbani Sasa.
 
Wale nugu wana matatizo makubwa sana.. kubaguliwa hawataki na kurudi Afrika hawataki. Nao wanaonaga huku ni bara la giza.
 
Eti Eminem hua anasema anaamini yeye ni mwafrica huku Pdiddy akisema anaamini yeye asili yake ni Ethiopia/Somalia.

Maanina hawa jamaa wanacheza waje huku wajionee mziki mnene eti huko US mtu mmoja tu anauwawa then wanaandamana mpk police wanapiga magoti kuomba msamaha aje ajionee huku kwa afande Mroto mtu anapigwa anakufa na nyie mliobaki mnaambiwa mtapewa kichapo cha mbwa mwizi na maisha yanaendelea poa kabisa.
 
Afrika ni motherland ya waafrika na wote wenye asili ya Afrika.
 
Waende Mashariki ya Kati, kule kutawafaa Sana.

Kiongozi, kule lndiko walitumikiswa na baada ya kuisha thaman yao ki uchumi waliuliwa na wengine kuhasiwa. Kuwapeleka kule ni kuwaokoa kwenye giza na kuwatumbukiza kwenye tanuru la moto. Kule hakufai kiongozi.
 
Afrika ni motherland ya waafrika na wote wenye asili ya Afrika.
You are right Richard. Let them come back rather than the horrible treatments they have been enduring for more than 400 years.
 
Wakirudi watakuwa wanaona sisi tuliozaliwa hapa hapa ni manyani wao ni better. Waliorudishwa Liberia walifanya hivyo mpaka leo decendants wao ndiyo first class na waliowakuta second class.
Kwanza ukweli ni kwamba hawataki kurudi, na ndiyo maana hata na pesa yao mtu kama floyd mayweather mara ngapi umemsikia kaja africa hata kutalii.
 
hapa Tz kwenyewe wakulima na wafugaji hapatoshi na kuna timbwili la kutosha tuu, alafu uongezee headache nyingine, kwanini msiwaalike jirani na ndugu zetu wa Kenya na Rwanda waje kumiliki Ardhi kwanza alafu ndiyo wafuatie hao ma -yo yo yo madhafaka!
 
Ni kwa sababu hawana pa kwenda. Wakipewa nchi, wanaishi kwao na nchi zilizowachukua utumwa zinalazimishwa kuwafidia.

Nafikiri serikali ya Tanzania inaweza kuwasaidia raia wake waishio nje ambao wanataka kurudi nyumbani.

Serikali kupitia kitengo maalum kwa ajili ya diaspora kinaweza kuandaa sera na mikakati maalum ya kuwakaribisha watanzania hao na kila nchi ikafuata.

Ila kwa sababu za kiusalama na kisiasa haiwezekani kuwaandalia hao sehemu moja na kuachia waende hapo halafu wasettle italeta taabu.

Tunayo mifano ya Haiti na Liberia.
 
Wananzengo, waswahili walisema maji hufuata mkondo.
Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
Akumulikaye mchana, usiku akuchoma.
Nakadhalika na kadhalika.

Tumeshuhudia kasi ya mateso na chuki kwa watu weusi ikipanda kiwango kila bara. Mtu mweusi anaonakana kama ni mtu ambaye utu wake ni wa kiwango cha chini kuliko binadamu. Mambo haya yamejidhihirisha miaka 400 (mianne) iliyopita ambapo mtu mweupe alianza kuchukua watumwa kutoka Africa. Watu wetu walitenganishwa na familia zao pasipo ridhaa.

Vilio na misiba ilizagaa katika kya. Mungu Samehe viongozi wetu waliokuwa wajinga, wabinafsi na dhaifu kwa kuamua hata kuwakamata vijana na kuwauza. Wengi walipoteza uhai kwa sababu mbalimbali kabla hawajafika walikokuwa wakienda. Waliofika utumwani walihesabiwa kama wanyama na si binadamu. Wengi waliuliwa kikatili na waliosalia walichukuliwa kama mifugo.

Baada ya kufutwa kwa utumwa, hao ndugu zetu walianza kuishi maisha yaliyobatizwa uhuru, wakati uhalisia ni kwamba kulikuwa na mapinduzi ya uzalishaji kiuchumi na hivyo hapakuwa na hitaji la watumwa tena. Hao ndugu zetu wameendelea kuishi katika jamii ambazo hazijabadilisha mentality kuhusu ubinadamu wetu.

Sote tunaona namna ubaguzi anaofanyiwa mwafrika sehemu nyingi duniani. Matukio yanayodhihirisha dhana hii ni mengi sana. Lakini tunaona kila siku yanayotokea kwa watoto wetu wanaokwenda uarabuni; tunaona mfano wa mauaji na George Floyd, mwafrika mwenzetu aliyepelekwa utumwani marekani na hatimaye anauawa hadharani kwa kuzuiwa kupumua huku akiwa amefungwa pingu mikono mgogoni.

Tumejionea namna hao wakamata watumwa, vile hasara waliyotusababishia kwa kutuchukua utumwani kwa nguvu, na kuacha familia huku zikilia vilio, walivyo na mitazamo miovu dhidi yetu kiasi cha kutangaza kutudunga sindano za majaribio za chanjo kwa lazima badala ya wanyama. Mahusiano ya kiuchumi yanaomfanya mtu mweusi kuendelea kuwa mtumwa kwa ngozi yake, na hata wanavyopanga kutupunguza eti dunia iwe na watu wachache kwa kupitia chanjo, na kadhalika na kadhalika.

Tuendelee kukubali kutumikishwa na hata kuuawa kwa maslahi ya rangi fulani ya ngozi? Ni nini ambacho hatuwezi hata tusiwe na dhana ya kujitegemea? Ni kweli hatuna elimu, raslimali wala uwezo wa kuzalisha mali na kuuziana wenyewe? Hatuna wataalamu wanaoweza kusimamia dhana ya kuj itegemea katika Africa, ili tupandishe kiwango hata tujenge msingi wa kuheshimiana na wafanyabiashara za binadamu weusi? La hasha.

Vipi ndugu zetu wanaotaabika vizazi na vizazi ughaibuni ambapo wanauawa kama chawa tena hdharani? Mmeona clip inayozungumzia wagonjwa wa Korona wakiwa hospitalini wenye ngozi nyeusi wanauliwa? Mmesikia hawa mawakala wa shetani wakitabiri Africa ingejaa mizoga ili kuwatia hofu waafirka kusudi wakubali kuchanjwa chanjo ambayo ni sumu na ywatu wawe watumwa tena watumwa wa hiyari?

Ndugu zangu huu ni muda wa mabadiliko si ya kabila wala ukoo mmoja mmoja.

Watu wote wenye rangi ni familia moja. Unajuaje kama George Floyd ni kaka ama mwanao kwa damu? Waarabu waliwaua na kuwahasi waafirka baada ya utumwa. Hata hawakutaka kuwaona. Tunasahau hayo, tunatuma watoto wetu wakawe wtumwa katika hizo nchi.

Ninaomba tuamke.

Ninajua viongozi wetu wanasoma haya mabandiko. Ninaomba serikai ya Tanzania ipeleke agenda AU ya kuwarejesha ndugu zetu walio utumwani katika nchi za ugeni.

Afrika ni bara kubwa na kuna sehemu kubwa hazijajaa. Waangalie nchi kama DRC ambayo ni kubwa sana ikiwa haina watu. Badala ya kuiacha kama maficho ya vita vya ndani, waigawanye sehemu moja wapewe ndugu zetu waliouhamishoni, wanaotaka kurudi Africa warudi wafanye nchi yao. Hii itawapa tumaini jipya la maisha kwa vizazi vyao kuliko hali ilivyo sasa ambapo mtu akitoka nyumbani, hamna hakika kama atarudi.

Agenda nyingine ya kusimamia ni kuimarisha mfumo wa uzalishaji na uhusiano wa kibiashara katika nchi zote za Africa ili tuondokane na udhalilishwaji wa kukataliwa sisi na kila kitu chetu hata kama hakina madhara. Mfano dawa ya Madagascar, raisi walivyoambiwa apewe dolla millioni ishirini ili aweke sumu kwenye hiyo dawa. hii ni dhahiri kwamba hawa watu hawataki dawa ipatikane, na wakitaka watu wafe kwa sababu wana agenda na korona hii.

Ninaomba tuendelee kujadiliana kama unapumzi. Wale walioishiwa pumzi hata hawaoni ubaya wa yote yanayotokea, ama kudhani hayawahusu, wanaweza kusoma tu na kupita bil kuchangia.

Karibuni
Wale ni black American na si waafrika nchi yao sahihi ni huko huko walipozaliwa.Shida za Africa awaziwezi.Ni heri kuishi kwenye ubaguzi lakini kwenye Neema kuliko kuishi ushenzini.Mwarabu na Mzungu wao walikuwa ni wanunuzi wa watumwa mkamataji alikuwa ni mwafrika anamkamata mwafrika mwenzake Kisha anamuuza kwa kupewa nguo,shanga,vioo,bunduki ili akavamie jirani zake tumeona machifu wakiuza Mateka wa Vita,tumeona wajomba wakiuza wapwa zao nk.Nadharia ya ubinafsi ni Jambo la asili halikuanza leo hata wanaokaa kimya Sasa huku Jamii ikiteseka sababu ni wanufaika ni muendelezo wa asili ya ubinafsi wa mwafrika kiasili.Wanunuzi wa watumwa walipita vijijini wakiwa na watumwa ambapo wanakijiji wangetaka kukomesha hio biashara wangeweza hata kwa kuwauwa kwa kuwashambulia wanunuzi image watu 10 watazidiwa vipi na umati wa Kijiji wakiamua kuwashughulikia ni kwa sababu wao waliona ayawahusu vivo vivo Kama ilivo Sasa wanufaika sababu wanashiba yatendekayo uona hayawahusu ni Hadi maslai yao yatakapoguswa.
Africa ni ngumu kuendelea sababu ya mifumo mibovu ya uongozi,ni Hadi tu Kama itabadilishwa.
Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake.Suala la ukatili mwafrika anamtendea mabaya mwafrika mwenzake kuliko hata mkoloni alivomtendea mwafrika,wengi wamezikimbia nchi zao Kama wakimbizi toka Africa na kupewa hifadhi USA,na Canada sababu ya watawala kuendekeza tumbo kwanza Jamii baadae,So hata wakifikiria kurudi Africa watakutana na madhila makuu kuliko hata huko walipo.Race zote zina good people na bad people.Huko Uarabuni wengi tu wameishi vizuri na mabosi zao huku wakiwa msaada Mkubwa sana kwa familia zao nyumbani kwa kuziinua kimaisha Hadi wengine wameolewa huko.Suala la ukatili ni race zote hata tz dada wa kazi utendewa ukatili kuliko hata watendewao na weupe kupigwa,kubakwa, kunyimwa haki zao,kuzulumiwa mishahara,kukosa likizo,ujira Mdogo,nk.
 
Wakirudi watakuwa wanaona sisi tuliozaliwa hapa hapa ni manyani wao ni better. Waliorudishwa Liberia walifanya hivyo mpaka leo decendants wao ndiyo first class na waliowakuta second class.
Kwanza ukweli ni kwamba hawataki kurudi, na ndiyo maana hata na pesa yao mtu kama floyd mayweather mara ngapi umemsikia kaja africa hata kutalii.
Waliporudishwa Liberia waliwauwa wenyeji waliowakuta wao ndio chanzo cha civil war ya Liberia kina Chaz tailor,kina fodey sanko.
Mayweather ametoa Mara nyingi tu kauli chafu za kuwaponda waafrika kwamba sisi ni wavivu ushindi wake ni jitihada zake
 
Back
Top Bottom