Ommy Dimpoz aambulia matusi ni baada ya kupost CCM

Mimi nadhani ushabiki wa vyama unaelekea pabaya,hakuna misingi ya kukosoa na kuiona kweli bali "chuki na angamiza yule"
Kwangu sioni mantiki ya mtu kujenga undugu na chama,jenga undugu na sera za chama tena zinzpokuwa katika maslahi mapana kwako na taifa kwaujumla.

hao wasanii wako kazini wanaweza kuajiriwa na mtu yeyote hata wewe waweza kuwajiri kwenda kumsuta mtu,kutongozea mtu na mambo mengineyo ya hovyo na ya maana.

nadhani ifike wakti tusiwekeane mipaka linapokuja suali la ushabiki wa vyama,hapa zanzibar ujinga huo uliwakuta ,watu walipoteza ajira,kufirisika,kushitakiwa bila haki,kupeana talaka ,undugu kufa kwa ujinaga wa huyu ccm yule cuf.

Ilifika wakati hata Mwenyezi Mungu walimkata mapande,huu msikiti wa ccm huu wa cuf!

Ndugu zangu tufanye siasa na akili timamu hizi ni propaganda za chuktena i za kijinga kabisa tuziache tafadhali-usimhukumu mtu kwa kuwa tu anaamini kitu ambacho wewe hukiamini zipo njia sahihi za kumpinga-kwenye uchaguzi sio kuchafuana kipuuzi tu.
 
124 Ali;

siasa za Tanzania hazijakomaa kiasi hicho, bado ni disko toto
 
Last edited by a moderator:
Alaf jamaa kafulia kimziki now dayz..

Nae ni star wa instagram tu kwa sasa..
 

Huu ni mtazamo wako dhaifu, like ni matakwa ya mashabiki, huwezi kulazimisha hilo. Kuna ubaya gani akipost post inayohusiana na wale waliomwalika?
 
Njaa bora iishie tumboni lakini ikipanda kichwani inakuwa na madhara makubwa sana....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…