Ombi...Tanesco uwanja wa Uhuru unachukua watu 22 elfu tu

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Asilimia kubwa ya wapenda soka kesho tutakua vibanda umiza tukiwaangalia mafundi wa mpira Ajibu,Niyonzima,Kabamba,Kotei kwenye mtanange wa kukata na Shoka baina ya Yanga na Simba pale Uhuru.

Tumeambiwa uwanja wa Uhuru unachukua watu 22 elfu tu na tetesi Tiketi Zimeisha binafsi nimeshampigia Mangi simu aniwekee siti ya mbele pale kibanda umiza chake.

Ila kunufaika na burudani ya kesho Nishati ya Umeme ni muhimu hivyo tunaomba Tanesco kesho mtuachie hii nishati muhimu sisi tucheze na Luku zetu tu.

Asanteni Mpenda Soka mimi
 
sawa hatutazima tumeshafanya research ya kutosha nakuona mtafuatilia kunako runingani kwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…