Glasnost
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 266
- 259
Jukumu moja wapo la chombo cha habari ni kuhabarisha watu wote bila ubaguzi, lakini sio hivyo kwa michezo kama raga, kriketi, mpira wa kikapu, tenisi na aina nyingine. Kwa mda mrefu sasa waandishi wa habari hapa Tanzania wamekuwa wakiupa mchezo wa mpira wa miguu kipaumbele zaidi katika uchambuzi, makala za redioni,magazetini na kwenye runinga.
Upendeleo na “ushabiki” huu mkubwa kutoka kwa wahariri na ufahamu mdogo wa mambo ya michezo wa waandishi wa habari imechangia kukuza tabia ya kutopenda au kufatilia habari zingine za michezo miongoni mwa wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali wa taifa katika kuleta maendeleo ya michezo hapa Tanzania. Kila kiongozi anapotaka kuchangia pesa au kutoa vifaa vya michezo basi mpira wa miguu upewa kipaumbele zaidi na michezo mingine kuachwa bila aina yoyote ya msaada.
Wahariri kukosa maarifa kuhusu habari za michezo kunachangia sana kujenga fikra potofu juu ya michezo mingine na hivyo kujenga taifa lisilopenda michezo zaidi ya mpira wa miguu. Ukinunua gazeti ni nadra sana kukuta habari za michezo zaidi ya mpira wa miguu kupewa nafasi kubwa mbele.
Pia tamaa ya kupata mapato makubwa na wasomaji wengi wa magazeti na mitandao yao ya jamii na hivyo kuacha kufanya kazi kwa misingi ya usawa na haki ya kupata habari. Ni lazima wajue na kutambua umuhimu wa habari zote kwa mwananchi na kwa maendeleo ya michezo nchini.
Mapenzi makubwa ya habari za kimataifa ni janga la taifa sasa hivi. Vyombo vyingi vya habari katika kipindi hichi cha digital age wamekuwa “magwiji” wa uchambuzi wa soka la ulaya na dunia na kusahau kuna michezo mingine inayohitaji ushirika wao katika kuhamasisha na kujenga vijana wa kesho kwenye michezo mbalimbali kama raga, gofu na kriketi.
Ni wakati wao sasa kubadilika na kuanza kuandika habari mbalimbali za michezo na kuzipa kipaumbele ili watoto, vijana na wadau waone umuhimu wa michezo hiyo, jambo litakalo toa vipaji na kukuza jina la nchi kimichezo na kiuchumi kama mataifa mengine. Pia serikali ibadilike katika uhamasishaji na ukuzaji wa michezo mashuleni, kwani ni rahisi kugundua kuwa serikali “inaminya” michezo mingine na kuupa mpira wa miguu kipaumbele zaidi.